Yusufu R H Sabura
JF-Expert Member
- Jun 26, 2020
- 740
- 828
As-salatu na salam, ewe Rasul wa Rahma,
Nuru yako bado inang’aa, hata karne zikipita,
Tumekuletea kilio cha Umma, kutoka Tanganyika hadi Gaza,
Kwamba hatuwezi tena kuishi bila mwongozo wako.
Baada yako, Bakr al-Siddiq aliweka msingi,
ʿUmar akaleta adili, ʿUthmān mnyenyekevu, ʿAlī jasiri,
Baada yao, Umawi wakapanua nchi,
Abbasiyyu wakaleta hekma, vitabu, na elimu,
Uthmani wakashika haramain kwa karne nyingi,
Salahuddin al-Ayyubi akalinda Baytul-Maqdis kwa upendo na rehema.
Lakini leo, ewe Mtume, tuangalie,
Umma wako umetawanyika, viongozi wamesahaulika,
Umoja umepotea, maovu yametanda kila kona,
Tunalia kwa machozi, tukikosa kiongozi wa kweli.
Enzi zako kijana akioa, leo tusubiri degree Mlimani,
Kwanza mali, kazi, kisha ndoa,
Miaka ya kusubiri, tukishindwa, zina inatanda,
Zina rahisi kuliko chakula, kila kona ni hatari.
Mbagala, ngoma za jadi zinasindikwa kwa uchi,
Wazee wetu hawakuviona hivi.
Je kuna Mtume mwingine atakuja,
Au tumeachwa pekee, tukipapasa giza?
Bakwata wanashindana na Ansarī,
Salafi wakilaumu masufi, kila mmoja akidai Sunna.
Mama Samia anaongoza, kiongozi wa taifa letu,
Lakini Salafi wakihoji, “Hii si Sunna yetu",
Wakimkataa, ewe Mtume, nani atasimamia Umma?
Je hawaoni fursa katikati ya manyanyaso ya kisiasa?
Lakini hatuwezi kusimama, nafasi hii ni mwanga,
Hata kama wanapinga, Umma unahitaji mwongozo wa kweli,
Tukiacha fursa, hatutaona njia,
Tukizizika tofauti, tunaweza kuungana na kumlinda.
Mazinge amesalimisha wengi, akiongoza pamoja na Dr Sulle,
Lakini watu wanamuita mganga mshirikina, je, Mtume,
Sulle ataenda peponi kwa kuwasilimisha waliokuwa wamekufuru,
Au ataangukia motoni kwa ilimu yake ya kisufi?
Othman Maalim, Salafi wanamzonga kwa kuponda nyoyo za kina mama,
Ewe Mtume, je Othman ataenda motoni kwa daawa yake laini
Au ataenda peponi kwa kumpa moyo rastamani, aendelee na sala akiwa amesuka?
Bidaa imeenea, Kassim Mafuta anaona ni upotevu,
Lakini Mtume, kwa mtazamo wako, bid‘a ni nini?
Katika kumtaja Allah, kusoma Qur’ān na kukuswalia?,
Je, hiii ni dhambi, au ni nuru kwa Umma wa sasa?
Pia, ewe Mtume, balaa la ushoga limeenea,
Wazungu waletea Afrika, wakifadhili shule na walimu.
Watoto wakidhihirishwa usagaji, kemikali zikaharibu fitra,
Ewe Mtume, ikiwa mtu apewa hii, je hii ni adhabu au umma ndo wamchokoza Allah?
Ulisema kila ugonjwa una tiba,
Lakini leo HIV unaua kimya kimya,
Familia zikivunjika, kizazi kikipotea,
Ewe Habib, tiba yake iko wapi?
Gaza inavuja damu kila siku, watoto wakiwa chini ya vifusi,
Mama wakiomba mbinguni, huku Makkah na Madinah kimya,
Je watu wa Kisemvule waililie Gaza?
Wakati Walinzi wa Haramain wako tulivu na kimya?
Ewe Habib, umma wako umechoka,
Sunna yako twaihubiri bila kuishi, Qur’ān twasoma bila kuelewa.
Tunasali kwako, tutumie shufaa yako mbele ya Arshi,
Allah atusamehe, aturudishe njia ya Madinah,
Atutakase, atuunganishe, atuinue kutoka fedheha.
Salam kwako, ewe Mtume,
Salam juu ya Ahli Beyti na Sahaba zako,
Twasubiri shufaa yako, na tumaini letu liwe kwa Allah,
Rehema isiyo na kikomo.
YUSUFU R H SABURA
0750883466