Barua ya Albert Einstein kumhusu Mungu yauzwa kwenye mnada kwa bei ya $2.9m(£2.3m).

aretasludovick

aretasludovick

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Messages
5,887
Points
2,000
aretasludovick

aretasludovick

JF-Expert Member
Joined Aug 8, 2015
5,887 2,000
Barua iliyoandikwa kwa hati ya mkono na Albert Einstein, ambapo anajadili suala la dini na imani, imeuzwa kwenye mnada kwa bei ya karibu $2.9m (£2.3m).

Bei hiyo imepita makadirio.

Barua hiyo ambayo kwa utani imekuwa ikiitwa "Barua ya Mungu" aliiandika Einstein mwaka 1954 na ilitarajiwa kuuzwa $1.5m (£1.2m) mnadani New York.

Mwanasayansi huyo aliyeshinda tuzo ya Nobel,aliandika barua hiyo ya ukurasa mmoja unusu akiwa na umri wa miaka 74. Lilikuwa ni kama jibu kwa mwanafalsafa Mjerumani Eric Gutkind kuhusu baadhi ya kazi zake. Gutkind alikuwa pia Myahudi.
Huwa inatazamwa na wengi kama tangazo la msimamo wa Einstein katika mjadala kuhusu sayansi na dini.

"Barua hii yenye uwazi sana, ya kibinafsi iliyoandikwa mwaka mmoja kabla ya kifo cha Einstein inasalia kuwa nyaraka pekee yenye kudhihirisha wazi msimamo wake wa kidini na kifalsafa," taarifa kutoka kwa waendesha mnada wa Christie inasema.

Barua hiyo iliuzwa karibu mara dufu ya bei iliyokadiriwa ambayo ilikuwa kati ya $1m-1.5m. Katika barua hiyo, aliyoiandika kwa Kijerumani ambayo ilikuwa lugha yake asilia, Einstein amekosoa imani ya sasa kumhusu Mungu.

"Neno la Mungu kwangu tu ni jambo la kuelezea udhaifu wa binadamu na ni matokeo ya udhaifu huu wa binadamu," naandika. "Biblia ni mkusanyiko wa hadithi za kale lakini za kuheshimiwa na kutukuzwa, ingawa kwangu zinaonekana zaidi kuwa za kitoto."

Anaendelea: "Hakuna fasiri yoyote, hata iwe ya kina na ya kupambanua zaidi kiasi gani, ambayo kwangu inaweza kubadilisha mtazamo huu wangu."

Mwanafizikia huyo pia anajadili asili na utambulisho wake, Uyahudi.

Anaandika kwamba dini hiyo "ni kama dini nyingine zote , ni mtazamo mpya wa hadithi za kale". "Wayahudi, ambao najivunia kuwa mmoja wao, na ambao nimejikita kwenye mtazamo wao wa maisha, bado kwangu hawana kitu chochote tofauti na wengine," ameandika.

"Kwa yale niliyoyaona, si bora kulikobinadamu wengine, ingawa wamelindwa dhidi ya saratani mbaya zaidi kutokana na kukosa mamlaka. Kando na hayo, sioni kitu chochote "kiteule" kuwahusu." (Aliandika hayo miaka michache tu baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia kumalizika, ambapo Wayahudi wengi waliuawa na utawala wa Nazi, na pia taifa la Israel lilikuwa bado halijapata nguvu).

Hii si mara ya kwanza kwa barua ya Enstein kuuzwa mnadani. Mwaka jana, barua aliyomwandikia mwanafunzi wakemia kutoka Italia ambaye alizuiwa kukutana naye iliuzwa $6,100.

Iliuzwa pamoja na barua nyingine za Einstein, ikiwemo barua moja ya mwaka 1928 iliyouzwa $103,000.

Kwenye barua hiyo alikuwa ameeleza mawazo yake kuhusu awamu ya tatu ya kile ambacho baadaye kiligeuka kuwa nadharia kuhusu uhusiano wa vitu kwenye maumbile, kwa Kiingereza Theory of Relativity.

