Baraza la viongozi wastaafu wa CCM

Baraza la viongozi wastaafu wa CCM

‘... Ukiona mtu anakufitini Mwambie Waziwazi, ukiona anabadilika basi tambua aliteleza nawe msamehe, ukiona anaendelea tambua hakukosea amekusudia kukuharibia,

hakikisha hakuharibii ila wewe usimuharibie mengine zaid ya kuharibu lengo lake la kukuharibia...’

Mmoja wa Wazee wa Kamati hiyo ya Wazee aliwahi kutupiga somo hilo na akawa anarudia Mara kwa Mara enzi hizooooo

Mwisho wa mchakato huu wa Clinic ya kuimarisha Afya ya Siasa ndani ya Chama I’m very sure Ccm itaibuka mshindi dhidi ya Wahuni wanaojaribu kutaka kumtoa Rais kwenye Msingi wa Chama
Hueleweki kama k
 
Hili jambo siyo jepesi , hii ndio hatua ya mwanzo ya mtu wa kwanza Tanzania kuwa Rais kwa miaka mitano tu ( 1 term president )

That is the bottom line. Lengo kuu la waraka ni kufikisha kwa umma ujumbe kuwa kwa mtazamo wa wenye chama chao mambo siyo shwari tena.
 
Hao wanajeshi hawana hilo, wanaangalia mishahara yao kwanza, hayo mengine ni mbwembwe tu.
Aisee ishu ingekuwa rahisi hivyo wala kusingekuwa na kitu kinaitwa uasi.
 
Namshukuru sana Mungu anawalipa wote waliotuletea shida sie wanadamu nao wanakinywea kikombe kile kile, cha kuisoma namba.Walikijua kikombe Kwa nje kumbe ndani cha moto,awakupaza sauti wapinzani walipokuwa wakifanyiziwa kama mbwa kokoko,nyoka akiingia ndani ya nyumba achagui,sie tulizoea kuisoma hivo nao watulie tu tuzame wote.
 
Aisee ishu ingekuwa rahisi hivyo wala kusingekuwa na kitu kinaitwa uasi.

Tanzania ya sasa hakuna mwanajeshi wa kuasi maana wengi wameingizwa na wajomba, makaka nk kutokana na ukosefu wa ajira. Nadhani 10% ndio wameingia kwa wito, wengine wote ni wasaka mishahara. Siku nchi hii ikiingia vitani ndio utajua kwamba jeshi limejaza macheckbob ambao uwezo wao ni kupambana na raia wasio na silaha.
 
Kwa uono wangu MAGUFULI hatoachia urais 2025 maana hatokua tayari kubeba mzigo wa dhambi hizi akiwa bado na akili timamu.
Sijui kama bado kuna asiyeuona ukweli wazi huu. Huyu sio wa kuachia bila kufurukutwa na nguvu za wananchi. Ni wananchi pekee ndio walio na nguvu iliyobaki kumwondoa; vinginevyo vikelele hivi vya pembeni kwake havina maana yoyote.

Umeuliza hao wawili walioleta 'waraka' watatumia 'platform' ipi kuwafikia wananchi?
Wakiacha unafiki, zipo njia nyingi sana za kuwafikia wananchi. Hawa kazi yao ya 'ukatibu' ndio ilikuwa inashughulika na wananchi hao hao.
Hawa wanajulikana sehemu zote nchini na wana 'connections' za moja kwa moja na wananchi hadi huko kwenye vijiji. Hawa hawawezi kamwe kukosa njia za kuwafikia wananchi hao, hata ikiwa kwa njia zilizo wazi, kwani kuna shida gani.
Kuna mtu gani wa kumwonea aibu wakati heshima haitaki.
Hata wakiunga juhudi za vyama vya upinzani kwa njia mbalimbali. Humo humo ndani ya CCM yenyewe iliyooza kuna wengi sana wako tayari kuruka toka jahazi hili linaloizamisha Tanzania.

Waache unafiki. Hizi sio siku za staha tena.
 
Kesho nitanunua gazeti la Musiba la Tanzanite kwa mara ya kwanza. Musiba endelea kuwapiga jambajamba hawa wastaafu. Hata JK wewe piga tu. Sambaratisha mizee yote mpaka inyooke
 
View attachment 1154180
Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ana Makamu wake (Zanzibar)
Dk. Ali Moahammed Shein wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa
Baraza la ushauri la viongozi wastaafu wa CCM, walipokuwa wanazindua baraza hilo mjini Dodoma (24/08/2013)
Kushoto ni aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda na kulia ni aliyekuwa
katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.

