Barua ya Albert Einstein kumhusu Mungu yauzwa kwenye mnada kwa bei ya $2.9m(£2.3m).

aretasludovick

aretasludovick

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Messages
5,887
Points
2,000
aretasludovick

aretasludovick

JF-Expert Member
Joined Aug 8, 2015
5,887 2,000
Barua iliyoandikwa kwa hati ya mkono na Albert Einstein, ambapo anajadili suala la dini na imani, imeuzwa kwenye mnada kwa bei ya karibu $2.9m (£2.3m).

Bei hiyo imepita makadirio.

Barua hiyo ambayo kwa utani imekuwa ikiitwa "Barua ya Mungu" aliiandika Einstein mwaka 1954 na ilitarajiwa kuuzwa $1.5m (£1.2m) mnadani New York.

Mwanasayansi huyo aliyeshinda tuzo ya Nobel,aliandika barua hiyo ya ukurasa mmoja unusu akiwa na umri wa miaka 74. Lilikuwa ni kama jibu kwa mwanafalsafa Mjerumani Eric Gutkind kuhusu baadhi ya kazi zake. Gutkind alikuwa pia Myahudi.
Huwa inatazamwa na wengi kama tangazo la msimamo wa Einstein katika mjadala kuhusu sayansi na dini.

"Barua hii yenye uwazi sana, ya kibinafsi iliyoandikwa mwaka mmoja kabla ya kifo cha Einstein inasalia kuwa nyaraka pekee yenye kudhihirisha wazi msimamo wake wa kidini na kifalsafa," taarifa kutoka kwa waendesha mnada wa Christie inasema.

Barua hiyo iliuzwa karibu mara dufu ya bei iliyokadiriwa ambayo ilikuwa kati ya $1m-1.5m. Katika barua hiyo, aliyoiandika kwa Kijerumani ambayo ilikuwa lugha yake asilia, Einstein amekosoa imani ya sasa kumhusu Mungu.

"Neno la Mungu kwangu tu ni jambo la kuelezea udhaifu wa binadamu na ni matokeo ya udhaifu huu wa binadamu," naandika. "Biblia ni mkusanyiko wa hadithi za kale lakini za kuheshimiwa na kutukuzwa, ingawa kwangu zinaonekana zaidi kuwa za kitoto."

Anaendelea: "Hakuna fasiri yoyote, hata iwe ya kina na ya kupambanua zaidi kiasi gani, ambayo kwangu inaweza kubadilisha mtazamo huu wangu."

Mwanafizikia huyo pia anajadili asili na utambulisho wake, Uyahudi.

Anaandika kwamba dini hiyo "ni kama dini nyingine zote , ni mtazamo mpya wa hadithi za kale". "Wayahudi, ambao najivunia kuwa mmoja wao, na ambao nimejikita kwenye mtazamo wao wa maisha, bado kwangu hawana kitu chochote tofauti na wengine," ameandika.

"Kwa yale niliyoyaona, si bora kulikobinadamu wengine, ingawa wamelindwa dhidi ya saratani mbaya zaidi kutokana na kukosa mamlaka. Kando na hayo, sioni kitu chochote "kiteule" kuwahusu." (Aliandika hayo miaka michache tu baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia kumalizika, ambapo Wayahudi wengi waliuawa na utawala wa Nazi, na pia taifa la Israel lilikuwa bado halijapata nguvu).

Hii si mara ya kwanza kwa barua ya Enstein kuuzwa mnadani. Mwaka jana, barua aliyomwandikia mwanafunzi wakemia kutoka Italia ambaye alizuiwa kukutana naye iliuzwa $6,100.

Iliuzwa pamoja na barua nyingine za Einstein, ikiwemo barua moja ya mwaka 1928 iliyouzwa $103,000.

Kwenye barua hiyo alikuwa ameeleza mawazo yake kuhusu awamu ya tatu ya kile ambacho baadaye kiligeuka kuwa nadharia kuhusu uhusiano wa vitu kwenye maumbile, kwa Kiingereza Theory of Relativity.

Mwaka 2017, barua yake ambapo alikuwa anatoa ushauri kuhusu maisha yenye furaha iliuzwa $1.56m mjini Jerusalem.
Barua hiyo yenye aya moja tu, inasema: "Maisha ya utulivu na ya kunyenyekea yatakuletea furaha zaidi kuliko juhudi za kutafuta ufanisi na misukosuko inayoambatana na harakati na ufanisi huo."

Einstein aliamini kwamba Mungu yupo?
Einstein alikuwa kwenye kundi la watu ambao imani yao huitwa Pantheism kwa Kiingereza. Ni watu wanaoamini kwamba "Mungu ni kila kitu". Mara kadha, alionyesha mtazamo huu kwenye mawasiliano yake na Rabbi Herbert S. Goldstein, "Ninaamini katika Mungu wa Spinoza, ambaye anajidhihirisha kupitia upatanifu wa vitu vyote vilivyomo, si katika Mungu anayejishughulisha katika hatima na matendo ya binadamu."

