Bariadi: Askari polisi aliyegonga gari la RPC Chatanda afariki dunia

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,828
21,460
Timoth Philipo, askari polisi wilayani Busega amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Simiyu baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongana na gari lililokuwa likiendeshwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda.

Taarifa iliyotolewa na kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Shadrack Masija leo Jumatano Oktoba 5, 2022 inaeleza kuwa ajali hiyo ilitokea Oktoba 2, 2022 eneo la Mizani Nyakabindi ikimhusisha Chatanda na Philipo.

"Toyota Harrier ilikuwa ikiendeshwa na ACP Chatanda iligongwa na Toyota Mark II ikitokea Bariadi kwenda Lamadi ikiendeshwa na Philipo na kusababisha majeraha kwa madereva wote wawili pamoja na H. 7123 Pc Emmanuel ambaye ni msaidizi wa Chatanda," amesema.

Amebainisha kuwa majeruhi wote walifikishwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya matibabu na kubainisha kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wa Philipo ambaye alihama upande na kwenda upande wa kulia na kisha kuligonga gari liliokuwa likiendeshwa na Chatanda.

Amesema Philipo alifariki dunia Oktoba 3, 2022 akiwa anapatiwa matibabu ikielezwa kuwa sukari ilishuka.
Katika taarifa hiyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limetoa pole kwa ndugu na familia ya marehemu na taratibu za mazishi zinafanyika kwa kushirikiana na familia na mwili utasafirishwa kwenda Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya mazishi.

Chanzo: Mwananchi
 
Watuambie chanzo cha ajali na ni nani alikuwa mzembe. Ajali za kugongana mara nyingi mmoja wa madereva kafanya uzembe wa kutofuata sheria.

Sasa nani alifanya hivi kati ya hawa wawili, maana wao wanajua kulima watu fine -- ooh ume-overtake kwenye solid line.

Sasa nani kasababisha hii ajali hapa ikiwa wote wawili wanapaswa kuwa vinara wa kufuata sheria?
 
Poleni

Sasa kama watunza usalama ndiyo hao nini sababu ya kutuandama wengine
 
chanzo cha ajali ni uzembe wa Philipo ambaye alihama upande na kwenda upande wa kulia na kisha kuligonga gari liliokuwa likiendeshwa na Chatanda
... nilitegemea hilo; kwamba jumba bovu ataangushiwa Philipo! Kama amehama kwenda kulia kisha kumgonga RPC maana yake RPC naye alikuwa amehama. In short, wote walikuwa wana-overtake, sema RPC alikuwa slow.
 
Timoth Philipo, askari polisi wilayani Busega amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Simiyu baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongana na gari lililokuwa likiendeshwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda.

Taarifa iliyotolewa na kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Shadrack Masija leo Jumatano Oktoba 5, 2022 inaeleza kuwa ajali hiyo ilitokea Oktoba 2, 2022 eneo la Mizani Nyakabindi ikimhusisha Chatanda na Philipo.

"Toyota Harrier ilikuwa ikiendeshwa na ACP Chatanda iligongwa na Toyota Mark II ikitokea Bariadi kwenda Lamadi ikiendeshwa na Philipo na kusababisha majeraha kwa madereva wote wawili pamoja na H. 7123 Pc Emmanuel ambaye ni msaidizi wa Chatanda," amesema.

Amebainisha kuwa majeruhi wote walifikishwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya matibabu na kubainisha kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wa Philipo ambaye alihama upande na kwenda upande wa kulia na kisha kuligonga gari liliokuwa likiendeshwa na Chatanda.

Amesema Philipo alifariki dunia Oktoba 3, 2022 akiwa anapatiwa matibabu ikielezwa kuwa sukari ilishuka.
Katika taarifa hiyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limetoa pole kwa ndugu na familia ya marehemu na taratibu za mazishi zinafanyika kwa kushirikiana na familia na mwili utasafirishwa kwenda Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya mazishi.

Chanzo: Mwananchi
R.I.P POT
 
Back
Top Bottom