Barua ya wazi kwa Mtume Mohammad (S A W)

Barua ya wazi kwa Mtume Mohammad (S A W)

Mkuu Al mukheef, nimeomba jambo gani hapo kwa mtume linalohodhi mamlaka ya Allah?

Hayo ni kama mazungumzo ya kufikirika tu kwamba, ikitokea umekutana na mtume utampasha habari gani?

ndio Mwandishi akaanza kusimulia historia ya dola tangu alipoondoka, na hali ya kijamii ilivyo sasa, largely ni maelezo na sio maombi kama unasoma vizuri.

Ombi hapo kwa mtume ni kutuombea huruma kwa Allah basi, kwa vile yeye ni bora mbele ya Allah kuliko sisi...sasa swali kwako mwana Tawheed, je mtume akienda kutuombea huruma kwa mola wake, Allah atakataaa katukatu?
Akuombee nini wakati kila siku mnamsalia,ni maiti hiyo ishaoza na kuvunda
 
Nimetaja neno ghaibu kabla ya wewe kuingiza habari za yesu
Sasa nakujibu rasmi ni kosa kumuomba uombezi kiumbe aliyopo kwenye ghaibu ikiwa ni malaika,jini au binadamu
Kwa hiyo mitume na manabii inatakiwa wao ndiyo watuombe sisi tuwa ombee uombezi kwa ALLAH 😁😁😁😁😁 HIKI NI KITUKO KAMA CHA MAKANISA NAO WANADAI 👉 WANAMBARIKI MUNGU 😁😁JE MUNGU ABARIKIWE NA KIUMBE WAKE KWA LIPI ?😁😁😁😁😁😁
 
Barua inamfikiaje na kama anaona kila kitu hata bila kuandika si anaweza hata kusoma mawazo yako hivyo hakuna haja ya kuandika ?

Unless unawaandikia wadau wenzako
 
Kwa hiyo mitume na manabii inatakiwa wao ndiyo watuombe sisi tuwa ombee uombezi kwa ALLAH 😁😁😁😁😁 HIKI NI KITUKO KAMA CHA MAKANISA NAO WANADAI 👉 WANAMBARIKI MUNGU 😁😁JE MUNGU ABARIKIWE NA KIUMBE WAKE KWA LIPI ?😁😁😁😁😁😁
Ya kanisani hayanihusu muhimu nimeshakujibu
 
As-salatu na salam, ewe Rasul wa Rahma,
Nuru yako bado inang’aa, hata karne zikipita,
Tumekuletea kilio cha Umma, kutoka Tanganyika hadi Gaza,
Kwamba hatuwezi tena kuishi bila mwongozo wako.

Baada yako, Bakr al-Siddiq aliweka msingi,
ʿUmar akaleta adili, ʿUthmān mnyenyekevu, ʿAlī jasiri,
Baada yao, Umawi wakapanua nchi,

Abbasiyyu wakaleta hekma, vitabu, na elimu,
Uthmani wakashika haramain kwa karne nyingi,
Salahuddin al-Ayyubi akalinda Baytul-Maqdis kwa upendo na rehema.

Lakini leo, ewe Mtume, tuangalie,

Umma wako umetawanyika, viongozi wamesahaulika,
Umoja umepotea, maovu yametanda kila kona,
Tunalia kwa machozi, tukikosa kiongozi wa kweli.

Enzi zako kijana akioa, leo tusubiri degree Mlimani,

Kwanza mali, kazi, kisha ndoa,
Miaka ya kusubiri, tukishindwa, zina inatanda,
Zina rahisi kuliko chakula, kila kona ni hatari.

Mbagala, ngoma za jadi zinasindikwa kwa uchi,

Wazee wetu hawakuviona hivi.
Je kuna Mtume mwingine atakuja,
Au tumeachwa pekee, tukipapasa giza?

Bakwata wanashindana na Ansarī,

Salafi wakilaumu masufi, kila mmoja akidai Sunna.

Mama Samia anaongoza, kiongozi wa taifa letu,

Lakini Salafi wakihoji, “Hii si Sunna yetu",
Wakimkataa, ewe Mtume, nani atasimamia Umma?
Je hawaoni fursa katikati ya manyanyaso ya kisiasa?

Lakini hatuwezi kusimama, nafasi hii ni mwanga,

Hata kama wanapinga, Umma unahitaji mwongozo wa kweli,
Tukiacha fursa, hatutaona njia,
Tukizizika tofauti, tunaweza kuungana na kumlinda.

