Muke Ya Muzungu
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 3,444
- 265
Mh. Rais, Jakaya Mrisho Kikwete
Nakuandikia nikiamini kwamba umzima wa afya huko Magogogoni st. ukilitumikia Taifa letu kwa uadilifu. nimeamua kutumia mtandao kwa maana barua nyingi nilizokutumia hazikufikii kwa maana sijawahi kupata jibu lako, wal sijaona hatua yoyote ikichukuliwa kusuluhisha matatizo yanayotukaili. Kwanza Kabisa napenda kujitambulisha kama Mwana UVCCM, mzaliwa wa Nyamongo wilayani Tarime.Mheshimiwa Rais, nikiwa kijana mdogo katika miaka ya 90, familia yangu na nyingine huko nyamongo ilitegemea kilimo, ufugaji pamoja na uchimbaji wa dhaabu ili kujikimu. Tumekuwa kwa furaha hasa kwa kile kidogo tulichokuwa nacho. Tumewasaidia wazazi wetu kazi nyingi za shamba na pia kuchimba dhaabu. Tumesomeshwa na hizi shughuli ndogondogo, na kwa hakika, maisha ya mbeleni yalikuwa na matumaini makubwa
Nikiwa mzalendo na kijana anayeamini ustaarabu katika kutatua matatizo yetu, nimeamua kukuandikia ili kutoa dukuduku langu na pia kutafuta suluhisho la kudumu kuhusiana na matatizo makubwa tunayokabiliana nayo. Takribani miaka sita iliyopita, nyumba yetu, pamoja na mashamba tuliyokuwa nayo yalichukuliwa na serikali. Tulilipwa kiasi cha shilingi million 6. Tukaanza maisha mapya ambayo hatukuyajua. Miaka sita baadae, hali yetu imedorora na kuwa mbaya zaidi. Tumeingia katika bahari ya ufukara na ukiwa. Ng'ombe, wetu wote wamefariki baada ya kunywa maji machafu kutoka katika mto tulioutegemea maisha yetu yote. Shamba tulilolitegemea kwa uchimbaji na kilimo wamepewa BARRICK Gold. Baba yangu, mdogo wangu wa Kike, waliugua ghafla magonjwa ya ajabu iliyofanya ngozi zao kukatika vipande vikubwa vikubwa na kutapika damu kwa wingi na hatimaye kufariki dunia. Mwanangu wa miaka 4, pia tunawasiwasi atakufa hivi karibuni.
Mheshimiwa Rais, wiki chache zilizopita, kaka yangu, ambaye alibaki nguzo ya familia, kutokana na ukiwa na umasikini, aliamua kwenda kuokota mawe kutoka katika shamba letu waliopewa Barrick, akiwa na vijana wenzake wanaokota mawe, walikuja polisi, na kuwaambia waondoke. Kukumbuka ardhi waliyokulia, amepewa mtu mwekezaji, waligoma kuondoka. Hapo ndipo Polisi, ambao inabidi watulinde waliwapiga risasi migongoni na kuwauwa. Matokeo yake wakaitwa majambazi na wahuni. Hapana, kaka yangu hakuwa jambawazi wala muhuni. Alienda kuokota mawe ambayo yalitupwa ili angalau apate chochote
Mh. Rais, sisi siyo ombaomba. Wakurya ni wachapakazi na wakulima hodari. Hatutaki Misaadi kutoka kwa mtu. Tatizo letu ni unanyasaji ambao unafanywa na serikali ya Tanzania kwa niaba ya Barrick Gold. Mh. Rais, nina maswali machache ambayo kama mzalendo, nadhani utaweza kuyashugulikia ikiwa wewe ni mtu mpenda amani
Majeshi makubwa yenye nguvu hayawezi kuzuia nguvu ya umma. Ikiwa wewe ni mtu anayeweza kuona mbali, kwa heshima na taadhima, tunakuomba na kukusihi kwa dhati uliokoe taifa la Tanzania pamoja na utawala wako. Tunakuomba ulifunge mgodi wa North Mara na Kusitisha mkataba wa Barrick Gold Tanzania. Hili ni shirika lenye historia mbaya ya unyanyasaji kote duniani. Wanatuibia na mnaona, hawalipi kodi wala kuchangi chochote hapa nchini. kila siku wanasafirisha michanga na ndege na serikali yetu iko kimya, na hata kufikia hatua ya kubisha kwamba muwekezaji hawasafirishi mchanga