Pantheism kwa njia rahisi zaidi ni imani kwamba kila kitu humwakilisha Mungu. Wenye kufuata imani hii mara nyingi hueleza kwamba Mungu ni vitu vyote vilivyopo, au kwamba mambo na vitu vyote ni Mungu.

Kwamba kila ukionacho ni sehemu ya Mungu.Aina ya Pantheism ya Spinoza aliyoiamini Einstein huamini kwamba kila kitu kinafanana na Mungu.

Kwamba Mungu hana ubinafsi na hayajali mambo ya binadamu. Kwa kila kitu kimeundwa na vitu vilevile vya msingi, ambavyo anatoka Mungu.

Kwamba Sheria za Fizikia hazina la kuzipinga, na kwamba kila jambo lina matokeo yake. Kila jambo linalotokea au kuwepo
lilitokana na hitaji lake kuwepo na lilikuwa nia ya Mungu.

Kwamba kwa binadamu, furaha na kuridhika maishani hutokana na kuifahamu dunia na vitu vinavyoizingira badala ya kuomba Mungu aingilie kati.

Benedict de Spinoza alikuwa mwanafalsafa Myahudi aliyezaliwa Uholanzi na wazazi Wayahudi kutoka Ureno Novemba 24, 1632, Amsterdam na akafariki Februari 21, 1677 mjini The Hague, Uholanzi.

Licha ya haya yote Einstein bado alidumisha baadhi ya tamaduni na mila za Wayahudi.

Hali kwamba alikuwa Mwanasayansi na kwamba aliongozwa na fikira katika kuufahamu ulimwengu ilimzuia kuwa na imani ambayo inaweza kuwafanya watu waseme alikuwa wa dini fulani.

Alikataa kupewa mazishi ya kitamaduni ya Wayahudi.

Ingawa bado alikuwa anazungumzia kuhusu kuamini kuhusu Mungu, alikuwa si Mungu wa dini za Kiabrahamu (Kikristo, Kiislamu na Kiyahudi ) na pia hakuwa Mungu anayerejelewa na watu walioamini kwamba Mungu yupo.

Alikuwa mara nyingi anajizuia kujiingiza kwenye mjadala kuhusu nani msema kweli, dini au sayansi.

Aidha, hakutaka kuamini kutumiwa kwa sayansi kama kielelezo katika kuamua maadili.

Wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, alinukuliwa akisema: "Bado wapo watu, wanaosema Mungu hayupo. Lakini kinachonighadhabisha zaidi ni kwamba huwa wananikuu wanapoeleza msimamo wao huo.

Bwana Kiranga natamani kusikia mtazamo wako kumhusu huyu mtu.
 
hakuna uchawi

hakuna uchawi

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2018
Messages
385
Points
500
hakuna uchawi

hakuna uchawi

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2018
385 500
Kuna mahali niliwahi kusoma kuhusu freemason nikagungua hawa jamaa wapo vizuri kimtazamo,wao wanataka mtu awe huru wanataka binadamu ajifunze kujitegemea ajijue yeye ni nani wanataka muunganiko wa jamii moja yenye lugha 1 wanatamani hata kesho kama ulimwengu ungekua na watu welevu.
Ahsante kwa kutuletea taarifa hii.

Mi ni moja wasio amini uwepo wa Mungu kwa zaidi ya miaka kumi sasa.
Nilianza kuamini hivi toka nikiwa form two na bado ninadunda tu.

Mungu hakuwahi kuwepo, hayupo, hana sababu ya kuwepo na hata kuwepo milele.
 
hakuna uchawi

hakuna uchawi

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2018
Messages
385
Points
500
hakuna uchawi

hakuna uchawi

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2018
385 500
Siamini mnavo funguka kuhusu mungu tumekalilishwa tu
Mwanasayansi anaeheshimiwa kasema Biblia ni ya kitoto ! Ukiangalia kwa makini ni kweli, ni kuogopesha watu ili waamini vitu visivyoonekana .
 
hakuna uchawi

hakuna uchawi

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2018
Messages
385
Points
500
hakuna uchawi

hakuna uchawi

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2018
385 500
Unauliza swali la aibu sana binadamu ni mnyama ka wanyama wengine utofaut alipewa utashi,kuhusu ukifa unaenda wapi je jiulize kuku akifa anaenda wapi na ngurue je na wanyama wote wakifa wanaenda wapi?ukifa habari yako imeisha hakuna maisha baada ya kifo,ok tukubali mnavo taka ni sayari ipi tunaenda kuishi?
ninachoshukuru wao wameishia kumkosoa Mungu ila Majibu mhimu ya maswali yetu yanayotusumbua kama haya(1)Tumetoka wapi? (2)kwanini tuko hapa? Lengo ni nini hasa
(3)Tunakwenda wapi baada ya Kufa? (4)Nini kisababishi pakuwepo na Wanyama binadamu wadudu na ndege(ihali vimekuepo katka maumbile tofaut ke/me ili vizaliane??( siku wakiweza kuyajibu haya na kuacha kumkosoa Mungu tu basi nitajiunga nao.
 
