Barua kwa John Pombe Magufuli

Barua kwa John Pombe Magufuli

Tatizo umeandika kinafiki, una ndimi 2. Inaonesha kuna mahali haupo sawa.
Ni kweli. Kwa mtu mnafiki, nimeandika kinafiki. Kwa mtu ambaye hayuko sawa, kweli kuna mahali siko sawa. Kwa mtu asiye sawa anayewahukumu wenzake bila kueleza hata anatumia vigezo au ujuzi gani hasa ikizingatiwa hawajui, siko sawa sawa naye asivyo sawa. Shukran.
 
JohPombe Magufuli Jiwe,

Nikiri. Najua hutasoma barua hii.
Najua wafuasi wako wataisoma. Naandika kwa hasira na uchungu. Yote ni kutokana na uliyotufanyia. Uliachia maumivu. Wapo wanaoumia tokana na pengo uliloacha. Pia, wapo wanaoumia kwa sababu ya ubaya ulioacha.

Bwana John, ni vigumu kwangu kukuelezea ilivyo. Ulikuwa kama kitunguu. Kikitumika kuungia mboga, kila mtu ataipenda. Ulijenga miundo mbinu na kuwabana wapigaji
Mkumbuke Bashiti wako.

Unakumbuka namna Bashungwa alivyokupigia magoti ukampa uwaziri? Ulifurahisha wengi. Uliiokoa wengi. Ulikembea mabeberu na kuamua kujitegemea kama taifa.
u mwamba kama Mwalimu Nyerere. kwa kujali watu na mjamaa. Kama Nyerere, ulifanya mema kiasi cha kukuita shujaa.

Tunapomaliza mwaka, sitaki niandike mengi. Ila huko uliko, ujue. Umetuachia ambavyo, vitachukua miaka mingi kuviondosha.
Rest John Pombe Magufuli.
JPM yupo!, huko alipo anakusoma!.

Ili kujua kuwa JPM yupo na anakusoma, anzia hapa' Life after Death: What happens after death?

Kisha njoo hapa
Life After Life: Je, wajua Magufuli huko alipo anayaona yote? Je, tuendeleze 'double standards' ya 'cherry picking' au tuiachie Karma iwashughulikie?

Ila pia jf tuna mijitu ya ajabu!, juzi kati kuna majitu yamewaua Watanzania kwa kuwamiminia risasi za moto vijana wetu hadi vitoto vichanga, badala ya kuwashutumu wauwaji hawa. jitu linaibuka siku ya krismasi na kumshutumu mtu aliyeisha twaliwa kitambo., amepita hukumuni mbele ya haki na sasa yuko peponi Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

Merry Christmas

P
 
Jamaa alikuwa mzalendo na alikuwa anajua kupiga mzigo, lakini legacy yake nyingine aliyoiachia Taifa ni wizi wa kura, utekaji na mauaji, madhara yake tumeyaona 2025
 
View attachment 3519648
JohPombe Magufuli Jiwe,

Nikiri. Najua hutasoma barua hii. Najua wafuasi wako wataisoma. Naandika kwa hasira na uchungu. Yote ni kutokana na uliyotufanyia. Uliachia maumivu. Wapo wanaoumia tokana na pengo uliloacha. Pia, wapo wanaoumia kwa sababu ya ubaya ulioacha.

Bwana John, ni vigumu kwangu kukuelezea ilivyo. Ulikuwa kama kitunguu. Kikitumika kuungia mboga, kila mtu ataipenda. Ila kikupasukia machoni, utakichukia na kujutia. Ulijenga miundo mbinu na kuwabana wapigaji ilhali ukiruhusu machawa wako kupiga na kuumiza. Mkumbuke Bashiti wako. Uliumiza wengi ulipoanzisha utekaji, upotezaji, na uuaji. Ulilite uchawa kwenye serikali yako na nchi yetu. Unakumbuka namna Bashungwa alivyokupigia magoti ukampa uwaziri? Hapa, ndipo chanzo cha uchawa kilipo.

Ulifurahisha na kukasirisha wengi. Uliiokoa na kuumiza wengi. Ulituachia mijitu ya hovyo ambayo, kwa sasa, imegeuka kansa kwa taifa. Uliua kwa siri. Haya majitu yako yaua wazi wazi. Ulikembea mabeberu na kuamua kujitegemea kama taifa. Mijitu yako inawakemea siyo kwa kutaka tujitegemea bali kwa kuambiwa ukweli.

John, iwe ni kwa bahati mbaya au makusudi, ulituumiza. Madhara ya sera na siasa zako yatachukua miaka kuondoka. Ulichofanya siyo cha kujivunia wala kufurahia bali kulaaniwa hata kama haupo.

Wapo wanaokuona u mwamba kama Mwalimu Nyerere. Naye alituachia viiio kwa kujenga mfumo wa kifalme huku akijifanya kujali watu na mjamaa. Kama Nyerere, ulifanya mema na mabaya karibia sawa kiasi cha kushindwa kukuita shujaa.

Ulijiinua na kutuangusha. Na mijitu yako inasoma kitabu kile kile. Ulituganya wanyonge. Mijitu yako imetufanya machawa.

Tunapomaliza mwaka, sitaki niandike mengi. Ila huko uliko, ujue. Umetuachia maumivu na uchafu ambavyo, licha ya kutugharimu na kutuumiza, vitachukua miaka mingi kuviondosha.
Rest in Trouble John Pombe Magufuli.
Kafi®we Huko ulipozoea.
 
Back
Top Bottom