Barua ya Albert Einstein kumhusu Mungu yauzwa kwenye mnada kwa bei ya $2.9m(£2.3m).

aretasludovick

aretasludovick

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Messages
5,887
Points
2,000
aretasludovick

aretasludovick

JF-Expert Member
Joined Aug 8, 2015
5,887 2,000
Barua iliyoandikwa kwa hati ya mkono na Albert Einstein, ambapo anajadili suala la dini na imani, imeuzwa kwenye mnada kwa bei ya karibu $2.9m (£2.3m).

Bei hiyo imepita makadirio.

Barua hiyo ambayo kwa utani imekuwa ikiitwa "Barua ya Mungu" aliiandika Einstein mwaka 1954 na ilitarajiwa kuuzwa $1.5m (£1.2m) mnadani New York.

Mwanasayansi huyo aliyeshinda tuzo ya Nobel,aliandika barua hiyo ya ukurasa mmoja unusu akiwa na umri wa miaka 74. Lilikuwa ni kama jibu kwa mwanafalsafa Mjerumani Eric Gutkind kuhusu baadhi ya kazi zake. Gutkind alikuwa pia Myahudi.
Huwa inatazamwa na wengi kama tangazo la msimamo wa Einstein katika mjadala kuhusu sayansi na dini.

"Barua hii yenye uwazi sana, ya kibinafsi iliyoandikwa mwaka mmoja kabla ya kifo cha Einstein inasalia kuwa nyaraka pekee yenye kudhihirisha wazi msimamo wake wa kidini na kifalsafa," taarifa kutoka kwa waendesha mnada wa Christie inasema.

Barua hiyo iliuzwa karibu mara dufu ya bei iliyokadiriwa ambayo ilikuwa kati ya $1m-1.5m. Katika barua hiyo, aliyoiandika kwa Kijerumani ambayo ilikuwa lugha yake asilia, Einstein amekosoa imani ya sasa kumhusu Mungu.

"Neno la Mungu kwangu tu ni jambo la kuelezea udhaifu wa binadamu na ni matokeo ya udhaifu huu wa binadamu," naandika. "Biblia ni mkusanyiko wa hadithi za kale lakini za kuheshimiwa na kutukuzwa, ingawa kwangu zinaonekana zaidi kuwa za kitoto."

Anaendelea: "Hakuna fasiri yoyote, hata iwe ya kina na ya kupambanua zaidi kiasi gani, ambayo kwangu inaweza kubadilisha mtazamo huu wangu."

Mwanafizikia huyo pia anajadili asili na utambulisho wake, Uyahudi.

Anaandika kwamba dini hiyo "ni kama dini nyingine zote , ni mtazamo mpya wa hadithi za kale". "Wayahudi, ambao najivunia kuwa mmoja wao, na ambao nimejikita kwenye mtazamo wao wa maisha, bado kwangu hawana kitu chochote tofauti na wengine," ameandika.

"Kwa yale niliyoyaona, si bora kulikobinadamu wengine, ingawa wamelindwa dhidi ya saratani mbaya zaidi kutokana na kukosa mamlaka. Kando na hayo, sioni kitu chochote "kiteule" kuwahusu." (Aliandika hayo miaka michache tu baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia kumalizika, ambapo Wayahudi wengi waliuawa na utawala wa Nazi, na pia taifa la Israel lilikuwa bado halijapata nguvu).

Hii si mara ya kwanza kwa barua ya Enstein kuuzwa mnadani. Mwaka jana, barua aliyomwandikia mwanafunzi wakemia kutoka Italia ambaye alizuiwa kukutana naye iliuzwa $6,100.

Iliuzwa pamoja na barua nyingine za Einstein, ikiwemo barua moja ya mwaka 1928 iliyouzwa $103,000.

Kwenye barua hiyo alikuwa ameeleza mawazo yake kuhusu awamu ya tatu ya kile ambacho baadaye kiligeuka kuwa nadharia kuhusu uhusiano wa vitu kwenye maumbile, kwa Kiingereza Theory of Relativity.

Mwaka 2017, barua yake ambapo alikuwa anatoa ushauri kuhusu maisha yenye furaha iliuzwa $1.56m mjini Jerusalem.
Barua hiyo yenye aya moja tu, inasema: "Maisha ya utulivu na ya kunyenyekea yatakuletea furaha zaidi kuliko juhudi za kutafuta ufanisi na misukosuko inayoambatana na harakati na ufanisi huo."

Einstein aliamini kwamba Mungu yupo?
Einstein alikuwa kwenye kundi la watu ambao imani yao huitwa Pantheism kwa Kiingereza. Ni watu wanaoamini kwamba "Mungu ni kila kitu". Mara kadha, alionyesha mtazamo huu kwenye mawasiliano yake na Rabbi Herbert S. Goldstein, "Ninaamini katika Mungu wa Spinoza, ambaye anajidhihirisha kupitia upatanifu wa vitu vyote vilivyomo, si katika Mungu anayejishughulisha katika hatima na matendo ya binadamu."