Mwaka 2017, barua yake ambapo alikuwa anatoa ushauri kuhusu maisha yenye furaha iliuzwa $1.56m mjini Jerusalem.
Barua hiyo yenye aya moja tu, inasema: "Maisha ya utulivu na ya kunyenyekea yatakuletea furaha zaidi kuliko juhudi za kutafuta ufanisi na misukosuko inayoambatana na harakati na ufanisi huo."

Einstein aliamini kwamba Mungu yupo?
Einstein alikuwa kwenye kundi la watu ambao imani yao huitwa Pantheism kwa Kiingereza. Ni watu wanaoamini kwamba "Mungu ni kila kitu". Mara kadha, alionyesha mtazamo huu kwenye mawasiliano yake na Rabbi Herbert S. Goldstein, "Ninaamini katika Mungu wa Spinoza, ambaye anajidhihirisha kupitia upatanifu wa vitu vyote vilivyomo, si katika Mungu anayejishughulisha katika hatima na matendo ya binadamu."

Pantheism kwa njia rahisi zaidi ni imani kwamba kila kitu humwakilisha Mungu. Wenye kufuata imani hii mara nyingi hueleza kwamba Mungu ni vitu vyote vilivyopo, au kwamba mambo na vitu vyote ni Mungu.

Kwamba kila ukionacho ni sehemu ya Mungu.Aina ya Pantheism ya Spinoza aliyoiamini Einstein huamini kwamba kila kitu kinafanana na Mungu.

Kwamba Mungu hana ubinafsi na hayajali mambo ya binadamu. Kwa kila kitu kimeundwa na vitu vilevile vya msingi, ambavyo anatoka Mungu.

Kwamba Sheria za Fizikia hazina la kuzipinga, na kwamba kila jambo lina matokeo yake. Kila jambo linalotokea au kuwepo
lilitokana na hitaji lake kuwepo na lilikuwa nia ya Mungu.

Kwamba kwa binadamu, furaha na kuridhika maishani hutokana na kuifahamu dunia na vitu vinavyoizingira badala ya kuomba Mungu aingilie kati.

Benedict de Spinoza alikuwa mwanafalsafa Myahudi aliyezaliwa Uholanzi na wazazi Wayahudi kutoka Ureno Novemba 24, 1632, Amsterdam na akafariki Februari 21, 1677 mjini The Hague, Uholanzi.

Licha ya haya yote Einstein bado alidumisha baadhi ya tamaduni na mila za Wayahudi.

Hali kwamba alikuwa Mwanasayansi na kwamba aliongozwa na fikira katika kuufahamu ulimwengu ilimzuia kuwa na imani ambayo inaweza kuwafanya watu waseme alikuwa wa dini fulani.

Alikataa kupewa mazishi ya kitamaduni ya Wayahudi.

Ingawa bado alikuwa anazungumzia kuhusu kuamini kuhusu Mungu, alikuwa si Mungu wa dini za Kiabrahamu (Kikristo, Kiislamu na Kiyahudi ) na pia hakuwa Mungu anayerejelewa na watu walioamini kwamba Mungu yupo.

Alikuwa mara nyingi anajizuia kujiingiza kwenye mjadala kuhusu nani msema kweli, dini au sayansi.

Aidha, hakutaka kuamini kutumiwa kwa sayansi kama kielelezo katika kuamua maadili.

Wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, alinukuliwa akisema: "Bado wapo watu, wanaosema Mungu hayupo. Lakini kinachonighadhabisha zaidi ni kwamba huwa wananikuu wanapoeleza msimamo wao huo.

