Barua ya wazi kwa Mtume Mohammad (S A W)

Barua ya wazi kwa Mtume Mohammad (S A W)

Sijui umeandika vitu gani mtume muhammad swala na amani ziwe juu yake yupo kaburini kwake wala hajui jamiiforums ni nini, Allah atupe maarifa na atuongoze njia ya sawa.
karibu, unashauri niipeleke barua kaburini kwake ama? elimu yako tafadhali?
 
Ungemuomba Allah na sio kumuomba binadamu mwenzako ambaye hawezi kuleta manufaa wala madhara
Mkuu Al mukheef, nimeomba jambo gani hapo kwa mtume linalohodhi mamlaka ya Allah?

Hayo ni kama mazungumzo ya kufikirika tu kwamba, ikitokea umekutana na mtume utampasha habari gani?

ndio Mwandishi akaanza kusimulia historia ya dola tangu alipoondoka, na hali ya kijamii ilivyo sasa, largely ni maelezo na sio maombi kama unasoma vizuri.

Ombi hapo kwa mtume ni kutuombea huruma kwa Allah basi, kwa vile yeye ni bora mbele ya Allah kuliko sisi...sasa swali kwako mwana Tawheed, je mtume akienda kutuombea huruma kwa mola wake, Allah atakataaa katukatu?
 
Unapeleka ujumbe kwa mtu aliyekufa kifo kama cha babu yako na unayemswalia kila siku kwa allah?Gaza gaza kwani Congo,Sudan hukuoni?
 
As-salatu na salam, ewe Rasul wa Rahma,
Nuru yako bado inang’aa, hata karne zikipita,
Tumekuletea kilio cha Umma, kutoka Tanganyika hadi Gaza,
Kwamba hatuwezi tena kuishi bila mwongozo wako.

Baada yako, Bakr al-Siddiq aliweka msingi,
ʿUmar akaleta adili, ʿUthmān mnyenyekevu, ʿAlī jasiri,
Baada yao, Umawi wakapanua nchi,

Abbasiyyu wakaleta hekma, vitabu, na elimu,
Uthmani wakashika haramain kwa karne nyingi,
Salahuddin al-Ayyubi akalinda Baytul-Maqdis kwa upendo na rehema.

Lakini leo, ewe Mtume, tuangalie,

Umma wako umetawanyika, viongozi wamesahaulika,
Umoja umepotea, maovu yametanda kila kona,
Tunalia kwa machozi, tukikosa kiongozi wa kweli.

Enzi zako kijana akioa, leo tusubiri degree Mlimani,

Kwanza mali, kazi, kisha ndoa,
Miaka ya kusubiri, tukishindwa, zina inatanda,
Zina rahisi kuliko chakula, kila kona ni hatari.

Mbagala, ngoma za jadi zinasindikwa kwa uchi,

Wazee wetu hawakuviona hivi.
Je kuna Mtume mwingine atakuja,
Au tumeachwa pekee, tukipapasa giza?

Bakwata wanashindana na Ansarī,

Salafi wakilaumu masufi, kila mmoja akidai Sunna.

Mama Samia anaongoza, kiongozi wa taifa letu,

Lakini Salafi wakihoji, “Hii si Sunna yetu",
Wakimkataa, ewe Mtume, nani atasimamia Umma?
Je hawaoni fursa katikati ya manyanyaso ya kisiasa?

Lakini hatuwezi kusimama, nafasi hii ni mwanga,

Hata kama wanapinga, Umma unahitaji mwongozo wa kweli,
Tukiacha fursa, hatutaona njia,
Tukizizika tofauti, tunaweza kuungana na kumlinda.

Mazinge amesalimisha wengi, akiongoza pamoja na Dr Sulle,

Lakini watu wanamuita mganga mshirikina, je, Mtume,
Sulle ataenda peponi kwa kuwasilimisha waliokuwa wamekufuru,
Au ataangukia motoni kwa ilimu yake ya kisufi?

Othman Maalim, Salafi wanamzonga kwa kuponda nyoyo za kina mama,

Ewe Mtume, je Othman ataenda motoni kwa daawa yake laini
Au ataenda peponi kwa kumpa moyo rastamani, aendelee na sala akiwa amesuka?