Mazinge amesalimisha wengi, akiongoza pamoja na Dr Sulle,

Lakini watu wanamuita mganga mshirikina, je, Mtume,
Sulle ataenda peponi kwa kuwasilimisha waliokuwa wamekufuru,
Au ataangukia motoni kwa ilimu yake ya kisufi?

Othman Maalim, Salafi wanamzonga kwa kuponda nyoyo za kina mama,

Ewe Mtume, je Othman ataenda motoni kwa daawa yake laini
Au ataenda peponi kwa kumpa moyo rastamani, aendelee na sala akiwa amesuka?

Bidaa imeenea, Kassim Mafuta anaona ni upotevu,

Lakini Mtume, kwa mtazamo wako, bid‘a ni nini?
Katika kumtaja Allah, kusoma Qur’ān na kukuswalia?,
Je, hiii ni dhambi, au ni nuru kwa Umma wa sasa?

Pia, ewe Mtume, balaa la ushoga limeenea,

Wazungu waletea Afrika, wakifadhili shule na walimu.
Watoto wakidhihirishwa usagaji, kemikali zikaharibu fitra,
Ewe Mtume, ikiwa mtu apewa hii, je hii ni adhabu au umma ndo wamchokoza Allah?

Ulisema kila ugonjwa una tiba,

Lakini leo HIV unaua kimya kimya,
Familia zikivunjika, kizazi kikipotea,
Ewe Habib, tiba yake iko wapi?

Gaza inavuja damu kila siku, watoto wakiwa chini ya vifusi,

Mama wakiomba mbinguni, huku Makkah na Madinah kimya,
Je watu wa Kisemvule waililie Gaza?
Wakati Walinzi wa Haramain wako tulivu na kimya?

Ewe Habib, umma wako umechoka,

Sunna yako twaihubiri bila kuishi, Qur’ān twasoma bila kuelewa.
Tunasali kwako, tutumie shufaa yako mbele ya Arshi,
Allah atusamehe, aturudishe njia ya Madinah,
Atutakase, atuunganishe, atuinue kutoka fedheha.

Salam kwako, ewe Mtume,

Salam juu ya Ahli Beyti na Sahaba zako,
Twasubiri shufaa yako, na tumaini letu liwe kwa Allah,
Rehema isiyo na kikomo.

YUSUFU R H SABURA
0750883466
Uandishi Mujarab..👍
Umenikumbusha riwaya za zamani, 'Alfu lela U lela'
Ni nadra sana kuona uandishi wa namna hii nyakati hizi.

Kuhusu maudhui ya ulichokiandika, ninakushauri simama na unachokiamini.
 
Ubunifu ni kitu kizuri ila ukileta ubunifu kwenye uislamu matokeo ndo haya, aaamyn.
Naam. Allah Atuongoze sote sisi na huyu ndugu yetu katika njia iliyonyooka na Atuhifadhi na Atufishe katika Tawheed na Sunnah.

Ombi hapo kwa mtume ni kutuombea huruma kwa Allah basi, kwa vile yeye ni bora mbele ya Allah kuliko sisi...sasa swali kwako mwana Tawheed, je mtume akienda kutuombea huruma kwa mola wake, Allah atakataaa katukatu?
Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) hakusikii hili. Yuko kaburini kwake na yuko katika barzakh hajui kinachoendelea huku Duniani. Kuombea kwa Allah ataombea Siku ya Qiyama akiwa kashafufuliwa. Achana na hili jambo ni hatari mno. Una malalamiko yako yamekukaba kwelikweli basi Muombe Allah Moja kwa Moja, usimuombe Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake)
Mtume katufundisha kumuomba Allah Peke yake.

Soma Hadith hii ifuatayo;

‘Kutoka kwa Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allahu ‘anhumaa) amesema: Siku moja nilikuwa nyuma ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) (juu ya mnyama). Akaniambia: “Ee kijana, mimi nitakufundisha maneno: Mhifadhi Allah Naye Atakuhifadhi. Mhifadhi Allah utamkuta yupo mbele yako. Unapoomba, muombe Allah. Unapotaka msaada, mtake Allah. Fahamu kuwa, lau ummah (wote) utajikusanya ili wakunufaishe kwa jambo, basi hawataweza kukunufaisha ila kwa jambo Alilokuandikia Allah; na wakijumuika ila wakudhuru kwa jambo, hawataweza kukudhuru ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah. Kalamu zimeshasimama na karatasi zimeshakauka.”