Baba Swalehe

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Messages
11,051
Points
2,000
Baba Swalehe

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2017
11,051 2,000
Ebu tuambie scientist wewe umegundua nini?
Reverse gravity

Number factors for lower mundesters

And other two things siwez weka hapa na bado ...vipo on progress

Mkuu usione watu tunaleta masihara sana humu , but we are also smart
 
Dr Philosopher

Dr Philosopher

Member
Joined
Dec 13, 2016
Messages
40
Points
125
Dr Philosopher

Dr Philosopher

Member
Joined Dec 13, 2016
40 125
Watu wengi wana tatizo hili. Ukiwa simple wanakudharau na kukubeza pasipo kuelewa CONTENT mtu aliyo nayo exceptionally. "Ni ngumu sana Mjinga kumtambua Mwerevu asipojitambua kwanza kwamba yeye ni Mjinga"
Reverse gravity

Number factors for lower mundesters

And other two things siwez weka hapa na bado ...vipo on progress

Mkuu usione watu tunaleta masihara sana humu , but we are also smart
 
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Messages
347
Points
250
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2014
347 250
Unauliza swali la aibu sana binadamu ni mnyama ka wanyama wengine utofaut alipewa utashi,kuhusu ukifa unaenda wapi je jiulize kuku akifa anaenda wapi na ngurue je na wanyama wote wakifa wanaenda wapi?ukifa habari yako imeisha hakuna maisha baada ya kifo,ok tukubali mnavo taka ni sayari ipi tunaenda kuishi?
Ungejibu yote basi ndugu? Mbona umeishia moja tu? Okay sawa nakubali mawazo yako iliurdhike japo hauko sahihi.....naomba niulize Kwa kuwa umekiri kuwa wanadam WAMEPEWA Utashi wa.........je! Aliewapa huo utashi Ni nani na yuko wapi?
 
kurlzawa

kurlzawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2018
Messages
6,423
Points
2,000
kurlzawa

kurlzawa

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2018
6,423 2,000
Mungu yupo ila mungu si kitu wala si mwili mungu ni kama upepo uvumao ila nguvu yake ni kubwa mno.lakini pia naamini mungu baada ya kuumba ulimwengu akaachana na mambo ya ulimwengu aliamua aishi mafichoni ndio haonekani kwa macho ndio maana hata walokole wengi wao wanasema yesu ndio mungu yaani hata wao wanavurugwa.
Mungu wenu ipo siku utamuita ata nywele kama Leo hii umemuita upepo pole sana
 
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Messages
347
Points
250
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2014
347 250
Elya alishawah kumuuliza Mungu kwann unasema utawachoma moto watu uliowaumba Kwa mikono yako?? Mungu Hakumjibu ila alimwambia apande shamba LA ngano ..alipopanda wakat wa kuvuna akavuna ngano na magugu akachoma moto.... Mungu akamuuliza Elya kwann kuyachoma moto mbona uliyapanda kwa mikono yako!? Elya akamjibu haya niliyapanda na mvua toka mbinguni iliyanyeshea pamj na wenzake lakn yamekuwa magugu hayajaweza kuzaa ivo yastahili kuchomwa moto.... Ndipo Mungu akamkumbusha swali lake kwa mfno huohuo.....( hivyo basi uelewe kupitia hili)
Kama lengo la Mungu kukuumba nakukuleta dunia alafu ufe uende mbinguni tena ama jehanam.. na isitoshe anaujua mwanzo wako na mwisho wako...

Kwanini asinge umba huyu anapelekea jehanam na huyu mbinguni... Ama kuangamiza jehenam kwa neno tuu na kusambaratika..

Maswala ya sini yanafikirisha sanaa haswa ukiacha ubongo ufikirie na sio kuwaza yale tunayo karirishwa
 