Bidaa imeenea, Kassim Mafuta anaona ni upotevu,

Lakini Mtume, kwa mtazamo wako, bid‘a ni nini?
Katika kumtaja Allah, kusoma Qur’ān na kukuswalia?,
Je, hiii ni dhambi, au ni nuru kwa Umma wa sasa?

Pia, ewe Mtume, balaa la ushoga limeenea,

Wazungu waletea Afrika, wakifadhili shule na walimu.
Watoto wakidhihirishwa usagaji, kemikali zikaharibu fitra,
Ewe Mtume, ikiwa mtu apewa hii, je hii ni adhabu au umma ndo wamchokoza Allah?

Ulisema kila ugonjwa una tiba,

Lakini leo HIV unaua kimya kimya,
Familia zikivunjika, kizazi kikipotea,
Ewe Habib, tiba yake iko wapi?

Gaza inavuja damu kila siku, watoto wakiwa chini ya vifusi,

Mama wakiomba mbinguni, huku Makkah na Madinah kimya,
Je watu wa Kisemvule waililie Gaza?
Wakati Walinzi wa Haramain wako tulivu na kimya?

Ewe Habib, umma wako umechoka,

Sunna yako twaihubiri bila kuishi, Qur’ān twasoma bila kuelewa.
Tunasali kwako, tutumie shufaa yako mbele ya Arshi,
Allah atusamehe, aturudishe njia ya Madinah,
Atutakase, atuunganishe, atuinue kutoka fedheha.

Salam kwako, ewe Mtume,

Salam juu ya Ahli Beyti na Sahaba zako,
Twasubiri shufaa yako, na tumaini letu liwe kwa Allah,
Rehema isiyo na kikomo.

YUSUFU R H SABURA
0750883466
Kwani ujui mimi mtume wako ni mzoga nipo kaburini kitambo 🥲🥲 du ile Sumu ya kahaba wa kiyahudi iliyo niua ilikuwa kali sana ...endeleeni kuniombea kwa kuniswalia labda nitafufuka .
@AI-mukheef
 
Kwa sasa hana uwezo wa kutuombea ila mpaka siku ya kiama
Kiufupi kumuomba Mtume akuombee kwa Allah ni shirk
Wewe badili jina linashindikana kutagiwa ...unakosa elimu ya dini niliyo wapa wenzio kwa kuwatag
@AI-mukheef
 
Ungemuomba Allah na sio kumuomba binadamu mwenzako ambaye hawezi kuleta manufaa wala madhara
Mkuu sasa huyo Allah mwenyewe anamtegemea Muddy.

Hapa mwarubauni na wakutegemewa NI kipenzi chetu cha dhati mwamba mkombozi wa waislamu Imam Hussain ibn Ali AS aliyeuwawa kikatili kuutetea kuulinda na kuupigania uislamu. Kupitia yeye tumepewa tawfiq/tawfeek the ability to win and succeed na tuna uhakika wa jannah na firdaus.

Mcheki mwamba hapo Chini akichanja mbuga kuelekea Karbala kuutetea, kuulinda kuupigania uislamu dhidi ya dhulma ukandamizaji unyanyasaji na uonevu akiwa juu ya Zuljanah.

Screenshot_2025-07-09-18-01-08-90_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12~2.jpg


adriz Jagina Dabil Nyamwi255
 
Hapa issue ni kumuomba akuombee kwa Allah
Mbona yeye naye kawaomba waislamu mmuombee kwa Allah? Yaani mtume mzima iwe ni sawa kuwaomba waislamu kumuombea yeye ila iwe haramu kwa mfuasi wa huyo mtume kumuomba huyo mtume kumuombea yeye kwa Allah 🙄🙄
 
As-salatu na salam, ewe Rasul wa Rahma,
Nuru yako bado inang’aa, hata karne zikipita,
Tumekuletea kilio cha Umma, kutoka Tanganyika hadi Gaza,
Kwamba hatuwezi tena kuishi bila mwongozo wako.

Baada yako, Bakr al-Siddiq aliweka msingi,
ʿUmar akaleta adili, ʿUthmān mnyenyekevu, ʿAlī jasiri,
Baada yao, Umawi wakapanua nchi,

Abbasiyyu wakaleta hekma, vitabu, na elimu,
Uthmani wakashika haramain kwa karne nyingi,
Salahuddin al-Ayyubi akalinda Baytul-Maqdis kwa upendo na rehema.