Bwana Kiranga natamani kusikia mtazamo wako kumhusu huyu mtu.
 
maxime

maxime

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2016
Messages
1,460
Points
2,000
maxime

maxime

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2016
1,460 2,000
ninachoshukuru wao wameishia kumkosoa Mungu ila Majibu mhimu ya maswali yetu yanayotusumbua kama haya(1)Tumetoka wapi? (2)kwanini tuko hapa? Lengo ni nini hasa
(3)Tunakwenda wapi baada ya Kufa? (4)Nini kisababishi pakuwepo na Wanyama binadamu wadudu na ndege(ihali vimekuepo katka maumbile tofaut ke/me ili vizaliane??( siku wakiweza kuyajibu haya na kuacha kumkosoa Mungu tu basi nitajiunga nao.
Ww hauwezi kuyajibu na wao hawawezi kuyajibu ... lakini angalau wao wameweka effort ya kutafuta uhalisia.... kwani hata uwepo wa Mungu umetokana na fikra za binadamu wenyewe......

Ni binadam tu ndio anawaza Mungu unlike other species, they don't care about that....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
maxime

maxime

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2016
Messages
1,460
Points
2,000
maxime

maxime

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2016
1,460 2,000
MIMI MTAZAMO WANGU NI HUU.... HAKUNA TATIZO KWA MTU ANAESEMA MUNGU YUPO NA HAKUNA TATIZO LA ANAESEMA KWAMBA MUNGU HAYUPO.....

BALI NINA TATIZO NA KILE ANACHOKITENDA MTU KUTOKANA NA MATOKEO YA KUAMINI HIVYO...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
maxime

maxime

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2016
Messages
1,460
Points
2,000
maxime

maxime

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2016
1,460 2,000
We pimbi uwe unaelewa

Umeme upo na na unathibitishika kama upo ndio mana hapa hatubishani kuto kuwepo kwake unaelewa

Nilikukataza mwanzo kua mi sibishi mungu yupo eti kwasababu haonekani, vitu vingi havionekani lakini vinathibitishika kua vipo pasipo mkanganyiko wowote mfano umeme upo unathibitishika kwa mfano mdogo tu upepo unathibitishika hata kwa ngozi yako kua upo,

Unapozungumzia kua mungu ndiye muumbaji wa kila kitu hutakiwi kuweka ukomo kwenye kumuelezea kama ulivyo fanya kuelezea vitu alivyo viumba yeye aliumbwa na nani

Ulisema kua kaumba viumbe vilivyo na visivyo hai

Swali je huyo mungu ni kiumbe hai au kisicho hai?
Kwa urahisi kabisa mkuu, vitu vyote vinavyomake sense vinafall kwenye milango mitano ya fahamu, kuona (macho), kusikia (masikio), kunusa (pua), kuonja (ulimi) na kuhisi (ngozi)... binadamu akikosa vyote hivyo kwa pamoja basi hakuna ambacho kitakuwa kinamake sense kwake.... huyo hana tofauti na mfu.Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAHENDEKA

MAHENDEKA

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2010
Messages
278
Points
225
MAHENDEKA

MAHENDEKA

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2010
278 225
wamesema wapi mkuu nisaidie hilo bandiko!
Kwa kukusaidia inasemekana Musa alimuona Mungu akipita,lakini Musa alimuona kwa nyuma ila sio kwa mbele,nmesahau ni kitabu gani kinaelezea hii stori lakini ni agano la kale kitu kama kitabu cha hesabu/numbers au kumbukumbu la torati/deutronomy hv (sikumbuki vizuri).

Kisa chenyewe ni kama ifuatavyo

Ilifika mahala Musa akamuomba Mungu ajitokeze ili aweze kumuona, Mungu akamwambia mwanadamu hawezi niona mimi Mungu halafu akaendelea kuishi ! lazima afe akishaniona.

Lakini kwa sababu Musa alitamani kumuona Mungu akamchukua Musa akamficha kwenye ufa uliopo kwenye mwamba,kisha Mungu akaweka kiganja chake pale juu ya ule ufa halafu akapita,alipomaliza kupita akafunua mkono wake ..kwa hio Musa akamuona Mungu kwa nyuma lakini sura hakuiona.