Pantheism kwa njia rahisi zaidi ni imani kwamba kila kitu humwakilisha Mungu. Wenye kufuata imani hii mara nyingi hueleza kwamba Mungu ni vitu vyote vilivyopo, au kwamba mambo na vitu vyote ni Mungu.

Kwamba kila ukionacho ni sehemu ya Mungu.Aina ya Pantheism ya Spinoza aliyoiamini Einstein huamini kwamba kila kitu kinafanana na Mungu.

Kwamba Mungu hana ubinafsi na hayajali mambo ya binadamu. Kwa kila kitu kimeundwa na vitu vilevile vya msingi, ambavyo anatoka Mungu.

Kwamba Sheria za Fizikia hazina la kuzipinga, na kwamba kila jambo lina matokeo yake. Kila jambo linalotokea au kuwepo
lilitokana na hitaji lake kuwepo na lilikuwa nia ya Mungu.

Kwamba kwa binadamu, furaha na kuridhika maishani hutokana na kuifahamu dunia na vitu vinavyoizingira badala ya kuomba Mungu aingilie kati.

Benedict de Spinoza alikuwa mwanafalsafa Myahudi aliyezaliwa Uholanzi na wazazi Wayahudi kutoka Ureno Novemba 24, 1632, Amsterdam na akafariki Februari 21, 1677 mjini The Hague, Uholanzi.

Licha ya haya yote Einstein bado alidumisha baadhi ya tamaduni na mila za Wayahudi.

Hali kwamba alikuwa Mwanasayansi na kwamba aliongozwa na fikira katika kuufahamu ulimwengu ilimzuia kuwa na imani ambayo inaweza kuwafanya watu waseme alikuwa wa dini fulani.

Alikataa kupewa mazishi ya kitamaduni ya Wayahudi.

Ingawa bado alikuwa anazungumzia kuhusu kuamini kuhusu Mungu, alikuwa si Mungu wa dini za Kiabrahamu (Kikristo, Kiislamu na Kiyahudi ) na pia hakuwa Mungu anayerejelewa na watu walioamini kwamba Mungu yupo.

Alikuwa mara nyingi anajizuia kujiingiza kwenye mjadala kuhusu nani msema kweli, dini au sayansi.

Aidha, hakutaka kuamini kutumiwa kwa sayansi kama kielelezo katika kuamua maadili.

Wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, alinukuliwa akisema: "Bado wapo watu, wanaosema Mungu hayupo. Lakini kinachonighadhabisha zaidi ni kwamba huwa wananikuu wanapoeleza msimamo wao huo.

Bwana Kiranga natamani kusikia mtazamo wako kumhusu huyu mtu.
 
oscarsolomon

oscarsolomon

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Messages
3,920
Points
2,000
oscarsolomon

oscarsolomon

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2017
3,920 2,000
Kubashiri ndo kufnyaje? Imani kila MTU anayo usijifche .....maana hapo mwenyew unaamini dunia ilitokea kwa bing bang. Hivyo kusema hutak kuamini Ni ujuaji tu usio na maana.
Kama hutaweza kuthibitisha mungu yupo pasipo kutumia misingi ya kiimani basi ni wazi kabisa hujui chochote

Hakuna mtu au sayansi ikielezea kua muamini dunia ilitokea kwa bing bang bila uthibitisho

Unajua palipo na uthibitisho imani haiwezikani kuwepo?

Watu wanaamini kwasababu hawajui, wakijua wanakua wamekwisha kuthibitisha hivyo hakuna tena imani, imani ni doubt hivi unaelewa hilo?
 
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Messages
347
Points
250
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2014
347 250
Kila jambo la kiimani au kisayansi lazima liwe na ushahidi hakuna jambo ambalo halina exhibit tunalopaswa kuliamini.........(uwepo wa Mungu tunaufasiri kwa hivi tuvionavyo) sifa kubwa ya Mungu Ni uumbaji na hata sisi ni products zake, sasa kama yeye alisema kaumba kitu flani na kumbe alichokiumba hakipo au kama sisi tunaamini kuwa kaumba vitu flani ambavyo havipo basi ungelikuwa na haki yakutuona mapunguani lakin sisi tunaamini kuwa hivi tuvionavyo vimeumbwa na yeye tusiemuona.......sasa imani yetu ina exhibit hauna sababu yakukebehi namna hii brother

Kwaiyo huyo mungu hathibitishiki kua yupo si ndiyo?
 