[At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh]

Riwaayah nyingine isiyokuwa ya At-Tirmidhiy imesema:

“Mhifadhi Allah utamkuta Yupo mbele yako. Mjue Allah katika raha Naye Atakujua katika shida. Ujue kuwa, lililokukosa halikuwa ni lenye kukupata, na lililokusibu halikuwa ni lenye kukukosa. Ujue kuwa nusura ipo pamoja na subira, faraja ipo pamoja na dhiki, na kwenye uzito kuna wepesi.

Hivyo ndivyo alivyofundisha Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake).

Haifai kumuomba yoyote katika lile analiweza Allah Peke yake.

Na hata yale ambayo Allah kawapa viumbe uwezo juu yake, haifai kuwaomba wasiokuwepo au wasioonekana kama waliofariki, au aliye hai lakini hakusikii au yuko mbali na wewe. Mfano unapigwa au umekwama kitu (mfano gari imekwama) na kuna mtu pembeni ukamuambia "naomba unisaidie ndugu yangu" hiyo yafaa, lakini amekufa huyo mtu au hayupo hapo halafu umepata shida kisha ukamuita ukimtaka msaada haifai.

Haifai kuomba Dua kwa yoyote isipokuwa kwa Allah. Dua zote zinaelekezwa kwa Allah.

Unaweza kumuambia mtu mwema aliye hai na yupo na anakusikia ukamuambia akuombee Dua kwa Allah. Lakini akifa au akiwa hayupo na hakusikii haifai kumuambia akuombee Dua kwa Allah.

Wakati Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) yupo hai watu walikuwa wakimfuata na kumuomba awaombee Dua kwa Allah, mfano amuombe Allah awanyeshelezee mvua na Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) akiomba Dua kwa Allah.

Ila baada ya kufariki Mtume (Swala na salamu ziwe juu yake) hawakuwa wakienda kwenye kaburi yake kumuambia awaombee Dua, sikuambii wakiwa popote pale. Wala hawakuwa wakimuomba awafanyie hata yale ambayo alipokuwa hai aliweza kuyafanya. Hawakufanya hivyo kwa sababu imekatazwa.

Hayo ni kama mazungumzo ya kufikirika tu kwamba, ikitokea umekutana na mtume utampasha habari gani?

ndio Mwandishi akaanza kusimulia historia ya dola tangu alipoondoka, na hali ya kijamii ilivyo sasa, largely ni maelezo na sio maombi kama unasoma vizuri.

Maswahaba (Allah Awaridhie) walipitia shida nyingi na mitihani mingi baada ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) lakini haikupokelewa kutoka kwao kuwa walikuwa wakilia kwa Mtume au kumuandikia barua za malalamiko au kumuandikia "mazungumzo ya kufikirika". Na hao ndio watu bora zaidi katika Ummah huu baada ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) na walimpenda zaidi na walikuwa na pupa zaidi ya kumfuata, bali tumeamrishwa tufuate njia yao.

Walifuata maagizo aliyowapa alipokuwa hai. Na hata walipokhitilafiana walirudisha mambo yao katika Kitabu cha Allah na Sunnah ya Mtume wake kama walivyoamrishwa katika Qur’ān (4:59) Mtume alipokuwa hai walikuwa wakikhitilafiana jambo wanarudi kwake kumuuliza, alipofariki wakawa wanarudi katika mafundisho yake. Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) alipokaribia kuondoka aliwausia wafuate Sunnah yake na Sunnah za Makhalifa wake waongofu baada yake na wazikamate kwa magego yao (washikamane nazo Barabara wasiziachie). Na walifanya hivyo.

Hakuna yoyote katika Makhalifa waongofu (Abu Bakr, 'Umar, 'Uthmaan wala 'Ali) alipopitia mitihani na changamoto alipeleka malalamiko yake kwa Mtume au kufanya naye "mazungumzo ya kufikirika" na hawa ndio watu bora zaidi baada ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) ambao tumeamrishwa kufuata mwenendo wao. Wala hakuna yoyote katika waliobakia katika wale waliobashiriwa Pepo wakiwa hai alifanya hivyo, wala yeyote katika watu wa nyumba ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) ikiwemo wake zake aliyefanya hivyo wala yeyote mwengine katika Maswahaba wa Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake). Allah Awaridhie Maswahaba wote wa Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake).

Wewe ndugu yangu ni nani kakutangulia katika hili?

Achana na hilo jambo. Ni hatari mnoo.
 
Naam. Allah Atuongoze sote sisi na huyu ndugu yetu katika njia iliyonyooka na Atuhifadhi na Atufishe katika Tawheed na Sunnah.

Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) hakusikii hili. Yuko kaburini kwake na yuko katika barzakh hajui kinachoendelea huku Duniani. Kuombea kwa Allah ataombea Siku ya Qiyama akiwa kashafufuliwa. Achana na hili jambo ni hatari mno. Una malalamiko yako yamekukaba kwelikweli basi Muombe Allah Moja kwa Moja, usimuombe Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake)
Mtume katufundisha kumuomba Allah Peke yake.

Soma Hadith hii ifuatayo;

‘Kutoka kwa Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allahu ‘anhumaa) amesema: Siku moja nilikuwa nyuma ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) (juu ya mnyama). Akaniambia: “Ee kijana, mimi nitakufundisha maneno: Mhifadhi Allah Naye Atakuhifadhi. Mhifadhi Allah utamkuta yupo mbele yako. Unapoomba, muombe Allah. Unapotaka msaada, mtake Allah. Fahamu kuwa, lau ummah (wote) utajikusanya ili wakunufaishe kwa jambo, basi hawataweza kukunufaisha ila kwa jambo Alilokuandikia Allah; na wakijumuika ila wakudhuru kwa jambo, hawataweza kukudhuru ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah. Kalamu zimeshasimama na karatasi zimeshakauka.”

[At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh]

Riwaayah nyingine isiyokuwa ya At-Tirmidhiy imesema:

“Mhifadhi Allah utamkuta Yupo mbele yako. Mjue Allah katika raha Naye Atakujua katika shida. Ujue kuwa, lililokukosa halikuwa ni lenye kukupata, na lililokusibu halikuwa ni lenye kukukosa. Ujue kuwa nusura ipo pamoja na subira, faraja ipo pamoja na dhiki, na kwenye uzito kuna wepesi.

Hivyo ndivyo alivyofundisha Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake).

Haifai kumuomba yoyote katika lile analiweza Allah Peke yake.

Na hata yale ambayo Allah kawapa viumbe uwezo juu yake, haifai kuwaomba wasiokuwepo au wasioonekana kama waliofariki, au aliye hai lakini hakusikii au yuko mbali na wewe. Mfano unapigwa au umekwama kitu (mfano gari imekwama) na kuna mtu pembeni ukamuambia "naomba unisaidie ndugu yangu" hiyo yafaa, lakini amekufa huyo mtu au hayupo hapo halafu umepata shida kisha ukamuita ukimtaka msaada haifai.

Haifai kuomba Dua kwa yoyote isipokuwa kwa Allah. Dua zote zinaelekezwa kwa Allah.

Unaweza kumuambia mtu mwema aliye hai na yupo na anakusikia ukamuambia akuombee Dua kwa Allah. Lakini akifa au akiwa hayupo na hakusikii haifai kumuambia akuombee Dua kwa Allah.

Wakati Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) yupo hai watu walikuwa wakimfuata na kumuomba awaombee Dua kwa Allah, mfano amuombe Allah awanyeshelezee mvua na Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) akiomba Dua kwa Allah.

Ila baada ya kufariki Mtume (Swala na salamu ziwe juu yake) hawakuwa wakienda kwenye kaburi yake kumuambia awaombee Dua, sikuambii wakiwa popote pale. Wala hawakuwa wakimuomba awafanyie hata yale ambayo alipokuwa hai aliweza kuyafanya. Hawakufanya hivyo kwa sababu imekatazwa.

Maswahaba (Allah Awaridhie) walipitia shida nyingi na mitihani mingi baada ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) lakini haikupokelewa kutoka kwao kuwa walikuwa wakilia kwa Mtume au kumuandikia barua za malalamiko au kumuandikia "mazungumzo ya kufikirika". Na hao ndio watu bora zaidi katika Ummah huu baada ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) na walimpenda zaidi na walikuwa na pupa zaidi ya kumfuata, bali tumeamrishwa tufuate njia yao.

Walifuata maagizo aliyowapa alipokuwa hai. Na hata walipokhitilafiana walirudisha mambo yao katika Kitabu cha Allah na Sunnah ya Mtume wake kama walivyoamrishwa katika Qur’ān (4:59) Mtume alipokuwa hai.walikuwa wakikhitilafiana jambo wanarudi kwake kumuuliza, alipofariki wakawa wanarudi katika mafundisho yake. Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) alipokaribia kuondoka aliwausia wafuate Sunnah yake na Sunnah za Makhalifa wake waongofu baada yake na wazikamate kwa magego yao (washikamane nazo Barbara wasiziachie). Na walifanya hivyo

Hakuna yoyote katika Makhalifa waongofu (Abu Bakr, 'Umar, 'Uthmaan wala 'Ali) alipopitia mitihani na changamoto alipeleka malalamiko yake kwa Mtume au kufanya naye "mazungumzo ya kufikirika" na hawa ndio watu bora zaidi baada ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) ambao tumeamrishwa kufuata mwenendo wao. Wala hakuna yoyote katika waliobakia katika wale waliobashiriwa Pepo wakiwa hai alifanya hivyo, wala yeyote katika watu wa nyumba ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) ikiwemo wake zake waliofanya hivyo wala yeyote mwengine katika Maswahaba wa Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake). Allah Awaridhie Maswahaba wote wa Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake).

Wewe ndugu yangu ni nani kakutangulia katika hili.

Achana na hilo jambo. Ni hatari mnoo.
Wallahi umefikisha na umetosheleza, huyu mwandishi wa hiyo barua imma ameamua kufungua mlango wa upotevu au amegundua njia bora kuliko njia ya mtume muhammad swala na amani ziwe juu yake.

Allah akulipe kheri na akuzidishie maarifa shekhe Baljurashi
 
Allahumma Aamiin. Mimi sio Shekhe ndugu yangu mkarimu, mimi ni mwanafunzi mdogo tu katika Waislam. Allah Atuzidishie maarifa sote.
 
Hadith 28, 40 Hadith an-Nawawi
On the authority of Abu Najeeh al-’Irbaad ibn Saariyah (may Allah be pleased with him) who said:
The Messenger of Allah (peace and blessings of Allah be upon him) gave us a sermon by which our hearts were filled with fear and tears came to our eyes. So we said, “O Messenger of Allah! It is as though this is a farewell sermon, so counsel us.” He (peace and blessings of Allah be upon him) said, “I counsel you to have taqwa (fear) of Allah, and to listen and obey [your leader], even if a slave were to become your ameer. Verily he among you who lives long will see great controversy, so you must keep to my Sunnah and to the Sunnah of the Khulafa ar-Rashideen (the rightly guided caliphs), those who guide to the right way. Cling to it stubbornly [literally: with your molar teeth]. Beware of newly invented matters [in the religion], for verily every bidah (innovation) is misguidance.”

[Abu Dawud]
It was related by at-Tirmidhi, who said that it was a good and sound hadeeth.

عَنْ أَبِي نَجِيحٍ الْعِرْبَاضِ بْنِ سَارِيَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: "وَعَظَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم مَوْعِظَةً وَجِلَتْ مِنْهَا الْقُلُوبُ، وَذَرَفَتْ مِنْهَا الْعُيُونُ، فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اللَّهِ! كَأَنَّهَا مَوْعِظَةُ مُوَدِّعٍ فَأَوْصِنَا، قَالَ: أُوصِيكُمْ بِتَقْوَى اللَّهِ، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ وَإِنْ تَأَمَّرَ عَلَيْكُمْ عَبْدٌ، فَإِنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيَرَى اخْتِلَافًا كَثِيرًا، فَعَلَيْكُمْ بِسُنَّتِي وَسُنَّةِ الْخُلَفَاءِ الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيينَ، عَضُّوا عَلَيْهَا بِالنَّوَاجِذِ، وَإِيَّاكُمْ وَمُحْدَثَاتِ الْأُمُورِ؛ فَإِنَّ كُلَّ بِدْعَةٍ ضَلَالَةٌ". [رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ]، وَاَلتِّرْمِذِيُّ [رقم:266] وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
 
Mkuu sasa huyo Allah mwenyewe anamtegemea Muddy.

Hapa mwarubauni na wakutegemewa NI kipenzi chetu cha dhati mwamba mkombozi wa waislamu Imam Hussain ibn Ali AS aliyeuwawa kikatili kuutetea kuulinda na kuupigania uislamu. Kupitia yeye tumepewa tawfiq/tawfeek the ability to win and succeed na tuna uhakika wa jannah na firdaus.

Mcheki mwamba hapo Chini akichanja mbuga kuelekea Karbala kuutetea, kuulinda kuupigania uislamu dhidi ya dhulma ukandamizaji unyanyasaji na uonevu akiwa juu ya Zuljanah.

View attachment 3448900

adriz Jagina Dabil Nyamwi255

KAPATA LIFT YA RAFIKI YAKE ; ANAENDA KUONYESHWA MIJI, ANAMTEGEMEA SHETANI KUPATA LIFT

1755952764083.jpeg
 
Back
Top Bottom