Barua ya amri ya kuitwa polisi kwa Mnyika

Mheshimiwa Mnyika tafadhali usiende huko watakuli-Ulimboka. Barua za polisi lazima ziwe na nembo ya Jeshi la Polisi si kama hii. Na ni lazima ipitie kwa mkuu wako (Spika) maana tayari uko kwenye imaya yake kikazi. Ukienda ujue haurudi tena, ama utarudi ni kipofu au vinginevyo. Huu ni ushauri wangu kwako.
 
Hawa usalama wa taifa wanataka kumkamata mchawi. Baada ya wao kwa wao kunyoosheana vidole na kushindwa kumpata mchawi anayevujisha siri, sasa wanadhani kwa kuwahoji waheshimiwa wa ukweli (Mnyika, Lema na Dr.) watamjua mchawi. Hawatoweza. Note: a house divided against itself will not stand. CCM will not stand whatever magic and enchanting they do with their sorcerers.
 
lazma zoka atakuwepo na plaiz, msangi atamalizia kazi, akirudi mzima huyo cjui, hakuna polisi, kuna mashetani tu.
au watakua na katool box kama kale alikua anakatumia sana Jackbauer kwenye series za 24.
 
policccm hapo ndio mwisho wao wa kiitelijensia ulipoishia..... wanafanya kama inzi anayejua uhai wake upo kwa siku saba tu.. Brother Mnyika kuwa makini wasikubahatishe kama Dr ulimboka
 
attachment.php

Wadau naomba mwongozo hapa, hizi hati za kuitwa polisi huwa hazichapwi kwenye letter head ya jeshi la polisi?? hakuna cha anwani wala nini, hii imekaaje?
 
Wadau naomba mwongozo hapa, hizi hati za kuitwa polisi huwa hazichapwi kwenye letter head ya jeshi la polisi?? hakuna cha anwani wala nini, hii imekaaje?


Kwa uandishi wa barua hii inaonyesha MaPs wa Jeshi la Polisi na bosi aliyesaini barua isiyo na nembo (crown) ni kihiyo nae. Ni jambo la kuchekesha kumpelekea Mh. Mnyika bila hata kumpa nakala spika wa bunge.

Hili nalo ni miongoni mwa vituko vya jeshi la Polisi na linajidhihirisha jinsi lilivyo utumwani kabisa.
 
Sio police wa JF, ni wale polisi waliojitambulisha kwa Ulimboka, kisha wakamdhuru
Mbona haina emblem ya police?

Kuitwa police kufanya nini? Haijaelezea hiyo barua kuwa wanamwita afanye nini?

Kingine why imeelekezwa kwa Mnyika wakati wanajua kuwa anashughuli za bunge?

Why wasianze na kina Dr Slaa na Lema kwani hawana kazi za kibunge?

Nadhani hii ineandikwa na police wa JF.

Alie andika akafanye editting aweke hata emblem ya kubumba.
 
..hata kijana wangu wa 4 yrs anaweza andika barua inayoeleweka kuliko hii !! heading inataja kifungu cha sheria na file number, na then subject inasema anazo taarifa kuhusu upelelezi wa shauri tajwa ? Mnyika hajawahi kufungua shauri sasa hiyo file # yeye atajuaje ? wow....vihiyo hawa mnapewa vyeo sababu ya kazi zenu za mabwepande ??? ........ninazenu !
 
Hiyo barua ni fake!
Hilo jarida la kesi si lilishapangiwa wapelelezi? Ndo hao wanapashwa kumfata Mnyika na kumhoji huko dodoma aliko.
Je anapashwa ku report kwa RCO au kwa Manumba?
Je ktk utendaji wa polisi huu ni utaratibu wao? kwa kweli ya kujiuliza ktk hiyo barua ni mengi mno!
 
Hili jeshi la polisi linatia aibu kweli ndiyo maana siku zote wanaambiwa wao hawatumii akili, wakiamrishwa tu hata jambo ambalo haliko kisheria wao wanakurupuka tu. Sasa kwanza kisa cha kutaka kuwakamata akina Mnyika na Dr. Slaa kinatokana na nini? Kwani wanatuhumiwa kwa kosa gani la kijinai? Kuuleza umma kwamba wanawindwa kutaka kuuawa? Hivi ipo sheria gani inayomlazimisha mtu ku-register tuhuma za jinai kituo cha polisi kama mwenyewe hataki kufanya hivyo? Mbona watu wengi tu wameumizwa na polisi na wengine wameuliwa ndugu zao mbona sijawahi kumsikia waziri au jeshi la polisi likiwataka hao wanaolituhumu jeshi la polisi kuua wafike kituo cha polisi kufungua kesi? Kwanza kesi zote za jinai hazifunguliwi na mtu bali zinafunguliwa na jamhuri na kwanza huwezi ukamlazimisha mtu kuwa shahidi au kutoa maelezo kama hataki, ila akikubali kutoa ushahidi au maelezo yanayohusiana na kosa la jinai atatakiwa kufika mahakamani kutoa ushahidi au km ipo sababu ya msingi ya kutofika mahakamani basi waendesha mashitaka wataiomba mahakama ipokee ushahidi wa maandishi, mahakama ikiridhia basi ushahidi unatolewa. Polisi walitakiwa kuwapuuza tu Dr. Slaa etc km hawataki kutoa ushahidi kwani itakula kwao km hawataki hao wanaowajua kupanga mipango wakawa huru uraiani. Vinginevyo sasa polisi wanataka kuwaundia kesi Dr Slaa na wenzake kesi ya uchochezi, na waseme hivyo kwamba wanawataka polisi kwa ajili ya tuhuma za uchochezi na si kuwalazimisha tu kufika kituo cha polisi bila kuelezea wanakwenda kufanya nini? Vinginevyo hawawatendei haki.
 
Upuuzi mtupu! Barua ya Wito yenyewe kwanza haina anuani sasa tukitaka kuijibu sijui ipelekwe wapi? Vituo vya polisiccm vipo vingi na hatujui ni wapi pa kwenda...... Sijui ni Msimbazi, Sarender, Magomeni, Chang'mbe, Buguruni, Tazara, Kawe, Tabora Central Police, Kigamboni au ...........!!!!!!!!!!!!!!!

Atakwenda au atapelekwa ni lazima tufuate sheria za nchi.
 
Kwanini waanze na Kaka Mnyika, au wanaona yeye ndio wa kuonea, au ndio kama walivyosema na kupanga kuwa atatangulizwa yeye kwanza, kisha Dr. Slaa na kumalizia na Lema, wasifanye upuuzi wao, watajuta mwaka huu, wananchi watawaadabisha, yaani watapotezwa mpaka washangae!
 
Back
Top Bottom