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Messages
347
Points
250
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2014
347 250
mbona una quarto bila kuelewa kwanza? Au hujui maana ya kuthibitka!? Je! Unaweza kumthibtishiaje kipofu kuwa kuna kitu kinaitwa umeme? Em niambie Ni mbinu gani unaweza kutumia kumthibtshia MTU wa aina hii uwepo wa umeme?

Usinitoe kwenye mstari kwa kuja na mifano mfu hapa

Ujajibu swali usihamishe mjadala kwa kivuli cha kipofu

Unakubali kua uwepo wa mungu hauthibitishiki?
 
oscarsolomon

oscarsolomon

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Messages
3,920
Points
2,000
oscarsolomon

oscarsolomon

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2017
3,920 2,000
Kila jambo la kiimani au kisayansi lazima liwe na ushahidi hakuna jambo ambalo halina exhibit tunalopaswa kuliamini.........(uwepo wa Mungu tunaufasiri kwa hivi tuvionavyo) sifa kubwa ya Mungu Ni uumbaji na hata sisi ni products zake, sasa kama yeye alisema kaumba kitu flani na kumbe alichokiumba hakipo au kama sisi tunaamini kuwa kaumba vitu flani ambavyo havipo basi ungelikuwa na haki yakutuona mapunguani lakin sisi tunaamini kuwa hivi tuvionavyo vimeumbwa na yeye tusiemuona.......sasa imani yetu ina exhibit hauna sababu yakukebehi namna hii brother
Wapi ulipo thibitisha yupo zaidi ya kuongelea vitu ambavyo vinaleta maswali zaidi dhidi ya ulichokieleza

Uwepo wa mungu tunautafsiri kwa tuvionavyo

Hapo unaleta maswali mengine kua visivyoonekana pia siyo kazi yake hapo kunamfanya asiwepo kutokana na mambo mengine ameshindwa kuyaumba
 
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Messages
347
Points
250
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2014
347 250
Yaishe mkuu nafikiri umenielewa vema ila ubishi tu lakin labda nikutoe tongotongo Japo najua unafny makusud kutoelewa......iko ivi kama kitu hakionekan kwa macho ila athar zake zinahisika au kuonekana kulingana na sifa ya kitu hicho....(nakupa zoezi ...em kafikirie umeme upepo nguvu na akili pia... Na sifa ya kila kimoja wapo kat ya hivyo....(huwa tunavithibitsha kuwa vipo kwa namna gani then lete mrejesho)))).
Wapi ulipo thibitisha yupo zaidi ya kuongelea vitu ambavyo vinaleta maswali zaidi dhidi ya ulichokieleza

Uwepo wa mungu tunautafsiri kwa tuvionavyo[\b]

Hapo unaleta maswali mengine kua visivyoonekana pia siyo kazi yake hapo kunamfanya asiwepo kutokana na mambo mengine ameshindwa kuyaumba
 
oscarsolomon

oscarsolomon

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Messages
3,920
Points
2,000
oscarsolomon

oscarsolomon

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2017
3,920 2,000
Yaishe mkuu nafikiri umenielewa vema ila ubishi tu lakin labda nikutoe tongotongo Japo najua unafny makusud kutoelewa......iko ivi kama kitu hakionekan kwa macho ila athar zake zinahisika au kuonekana kulingana na sifa ya kitu hicho....(nakupa zoezi ...em kafikirie umeme upepo nguvu na akili pia... Na sifa ya kila kimoja wapo kat ya hivyo....(huwa tunavithibitsha kuwa vipo kwa namna gani then lete mrejesho)))).
We pimbi uwe unaelewa

Umeme upo na na unathibitishika kama upo ndio mana hapa hatubishani kuto kuwepo kwake unaelewa

Nilikukataza mwanzo kua mi sibishi mungu yupo eti kwasababu haonekani, vitu vingi havionekani lakini vinathibitishika kua vipo pasipo mkanganyiko wowote mfano umeme upo unathibitishika kwa mfano mdogo tu upepo unathibitishika hata kwa ngozi yako kua upo,

Unapozungumzia kua mungu ndiye muumbaji wa kila kitu hutakiwi kuweka ukomo kwenye kumuelezea kama ulivyo fanya kuelezea vitu alivyo viumba yeye aliumbwa na nani

Ulisema kua kaumba viumbe vilivyo na visivyo hai

Swali je huyo mungu ni kiumbe hai au kisicho hai?
 
