Njowepo
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 9,710
- 2,227
Barrick Gold kuchangia Sh16 bilioni kwa maendeleo ya jamii |
Wednesday, 07 September 2011 21:30 |
Mwandishi Wetu/mwananchi news paper KAMPUNI ya African Barrick Gold (ABG) imezindua mfuko wa maendeleo kwa jamii na kuidhinisha Sh 6 bilioni kila mwaka. Mfuko huo ndiyo utakaokuwa kitengo cha uwajibikaji kwa jamii cha ABG. Akizindua mfuko huo jana, Mjumbe Huru wa Bodi ya Kampuni ya Barrick Gold, Balozi Juma Mwapachu alisema Bodi ya ABG imeidhinisha bajeti ya Sh16 bilioni kila mwaka kwa ajili ya mfuko huo na hivyo kudhihirisha msimamo wa kampuni wa kufanikisha maendeleo endelevu nchini Tanzania na kusaidia kuboresha maisha ya watu.Alisema uzinduzi wa mfuko huo jana utaunda uwekezaji mkubwa zaidi kwenye jamii kuwahi kufanywa Tanzania na kampuni yoyote ile. "Tunapolenga kodi ya mapato tu na au mrabaha tunasahau mchango mkubwa sana unaofanywa na kampuni hizi kwenye uchumi wa nchi, hebu chukulia mfano wa ABG imetoa ajira za moja kwa moja kwa Watanzania zaidi ya 8,800, lakini pia imefanya manunuzi ya bidhaa na huduma ya mamilioni ya shilingi, hii ni faida kwa uchumi wa nchi yetu, lazima tuliangalie hili," alisema. |
Kama mwaka jana walizalisha ounces 564,000 lets assume the same mwaka huu.
http://www.barrick.com/GlobalOperations/Footnotes/default.aspx
With 564,000 ounces kwa bei ya sasa ya 1600 usd kwa ounces unapata 1.4 trillion za kitanzania kwa exchange rate ya 1600.
Sasa iyo 16 billion waliotoa ni sawa na 1.1% ya mapato yao ndugu yangu Mwapachu ilo nalo la kulitetea?
Izo ajira 8800 kama ni kwa watanzania uliza wanalipwa tsh ngapi na madhara wanayopata kiafya kwa kwenda chini sometimes umbali wa mita 600 leave alone mionzi wanayopigwa kudhibiti wizi wa dhahabu.
As data zao wenyewe zinonyesha 2004 Bulya 349,864 ounces,buzwagi 189,000 ounces,North Mara 280000 ounces na Tulawaka 124743 ounces grand total ni 942000 ounces apprx
Jamani tupeni data za ukweli maana mara 564000 ounces mara 942000 ounces which is which
Ni matumaini yangu izo ounces zaongezeka on the year basis ndo maana bado mpo mnachimba
http://www.tanzaniagold.com
Maombi yangu
1.Retain some of the money in Tz to stabilize our currence as iyo gold ni ya Tanzania
2.Muanze kulipa kodi ili muipiku TBL katika ulipaji wa kodi as mko na migodi mine you deserve to be topping the list
3.Mchango wenu angalau ufike 10% from 1.1% angalau nasi tufeel kuwa Gold inachimbwa Tz
Vinginevyo migogoro na wananchi pamoja na kelele za wananchi juu ya ABG hazitakoma milele.
4.Hao watu 8800 let them be paid kwa rate sambamba ni migodi mingine angalau Africa maana nkisema ulaya ntakuwa nimeenda mbali.You the rates that other mines get paid