Lakini leo, ewe Mtume, tuangalie,

Umma wako umetawanyika, viongozi wamesahaulika,
Umoja umepotea, maovu yametanda kila kona,
Tunalia kwa machozi, tukikosa kiongozi wa kweli.

Enzi zako kijana akioa, leo tusubiri degree Mlimani,

Kwanza mali, kazi, kisha ndoa,
Miaka ya kusubiri, tukishindwa, zina inatanda,
Zina rahisi kuliko chakula, kila kona ni hatari.

Mbagala, ngoma za jadi zinasindikwa kwa uchi,

Wazee wetu hawakuviona hivi.
Je kuna Mtume mwingine atakuja,
Au tumeachwa pekee, tukipapasa giza?

Bakwata wanashindana na Ansarī,

Salafi wakilaumu masufi, kila mmoja akidai Sunna.

Mama Samia anaongoza, kiongozi wa taifa letu,

Lakini Salafi wakihoji, “Hii si Sunna yetu",
Wakimkataa, ewe Mtume, nani atasimamia Umma?
Je hawaoni fursa katikati ya manyanyaso ya kisiasa?

Lakini hatuwezi kusimama, nafasi hii ni mwanga,

Hata kama wanapinga, Umma unahitaji mwongozo wa kweli,
Tukiacha fursa, hatutaona njia,
Tukizizika tofauti, tunaweza kuungana na kumlinda.

Mazinge amesalimisha wengi, akiongoza pamoja na Dr Sulle,

Lakini watu wanamuita mganga mshirikina, je, Mtume,
Sulle ataenda peponi kwa kuwasilimisha waliokuwa wamekufuru,
Au ataangukia motoni kwa ilimu yake ya kisufi?

Othman Maalim, Salafi wanamzonga kwa kuponda nyoyo za kina mama,

Ewe Mtume, je Othman ataenda motoni kwa daawa yake laini
Au ataenda peponi kwa kumpa moyo rastamani, aendelee na sala akiwa amesuka?

Bidaa imeenea, Kassim Mafuta anaona ni upotevu,

Lakini Mtume, kwa mtazamo wako, bid‘a ni nini?
Katika kumtaja Allah, kusoma Qur’ān na kukuswalia?,
Je, hiii ni dhambi, au ni nuru kwa Umma wa sasa?

Pia, ewe Mtume, balaa la ushoga limeenea,

Wazungu waletea Afrika, wakifadhili shule na walimu.
Watoto wakidhihirishwa usagaji, kemikali zikaharibu fitra,
Ewe Mtume, ikiwa mtu apewa hii, je hii ni adhabu au umma ndo wamchokoza Allah?

Ulisema kila ugonjwa una tiba,

Lakini leo HIV unaua kimya kimya,
Familia zikivunjika, kizazi kikipotea,
Ewe Habib, tiba yake iko wapi?

Gaza inavuja damu kila siku, watoto wakiwa chini ya vifusi,

Mama wakiomba mbinguni, huku Makkah na Madinah kimya,
Je watu wa Kisemvule waililie Gaza?
Wakati Walinzi wa Haramain wako tulivu na kimya?

Ewe Habib, umma wako umechoka,

Sunna yako twaihubiri bila kuishi, Qur’ān twasoma bila kuelewa.
Tunasali kwako, tutumie shufaa yako mbele ya Arshi,
Allah atusamehe, aturudishe njia ya Madinah,
Atutakase, atuunganishe, atuinue kutoka fedheha.

Salam kwako, ewe Mtume,

Salam juu ya Ahli Beyti na Sahaba zako,
Twasubiri shufaa yako, na tumaini letu liwe kwa Allah,
Rehema isiyo na kikomo.

YUSUFU R H SABURA
0750883466


Hii haifai.
 
Mbona yeye naye kawaomba waislamu mmuombee kwa Allah? Yaani mtume mzima iwe ni sawa kuwaomba waislamu kumuombea yeye ila iwe haramu kwa mfuasi wa huyo mtume kumuomba huyo mtume kumuombea yeye kwa Allah 🙄🙄
Kwani sisi tumekufa
 
Kwani sisi tumekufa
Muhammad kasema mtu akifa bado anakuwa hai ....hata kaburini anaulizwa maswali na kujibu na akifanikiwa kuyajibu vema anakuwa mbali na adhabu ya kaburi sasa kama ni hai kwanini asiombwe ?
 
Back
Top Bottom