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Messages
347
Points
250
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2014
347 250
We pimbi uwe unaelewa

Umeme upo na na unathibitishika kama upo ndio mana hapa hatubishani kuto kuwepo kwake unaelewa

Nilikukataza mwanzo kua mi sibishi mungu yupo eti kwasababu haonekani, vitu vingi havionekani lakini vinathibitishika kua vipo pasipo mkanganyiko wowote mfano umeme upo unathibitishika kwa mfano mdogo tu upepo unathibitishika hata kwa ngozi yako kua upo,

Unapozungumzia kua mungu ndiye muumbaji wa kila kitu hutakiwi kuweka ukomo kwenye kumuelezea kama ulivyo fanya kuelezea vitu alivyo viumba yeye aliumbwa na nani

Ulisema kua kaumba viumbe vilivyo na visivyo hai

Swali je huyo mungu ni kiumbe hai au kisicho hai?
Kwa kuwa umeona kutukana ndio suluhisho LA dhamir yako sihukumu katka hilo.
.ila naenda kukujibu swali lako juu ya kile ninachojua kuhusu Mungu ninaemwabudu Mimi.
.
Mkuu.
.Mungu si nafsi iliyotokana na kitu kingne si matunda ya uumbaji hata ivo nashangaa kama Mungu angeiona hoja hii yote kuwa nyepesi namna hii.
Kwasababu tunafikiri kuhusu VYANZO Ndani ya muda na pia ndani yake .na kama muda nikitu kimojawapo kilichoumbwa na Mungu, basi kusema kuwa hali ilikuaje kabla ya kuwepo Mungu Ni kujipinga.

Mimi.naishia hapa mkuu mengne tutakutana nayo katka mazngira tunamoishi na yatatufundsha mengi kuhusu yeye aliye Mungu.

Ila matusi Ni dalili ya MTU ambaye hajitambui na hayuko tayari kujitambua.

Kwaheri
 
oscarsolomon

oscarsolomon

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Messages
3,920
Points
2,000
oscarsolomon

oscarsolomon

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2017
3,920 2,000
Kwa kuwa umeona kutukana ndio suluhisho LA dhamir yako sihukumu katka hilo.
.ila naenda kukujibu swali lako juu ya kile ninachojua kuhusu Mungu ninaemwabudu Mimi.
.
Mkuu.
.Mungu si nafsi iliyotokana na kitu kingne si matunda ya uumbaji hata ivo nashangaa kama Mungu angeiona hoja hii yote kuwa nyepesi namna hii.
Kwasababu tunafikiri kuhusu VYANZO Ndani ya muda na pia ndani yake .na kama muda nikitu kimojawapo kilichoumbwa na Mungu, basi kusema kuwa hali ilikuaje kabla ya kuwepo Mungu Ni kujipinga.

Mimi.naishia hapa mkuu mengne tutakutana nayo katka mazngira tunamoishi na yatatufundsha mengi kuhusu yeye aliye Mungu.

Ila matusi Ni dalili ya MTU ambaye hajitambui na hayuko tayari kujitambua.

Kwaheri
Hujathibitisha mungu yupo zaidi ya kunichanganyia habari zingine zinazo zaa maswali mengine mapya

Unavyo muelekeza mtu kuhusu utata wa neno au kitu usitumie maneno tata yenye kuzaa maswali mengine, ukifanya hivyo mjadala unauhamisha kwenda kwenye hilo neno tata ulilolitumia kama ufafanuzi wa utata wa neno la awali

Nafsi ni nini?

Hapo mjadala ulikua ni wewe uthibitishe mungu yupo pasipo kujipinga, sasa naona unataka kuupeleka kwingine kutokana na hoja unazotumia kuichambua mada yako kua na utata
 
dramaqueen1

dramaqueen1

Senior Member
Joined
Apr 23, 2018
Messages
115
Points
250
dramaqueen1

dramaqueen1

Senior Member
Joined Apr 23, 2018
115 250
Shetani hutumia wasomi sababu wanaaminiwa na watu. Mungu hutumia viumbe dhaifu na kuwapatia nguvu ili waguse imani za watu
 
kurlzawa

kurlzawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2018
Messages
6,423
Points
2,000
kurlzawa

kurlzawa

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2018
6,423 2,000
Hauna ubongo kichwani maana unaandika utumbo tupu
mbona una quarto bila kuelewa kwanza? Au hujui maana ya kuthibitka!? Je! Unaweza kumthibtishiaje kipofu kuwa kuna kitu kinaitwa umeme? Em niambie Ni mbinu gani unaweza kutumia kumthibtshia MTU wa aina hii uwepo wa umeme?
 
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Messages
347
Points
250
Anikajema

Anikajema

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2014
347 250
Hauna ubongo kichwani maana unaandika utumbo tupu
Huna hoja ya msingi bila shaka wewe. Ni Moja wapo wawatu wanaotetewa na wazungu kupatiwa haki zao kwenye nchi ya tz.... Subiri nitaleta posa sheria ikipitishwa.
 
Forum statistics

Threads 1,315,253
Members 505,171
Posts 31,851,499
Top