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Messages
347
Points
250
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2014
347 250
Hujajibu swali hata moja hapo,unaleta porojo tu.
Umemjibu vema sana et watu walikosa majibu akat tayar tunayo kuwa Ni (Mungu kayayafnya!!)/ yey ndio hana majibu ...hoja zao Ni dhaifu et kitu kama hakionekan basi hakipo ...lakn kwakuwa yeye ndiye yeye anayebisha uwepo wa Mungu!, kazi ya kutoa ushahidi inamwangukia yeye mwenyewe.. Hivi vilivyopo vinatoka wapi? Kama vitu vilitokea kwenye big bang hivyo vilivyogongana vimetokea wapi? Kazi ya kurudi nyuma anayo yeye ..sisi tushamaliza kazi: ukirud nyuma na kurudi na kurudi utafika kwenye uwepo wa Mungu ambao sisi tunautafsri kwa hivi tuvionavyo......kwetu sisi hivi vyenye mpangilio wenye akili haviwezi kuanzia kwenye bahati nasibu wala ajali ya bing bang ..bahat nasibu haiwez kuwa na akili na nidhamu kama iliyopo ulimwenguni sembuse ajali!!!!! Mkuu watu kama hawa wasikupe shida ata hawajielewi. Kasome Ayubu 21 yoote. Utajifunza kitu kuhusu hawa jamaa
 
kurlzawa

kurlzawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2018
Messages
6,423
Points
2,000
kurlzawa

kurlzawa

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2018
6,423 2,000
Unamwandiko mbaya sana kuliko watu wote Tanzania
Umemjibu vema sana et watu walikosa majibu akat tayar tunayo kuwa Ni (Mungu kayayafnya!!)/ yey ndio hana majibu ...hoja zao Ni dhaifu et kitu kama hakionekan basi hakipo ...lakn kwakuwa yeye ndiye yeye anayebisha uwepo wa Mungu!, kazi ya kutoa ushahidi inamwangukia yeye mwenyewe.. Hivi vilivyopo vinatoka wapi? Kama vitu vilitokea kwenye big bang hivyo vilivyogongana vimetokea wapi? Kazi ya kurudi nyuma anayo yeye ..sisi tushamaliza kazi: ukirud nyuma na kurudi na kurudi utafika kwenye uwepo wa Mungu ambao sisi tunautafsri kwa hivi tuvionavyo......kwetu sisi hivi vyenye mpangilio wenye akili haviwezi kuanzia kwenye bahati nasibu wala ajali ya bing bang ..bahat nasibu haiwez kuwa na akili na nidhamu kama iliyopo ulimwenguni sembuse ajali!!!!! Mkuu watu kama hawa wasikupe shida ata hawajielewi. Kasome Ayubu 21 yoote. Utajifunza kitu kuhusu hawa jamaa
 
Baba Swalehe

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Messages
11,051
Points
2,000
Baba Swalehe

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2017
11,051 2,000
Thats a problem na hua sion maana ya kuish kwa kujikweza

Ni stupidy life sijawah ona ...

Kuna muda napotea jukwaan hata for two month ....

Aaah ki baba swalehe ....
Watu wengi wana tatizo hili. Ukiwa simple wanakudharau na kukubeza pasipo kuelewa CONTENT mtu aliyo nayo exceptionally. "Ni ngumu sana Mjinga kumtambua Mwerevu asipojitambua kwanza kwamba yeye ni Mjinga"
 
oscarsolomon

oscarsolomon

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Messages
3,920
Points
2,000
oscarsolomon

oscarsolomon

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2017
3,920 2,000
Umemjibu vema sana et watu walikosa majibu akat tayar tunayo kuwa Ni (Mungu kayayafnya!!)/ yey ndio hana majibu ...hoja zao Ni dhaifu et kitu kama hakionekan basi hakipo ...lakn kwakuwa yeye ndiye yeye anayebisha uwepo wa Mungu!, kazi ya kutoa ushahidi inamwangukia yeye mwenyewe.. Hivi vilivyopo vinatoka wapi? Kama vitu vilitokea kwenye big bang hivyo vilivyogongana vimetokea wapi? Kazi ya kurudi nyuma anayo yeye ..sisi tushamaliza kazi: ukirud nyuma na kurudi na kurudi utafika kwenye uwepo wa Mungu ambao sisi tunautafsri kwa hivi tuvionavyo......kwetu sisi hivi vyenye mpangilio wenye akili haviwezi kuanzia kwenye bahati nasibu wala ajali ya bing bang ..bahat nasibu haiwez kuwa na akili na nidhamu kama iliyopo ulimwenguni sembuse ajali!!!!! Mkuu watu kama hawa wasikupe shida ata hawajielewi. Kasome Ayubu 21 yoote. Utajifunza kitu kuhusu hawa jamaa
Wapi nimesema siamini mungu yupo kwasababu haonekani kwa macho kama upepo?
 
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Messages
347
Points
250
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2014
347 250
Sitaki kuamini mi nataka kujua

Imani huja kwa kubashiri na ukweli haupati kwa kubashiri
Kubashiri ndo kufnyaje? Imani kila MTU anayo usijifche .....maana hapo mwenyew unaamini dunia ilitokea kwa bing bang. Hivyo kusema hutak kuamini Ni ujuaji tu usio na maana.
 
Forum statistics

Threads 1,315,263
Members 505,171
Posts 31,851,760
Top