Nashukuru kwa kunisikiliza, na pia kuweza kuchukua maamuzi ya haraka kuhusu Barrick Gold, vinginevyo barua yangu uitunze kama kumbukumbu kuashiria mchakato mpya wa kimapinduzi ya aina yake Barani Afrika. Hatutanyamazishwa na bunduki wala mzinga. Tutakufa wote hadi hapo Barrick Watakapooondoka nchini kwetu. Ukizima, maoni yangu, basi utambue kwamba watu million 40 wapo tayari kuchukua hatua ili kuondokaa na unyanyasaji. Mapinduzi yanyoendele katika nchi za kiarabu ilianzishwa na kijana mmoja nchini tunisia aliyejitoa mhanga kwa kijiwasha moto akipinga unyanyasaji... Tanzania hali mbaya ya sasa ikiendelea, basi mwisho utakuwa mbaya kwako na serikali yako. Tunakuomba ujiuzulu kwa niaba ya CCM na Tanzania. Fanya ustraarabu kama Thabo Mbeki, iokoe Tanzania, zuia umwagikaji wa damu kwani nchi inaelekea kubaya
[video=youtube_share;9tSDVM327uo]http://youtu.be/9tSDVM327uo[/video]
[video]http://phillipmogendi.com/plugins/content/jw_allvideos/includes/players/mediaplayer/player.swf[/video]
[video]http://phillipmogendi.com/plugins/content/jw_allvideos/includes/players/mediaplayer/player.swf" [/video]

- Kwa nini serikali yetu ituue na kutuita sisi wahuni wakati tunachokitafuta ni kuishi na kulisha watoto wetu? Ndugu zetu hawakuenda kuiba, bali kuokota mawe iliyotupwa na Barrick Gold
- Kwa nini tuingie kwenye umasikini zaidi, wakati hapo hawali tulitegemea hii migodi kujikimu?
- Wewe kama mzazi, unaweza kukubali wanao kama Khalfani na Ridhiwani kuuwawa wakiokota maembe kwenye shamba lako huko chalinze?
- Kwa nini Chama Cha Mapinduzi inazuia Mjadala wa Migodi ya Nroth Mara Bungeni?
- Je ni halali huyu mwekezaji kutuachia mashimo ilhali keshachukua mali zetu zote? Haya mashimo tutayafukia vipi?
- Utajisikiaje baba yako, kaka yako, na mdogo wako kuuwawa kinyama kwa sababu ya mwekezaji?
- Kwa nini mashamba yetu, na dhaabu zetu zitoe ajira kwa wageni (makaburu, wakenya na mataifa mengine) wakati sis wazawa hatukubaliki kwenye hii migodi. Mkenya kachangia nini kwenye mgodi wa North Mara, au mkaburu kwa nini aendeshe trekta?
Majeshi makubwa yenye nguvu hayawezi kuzuia nguvu ya umma. Ikiwa wewe ni mtu anayeweza kuona mbali, kwa heshima na taadhima, tunakuomba na kukusihi kwa dhati uliokoe taifa la Tanzania pamoja na utawala wako. Tunakuomba ulifunge mgodi wa North Mara na Kusitisha mkataba wa Barrick Gold Tanzania. Hili ni shirika lenye historia mbaya ya unyanyasaji kote duniani. Wanatuibia na mnaona, hawalipi kodi wala kuchangi chochote hapa nchini. kila siku wanasafirisha michanga na ndege na serikali yetu iko kimya, na hata kufikia hatua ya kubisha kwamba muwekezaji hawasafirishi mchanga
Nashukuru kwa kunisikiliza, na pia kuweza kuchukua maamuzi ya haraka kuhusu Barrick Gold, vinginevyo barua yangu uitunze kama kumbukumbu kuashiria mchakato mpya wa kimapinduzi ya aina yake Barani Afrika. Hatutanyamazishwa na bunduki wala mzinga. Tutakufa wote hadi hapo Barrick Watakapooondoka nchini kwetu. Ukizima, maoni yangu, basi utambue kwamba watu million 40 wapo tayari kuchukua hatua ili kuondokaa na unyanyasaji. Mapinduzi yanyoendele katika nchi za kiarabu ilianzishwa na kijana mmoja nchini tunisia aliyejitoa mhanga kwa kijiwasha moto akipinga unyanyasaji... Tanzania hali mbaya ya sasa ikiendelea, basi mwisho utakuwa mbaya kwako na serikali yako. Tunakuomba ujiuzulu kwa niaba ya CCM na Tanzania. Fanya ustraarabu kama Thabo Mbeki, iokoe Tanzania, zuia umwagikaji wa damu kwani nchi inaelekea kubaya
[video=youtube_share;9tSDVM327uo]http://youtu.be/9tSDVM327uo[/video]
[video]http://phillipmogendi.com/plugins/content/jw_allvideos/includes/players/mediaplayer/player.swf[/video]
[video]http://phillipmogendi.com/plugins/content/jw_allvideos/includes/players/mediaplayer/player.swf" [/video]
[video]http://phillipmogendi.com/plugins/content/jw_allvideos/includes/players/mediaplayer/player.swf" [/video]
Last edited by a moderator: