Barua hii ya Kijasusi kutoka Uingereza kuhusu uchunguzi wa mtoto wa mgombea Urais Mtarajiwa ....

Status
Not open for further replies.
Tunasema hiyo Nyumba huko uingereza itaifishwe.mtoto babake kamfundisha wizi.
 
Huyu aliyeileta hii, ameileta kwa sababu ndiyo aliyokuwa nayo hadi sasa. Yeye anaamini kuwa huyu LOWASSA bado hajasafishwa, maana hajaiona hiyo nyingine ya kumsafisha LOWASSA. Cha msingi ni hiki: kama wewe unayo hiyo nyingine ambayo imemsafisha LOWASSA, basi ilete jamvini tuione. Huwezi kusema LOWASSA alishasafishwa bila kutuwekea barua ya kumsafisha. Swala jingine kuhusu "For Intelligence Use Only": Ni nani aliyekuambia kuwa kila lililo la siri basi ni la siri? Litakuwa la siri kama limeendelea kuwa la siri, bali likishabumburuka kwa watu haliwi la siri tena. Hata kama limeandikwa ni la kiintelijensia, basi nasi tunakuwa sehemu ya intelijensia hiyo maana tumeshalifahamu tayari! Acha ushabiki, kuwa na uchungu kwa taifa lako Mkuu.
 
UK kwenye uchunguzi hawaangalii mtu na wapo makini sana. Frederick mpaka leo yupo mtaani, jibu utakuwa nalo. Ndo wanaziita siasa za maji taka hizo!
 
acha PROPAGANDA zako wewe! hii barua ipo kitambo tu humu JF, miaka sita imepita hakuna chochote kilichothibitishwa
ila nashukuru kama CHAGADEMA mnamtambua kuwa EL ndio mgombea wa chama tawala

Soma thread usikurupuke. Hujaambiwa ni mpya. Umeulizwa kama ilishawahi kutolewa maelezo?
 

Uzuri katika hili ni kukubali kuwa Alisha chafuka na juhudi zinafanywa kumsafisha. Watanzania hawataki kiongozi aliyewahi kuchafuka kama EL
 
saa nane ni kama mtu aliyeacha mke huku anampenda, kila saa ni kumuwaza na kumuonea wivu. huyu jamaa akili yake yote iko CCM
 
miaka 6 sasa tusisikie matokeo, hamna kitu hapo.
ijapokuwa hakuna anayejua authenticity ya hiyo barua.
 

Kweli ukipenda hata chongo unaona kengeza ......................... This letter is clearly dated 21st of May 2009. Where the hell did you get that F%$#n 1990!!? Hivi 1990 Lowasa alikuwa ni Former PM!!?

Kwa vile serikali haijatupa majibu basi kuna haja ya kufuatilia ili ukweli ujulikane. Si huwa mnadai siyo Fisadi, sasa tuambieni hizo pounds amezitoa wapi!!?
 
Bado na wewe ni walewale wajadilio mambo kwa mihemko! Soma tena maoni yangu utaelewa vizuri wewe Mr. Zero! Watu hamwelewi Kiswahili, mkiandikiwa Kiingereza si ndo mtaingia chaka kabisa!
 
Lowasa kwa utendaji kazi ni mzuri sana na hamna wa kufananisha naye . Kasoro yake moja tu fedha sijui hufiche wapi akiziona tu shiiiiiiiidaaaaaaa
 

huo mwaka 1990 katolea mfano.mbona hamtulii mkasoma mkaelewa papara za nini?
 
huo mwaka 1990 katolea mfano.mbona hamtulii mkasoma mkaelewa papara za nini?
Ndio hao hao walio mstari wa mbele kutuletea hili liFISi lije kuendeleza alipoishia Mr Dhaifu na hivyo tuishe kabisa!!! Kwa nini watu wanag'ang'ania mafisi yale yale, wizi ule ule, mambo yale yale, mawazo na fikira zile zile..? Wabongo aliyetuloga alikwishafariki na hakuna wa kutulogoa!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…