Barua ya wazi kwa afisa elimu(sekondari)- Bunda Mji

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Sep 19, 2023
305
744
Nakusalimu kwa jina la Jamhuri...Kazi iendelee.Nimekuandikia waraka huu nikitaka kushare nawe mambo kadhaa.

Tuanzie kwako,wewe ni kiongozi smart sana katika idara ya elimu sekondari hapa kwenye halmashauri yetu ya Bunda mji.Hujikwezi na umeifanya ofisi kuwa sehemu ya utendaji kazi badala ya majungu kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Mheshimiwa Afisaelimu Mkuu wa shule ya Sekondari Nyiendo alikuwa mkuu wa shule ya Dr.Nchimbi akaiharibu akawagawa walimu mwisho wa siku akasababisa vurugu .Badala ya kumuwajibisha mkampeleka Shule ya Sekondari Wariku napo ambako pia akaiharibu.Bado hamkutosheka mkamhamishia Shule ya Sekondari Nyiendo alipo mpaka sasa.Mtu kaharibu shule mbili Kwa nini asipewe demotion?

Maajabu sasa:
Alipofika hapo Nyiendo alichukia kundi kubwa la walimu active ambao walikuwa wanahoji mambo mbalimbali ya kimaendeleo.Akawahamisha walimu 11 kwenda shule za msingi wakiwemo walimu sita wa somo la jiografia.Akachagua kubaki na shule ya walimu wasioweza kuhoji chochote.Leo shule ina mwalimu mmoja wa somo la Jiografia wa serikali.Kwenye vikao vya wdc wazazi wanalaumu serikali ik kutokuajiri walimu wakati mtu mmoja aliamua kuondoa walimu wa somo husika kwa matakwa yake binafsi.Hii ni hujuma Kwa serikali.Huyu mkuu wa shule anaichonganisha serikali na wananchi.

Leo katika watahiniwa 245 waliofanya mtihani wa somo la Jiografia,ni wafunzi 26 tu waliofaulu.Pia shule imekuwa nafasi ya 19 kati ya shule 20 za halmashauri.Walimu hawana morali ya kazi isipokuwa wawili watatu ndio wapo pamoja nae

Mheshimiwa D.e.O ondoeni huyu mtu hali ni mbaya,shule inaelekea kaburini.
 
Back
Top Bottom