Barrick vs Tanzania: Tukubali tu kwamba tumezidiwa ujanja na Wazungu

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,603
2,000
1. Hakuna kubadili sheria ya madini mpaka Barrick waondoke nchini.

2. Hakuna kuishtaki Barrick mahakama za ndani.

3. Barrick haitajisajili ndani ya DSE.

4. Hakuna Mtanzania atakayeweza kununua hisa kwenye kampuni.

5. Serikali itapata share ya net profit na net loss kwa 50%.

Kwa mkataba huu tumepakatwa na hatuna pa kutokea uzalendo kweli ndio huu?

Kabudi Mungu anakuona
 

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
12,979
2,000
Hivi pale ikulu JK na Mkapa walikuwepo? Vipi zile kesi za watingaji waliodhulumiwa ajira?
 

Ole

JF-Expert Member
Dec 16, 2006
1,760
2,000
technically,
1. Toa ushahidi ulionao.
2. Barrick ni shareholder wa kampuni ya Twiga pamoja na TZ Government.
3. Twiga watajisajili DSE
4. Unaweza kununua shares za Twiga DSE au Barrrick LSE, CNSX au NSE popote unaponunua its value will be the same. (ie determined by the market)
5. Usitegemee kupata faida wakati hakuna uzalishaji.
 

Ole

JF-Expert Member
Dec 16, 2006
1,760
2,000
Hivi unakuwaje na ubia wa usawa wakati unamiliki asilimia 16 na mwenzako 84
Asilimia hizo ni share holding, ie 16% ya shares zote za Barrick na wao Barick wanamiliki 84%.(In actual fact hizo 84% wanaweza wasizimiliki wao Barrick kwa sababu kila mtu ana uhuru wa kununua shares kwenye stock exchange worldwide ie From Hong Kong, Tokyo, Melbourne, London, Paris, New York au Toronto etc.

Kampuni huwa na shares 100 percent ambazo zinajulikana, sifahamu Barrick wana kiasi gani cha shares, usichanganye number of shares na percentage. (FYI shares za Barrick ni worldwide wana chimba Gold kila mahali ulimwenguni na makadirio yao kipato kinachopatikana Tanzania ni kama 16% ya value ya Barrick worldwide, that is why Twinga wapo 50-50 percentagewise. Natumaini unaweza kuwa umeambulia kitu.
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,065
2,000
Ole,
Ninakushukuru sana kwa kutoa elimu nzuri kwa mleta mada lakini naomba uelewe kuwa tatizo la wengi hapa Jamiiforums wanadhani wanajua wakati hawajui. Wengine wanadhani mambo ya siasa ni sawa na ushabiki wa vyama vya michezo kama simba na yanga!

Mtu anayedhani anajua wakati hajui ni vigumu sana kuelimishwa na kuelimika!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom