The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 10,959
- 13,429
JohPombe Magufuli Jiwe,
Nikiri. Najua hutasoma barua hii. Najua wafuasi wako wataisoma. Naandika kwa hasira na uchungu. Yote ni kutokana na uliyotufanyia. Uliachia maumivu. Wapo wanaoumia tokana na pengo uliloacha. Pia, wapo wanaoumia kwa sababu ya ubaya ulioacha.
Bwana John, ni vigumu kwangu kukuelezea ilivyo. Ulikuwa kama kitunguu. Kikitumika kuungia mboga, kila mtu ataipenda. Ila kikupasukia machoni, utakichukia na kujutia. Ulijenga miundo mbinu na kuwabana wapigaji ilhali ukiruhusu machawa wako kupiga na kuumiza. Mkumbuke Bashiti wako. Uliumiza wengi ulipoanzisha utekaji, upotezaji, na uuaji. Ulilite uchawa kwenye serikali yako na nchi yetu. Unakumbuka namna Bashungwa alivyokupigia magoti ukampa uwaziri? Hapa, ndipo chanzo cha uchawa kilipo.
Ulifurahisha na kukasirisha wengi. Uliiokoa na kuumiza wengi. Ulituachia mijitu ya hovyo ambayo, kwa sasa, imegeuka kansa kwa taifa. Uliua kwa siri. Haya majitu yako yaua wazi wazi. Ulikembea mabeberu na kuamua kujitegemea kama taifa. Mijitu yako inawakemea siyo kwa kutaka tujitegemea bali kwa kuambiwa ukweli.
John, iwe ni kwa bahati mbaya au makusudi, ulituumiza. Madhara ya sera na siasa zako yatachukua miaka kuondoka. Ulichofanya siyo cha kujivunia wala kufurahia bali kulaaniwa hata kama haupo.
Wapo wanaokuona u mwamba kama Mwalimu Nyerere. Naye alituachia viiio kwa kujenga mfumo wa kifalme huku akijifanya kujali watu na mjamaa. Kama Nyerere, ulifanya mema na mabaya karibia sawa kiasi cha kushindwa kukuita shujaa.
Ulijiinua na kutuangusha. Na mijitu yako inasoma kitabu kile kile. Ulituganya wanyonge. Mijitu yako imetufanya machawa.
Tunapomaliza mwaka, sitaki niandike mengi. Ila huko uliko, ujue. Umetuachia maumivu na uchafu ambavyo, licha ya kutugharimu na kutuumiza, vitachukua miaka mingi kuviondosha.
Rest in Trouble John Pombe Magufuli.