Kwa wasomaji wazuri wa Biblia watagundua kua ule ufa aliofichwa Musa ndo mahala ambapo nabii eliya alikwenda kujificha miaka ya baadae sana baada ya kutabiri njaa ya miaka mitatu halafu akaenda kujificha ili aiuwawe ....akawa analetewa mkate na kunguru na kunywa maji ya mto.
 
msomi uchwara

msomi uchwara

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2017
Messages
1,685
Points
2,000
msomi uchwara

msomi uchwara

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2017
1,685 2,000
Mbona inaonesha alikua na mawazo ya kawaida sana huyo mtu?....watu wa zamani walipenda kujikweza sana na kujiona wao wanaakili kumbe hakuna lolote zaid ya ubabaishaji tu.
 
Elungata

Elungata

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Messages
31,656
Points
2,000
Elungata

Elungata

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2011
31,656 2,000
@MAHENDEKA,moses aliwahi kukabwa shingo na mungu,mpaka akaokolewa na mkewe Zilipa,kwahiyo kwa mjibu wa kumbukumbu ya torati,moses kamwona mungu uso kwa uso
 
okiwira

okiwira

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2018
Messages
826
Points
1,000
okiwira

okiwira

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2018
826 1,000
Duuuuuuuh@MAHENDEKA,moses aliwahi kukabwa shingo na mungu,mpaka akaokolewa na mkewe Zilipa,kwahiyo kwa mjibu wa kumbukumbu ya torati,moses kamwona mungu uso kwa uso
 
mark girland

mark girland

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2019
Messages
623
Points
500
mark girland

mark girland

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2019
623 500
Unataka kukimbia maada kwa njia ya beyeism....ila ukweli utabaki palepale na mimi kuokujua Dini ya Beyonce haimaanishi mimi sijui Dini yangu: Kama Beyonce ana dini yake(hakuna tatzo) kuna dini nyingi sana tu Duniani na wala hazjaweza kuuondoa uwepo wa Mungu) siijui dini ya beyonce ila ninayoimani kama wanamuabudu Beyonce kama Mungu wao basi wao pia wanaamini uwepo wa Mungu ila bado hawamjui Mungu wa kweli ni yupi kat ya wengi wanaotajwa duniani na kuabudiwa;(Kitu ambacho kinatuua waafrica nikwasababu tupo wepes wa kumata na story za mtandaoni bila uthibtsho(Tujifunze kwenda na wakati unaposikia kitu kabla ya kushadadia nenda hakikisha uje utupatie mhitasari)
Mkuu kwani hiyo imani yako kwa mara ya kwanza uliijua vipi?
 
mark girland

mark girland

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2019
Messages
623
Points
500
mark girland

mark girland

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2019
623 500
Mungu yupo ila mungu si kitu wala si mwili mungu ni kama upepo uvumao ila nguvu yake ni kubwa mno.lakini pia naamini mungu baada ya kuumba ulimwengu akaachana na mambo ya ulimwengu aliamua aishi mafichoni ndio haonekani kwa macho ndio maana hata walokole wengi wao wanasema yesu ndio mungu yaani hata wao wanavurugwa.
Wewe JamAa utakuwa muumini wa wale wanaojiita deist...
 
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Messages
15,896
Points
2,000
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2010
15,896 2,000
Mbona wanasema Mussa ndio binadam pekee alieweza kumuona mungu
hakuna mwanadamu yoyote aliyewahi kumwona Mungu, wengi walioteshwa unabii na kupewa nguvu kubwa akiwemo Mussa na Elia...
 
mtafuta-maisha

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2016
Messages
2,016
Points
2,000
mtafuta-maisha

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Joined Nov 5, 2016
2,016 2,000
Hata siyo wa zamani hivi ulishawahi fuatilia mawazo yake mengine. Jamaa anaitwa father of modern physics na hakuwa anajikweza maana hata alipoulizwa inajisikia vipi kuwa mtu mwenye akili nyingi kuliko wote jibu lake lilikuwa akaulizwe Tesla maana kwake yeye ndiye mwenye akili nying
Mbona inaonesha alikua na mawazo ya kawaida sana huyo mtu?....watu wa zamani walipenda kujikweza sana na kujiona wao wanaakili kumbe hakuna lolote zaid ya ubabaishaji tu.
 
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
44,652
Points
2,000
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
44,652 2,000
Barua iliyoandikwa kwa hati ya mkono na Albert Einstein, ambapo anajadili suala la dini na imani, imeuzwa kwenye mnada kwa bei ya karibu $2.9m (£2.3m).

Bei hiyo imepita makadirio.

Barua hiyo ambayo kwa utani imekuwa ikiitwa "Barua ya Mungu" aliiandika Einstein mwaka 1954 na ilitarajiwa kuuzwa $1.5m (£1.2m) mnadani New York.

Mwanasayansi huyo aliyeshinda tuzo ya Nobel,aliandika barua hiyo ya ukurasa mmoja unusu akiwa na umri wa miaka 74. Lilikuwa ni kama jibu kwa mwanafalsafa Mjerumani Eric Gutkind kuhusu baadhi ya kazi zake. Gutkind alikuwa pia Myahudi.
Huwa inatazamwa na wengi kama tangazo la msimamo wa Einstein katika mjadala kuhusu sayansi na dini.

"Barua hii yenye uwazi sana, ya kibinafsi iliyoandikwa mwaka mmoja kabla ya kifo cha Einstein inasalia kuwa nyaraka pekee yenye kudhihirisha wazi msimamo wake wa kidini na kifalsafa," taarifa kutoka kwa waendesha mnada wa Christie inasema.

Barua hiyo iliuzwa karibu mara dufu ya bei iliyokadiriwa ambayo ilikuwa kati ya $1m-1.5m. Katika barua hiyo, aliyoiandika kwa Kijerumani ambayo ilikuwa lugha yake asilia, Einstein amekosoa imani ya sasa kumhusu Mungu.

"Neno la Mungu kwangu tu ni jambo la kuelezea udhaifu wa binadamu na ni matokeo ya udhaifu huu wa binadamu," naandika. "Biblia ni mkusanyiko wa hadithi za kale lakini za kuheshimiwa na kutukuzwa, ingawa kwangu zinaonekana zaidi kuwa za kitoto."

Anaendelea: "Hakuna fasiri yoyote, hata iwe ya kina na ya kupambanua zaidi kiasi gani, ambayo kwangu inaweza kubadilisha mtazamo huu wangu."

Mwanafizikia huyo pia anajadili asili na utambulisho wake, Uyahudi.

Anaandika kwamba dini hiyo "ni kama dini nyingine zote , ni mtazamo mpya wa hadithi za kale". "Wayahudi, ambao najivunia kuwa mmoja wao, na ambao nimejikita kwenye mtazamo wao wa maisha, bado kwangu hawana kitu chochote tofauti na wengine," ameandika.

"Kwa yale niliyoyaona, si bora kulikobinadamu wengine, ingawa wamelindwa dhidi ya saratani mbaya zaidi kutokana na kukosa mamlaka. Kando na hayo, sioni kitu chochote "kiteule" kuwahusu." (Aliandika hayo miaka michache tu baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia kumalizika, ambapo Wayahudi wengi waliuawa na utawala wa Nazi, na pia taifa la Israel lilikuwa bado halijapata nguvu).

Hii si mara ya kwanza kwa barua ya Enstein kuuzwa mnadani. Mwaka jana, barua aliyomwandikia mwanafunzi wakemia kutoka Italia ambaye alizuiwa kukutana naye iliuzwa $6,100.

Iliuzwa pamoja na barua nyingine za Einstein, ikiwemo barua moja ya mwaka 1928 iliyouzwa $103,000.

Kwenye barua hiyo alikuwa ameeleza mawazo yake kuhusu awamu ya tatu ya kile ambacho baadaye kiligeuka kuwa nadharia kuhusu uhusiano wa vitu kwenye maumbile, kwa Kiingereza Theory of Relativity.

Mwaka 2017, barua yake ambapo alikuwa anatoa ushauri kuhusu maisha yenye furaha iliuzwa $1.56m mjini Jerusalem.
Barua hiyo yenye aya moja tu, inasema: "Maisha ya utulivu na ya kunyenyekea yatakuletea furaha zaidi kuliko juhudi za kutafuta ufanisi na misukosuko inayoambatana na harakati na ufanisi huo."

Einstein aliamini kwamba Mungu yupo?
Einstein alikuwa kwenye kundi la watu ambao imani yao huitwa Pantheism kwa Kiingereza. Ni watu wanaoamini kwamba "Mungu ni kila kitu". Mara kadha, alionyesha mtazamo huu kwenye mawasiliano yake na Rabbi Herbert S. Goldstein, "Ninaamini katika Mungu wa Spinoza, ambaye anajidhihirisha kupitia upatanifu wa vitu vyote vilivyomo, si katika Mungu anayejishughulisha katika hatima na matendo ya binadamu."

Pantheism kwa njia rahisi zaidi ni imani kwamba kila kitu humwakilisha Mungu. Wenye kufuata imani hii mara nyingi hueleza kwamba Mungu ni vitu vyote vilivyopo, au kwamba mambo na vitu vyote ni Mungu.

Kwamba kila ukionacho ni sehemu ya Mungu.Aina ya Pantheism ya Spinoza aliyoiamini Einstein huamini kwamba kila kitu kinafanana na Mungu.

Kwamba Mungu hana ubinafsi na hayajali mambo ya binadamu. Kwa kila kitu kimeundwa na vitu vilevile vya msingi, ambavyo anatoka Mungu.

Kwamba Sheria za Fizikia hazina la kuzipinga, na kwamba kila jambo lina matokeo yake. Kila jambo linalotokea au kuwepo
lilitokana na hitaji lake kuwepo na lilikuwa nia ya Mungu.

Kwamba kwa binadamu, furaha na kuridhika maishani hutokana na kuifahamu dunia na vitu vinavyoizingira badala ya kuomba Mungu aingilie kati.

Benedict de Spinoza alikuwa mwanafalsafa Myahudi aliyezaliwa Uholanzi na wazazi Wayahudi kutoka Ureno Novemba 24, 1632, Amsterdam na akafariki Februari 21, 1677 mjini The Hague, Uholanzi.

Licha ya haya yote Einstein bado alidumisha baadhi ya tamaduni na mila za Wayahudi.

Hali kwamba alikuwa Mwanasayansi na kwamba aliongozwa na fikira katika kuufahamu ulimwengu ilimzuia kuwa na imani ambayo inaweza kuwafanya watu waseme alikuwa wa dini fulani.

Alikataa kupewa mazishi ya kitamaduni ya Wayahudi.

Ingawa bado alikuwa anazungumzia kuhusu kuamini kuhusu Mungu, alikuwa si Mungu wa dini za Kiabrahamu (Kikristo, Kiislamu na Kiyahudi ) na pia hakuwa Mungu anayerejelewa na watu walioamini kwamba Mungu yupo.

Alikuwa mara nyingi anajizuia kujiingiza kwenye mjadala kuhusu nani msema kweli, dini au sayansi.

Aidha, hakutaka kuamini kutumiwa kwa sayansi kama kielelezo katika kuamua maadili.

Wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, alinukuliwa akisema: "Bado wapo watu, wanaosema Mungu hayupo. Lakini kinachonighadhabisha zaidi ni kwamba huwa wananikuu wanapoeleza msimamo wao huo.

Bwana Kiranga natamani kusikia mtazamo wako kumhusu huyu mtu.
Kama mimi, Einstein hakukubali uwepo wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kama aliyeandikwa katika Biblia na Quran.
 
aimi lyatuu

aimi lyatuu

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Messages
342
Points
250
aimi lyatuu

aimi lyatuu

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2015
342 250
anaghadhibishwa sana na watu kama ninyi mnaemnukuu mnapoelezea misimamo yenu!...kimsingi hata yeye mwenyewe anaamini MUNGU yupo ila alikuwa anatafuta challenge na anachukia mnapo-force awe role-model wenu...ni kama mnamwengezea dhambi ya kuwa chanzo cha mpotoshaji wa binadamu wenzake
 
Forum statistics

Threads 1,315,263
Members 505,171
Posts 31,851,760
Top