NITASHANGAA SANA KAMA KINANA NA MAKAMBA WANATAKA HAWA WAZEE WAKAMJADILI MHUNI MMOJA ALIYEJIPA CHEO CHA UANAHARAKATI ANAYEITWA MUSIBA.

IT IS NEVER GOING TO HAPPEN, LABDA WAWE WAMETUMWA NA HAO WAZEE WAPATE SABABU YA KUMPIGA PINI JIWE.
Karudie tena kusoma waraka...
 
The same boiling water that hardens an egg softens a potato.
EeeHe Heee!!!

Enzi zile za kujibu maswali kwa kuandika 'insha', unapewa 'statement' kama hiyo.
Mtu unajikunja unatoa kurasa tano; tena zikiambatana na vielelezo (diagrams) ukiwa katika chumba cha mtihan wa masaa matatui!

Wacha aaaiiseeee!
Sijui ile elimu ilienda wapi!!!!
 
Hahaha, comments za uzi huu zinachekesha sana.

Baada ya kuweka mambo yake sawa kwingine kote, Sasa hivi Magufuli anaenda kumalizia na CCM na anaenda kupata ABSOLUTE POWER.

Miezi 6 hii ijayo tutaona mengi tuombe tu uzima. Kama Charles Dickens alivyowahi kuandika, these are the best of times and they are the worst of times!
 
Tanzania ya sasa hakuna mwanajeshi wa kuasi maana wengi wameingizwa na wajomba, makaka nk kutokana na ukosefu wa ajira. Nadhani 10% ndio wameingia kwa wito, wengine wote ni wasaka mishahara. Siku nchi hii ikiingia vitani ndio utajua kwamba jeshi limejaza macheckbob ambao uwezo wao ni kupambana na raia wasio na silaha.
you are wrong my friend.
Ukiachilia wapiganaji wa kiTz waliopo nchi zingine kama DRC n.k wakilinda amani' Kuna vijana wengi sana mipakani wanapigana na kulinda amani ya nchi na mipaka ya TZ. Ukiona nchi imetulia si kwamba hakuna wanaokufa wakiilinda pale kunapotokea tishio. Nchi ipo salama sababu ni ngumu kuingilika, kwa rasilimali tulizonazo tungekuwa dhaifu kama usemavyo tungetembelewa sana.
 
Hahahahahahaha

Hebu tupe mfano kumhusu huyo Baba wa Shangazi
Mkuu uwekwe kati na wazee usitoke!! basi ww utakuwa ni mlemavu. Ukishazeeka unaishi kwa hisani. Huna ubavu wa kumuweka mtu yoyote kati. Kibaya zaidi hao wazee hata wakiacha laana haimpati mtu maana hata wao ni wachafu. Hapo mtu anayeweza kuongea bila woga ni Karume tu, hao wengine wote wakiongea chochote wataishia jela.
 
you are wrong my friend.
Ukiachilia wapiganaji wa kiTz waliopo nchi zingine kama DRC n.k wakilinda amani' Kuna vijana wengi sana mipakani wanapigana na kulinda amani ya nchi na mipaka ya TZ. Ukiona nchi imetulia si kwamba hakuna wanaokufa wakiilinda pale kunapotokea tishio. Nchi ipo salama sababu ni ngumu kuingilika, kwa rasilimali tulizonazo tungekuwa dhaifu kama usemavyo tungetembelewa sana.

Mkuu acha upotoshaji, ukiondoa sehemu ambayo Tanzania imepakana na nchi zenye vita, hakuna mpaka/mahali wanajeshi wetu wana hatari ya kuuwawa au wameshauwawa kwa kulinda mipaka yetu. Kuna wanajeshi wamejiunga na jeshi baada ya vita vya Uganda mpaka wamestaafu hawajapigana vita zaidi ya kufanya mazoezi ya kijeshi. Raslimali zetu kwani watu wanahitaji kutumia vita kuzipata wakati wanakuja na kuingia mkataba na kuzipata tu?
 
Chama cha mapinduzi kuna nini?
Tusubiri muziki wa ala, baada ya mapumziko ya Chato.
Mbio hizo za marathon zinahitaji stamina sioni hilo kwa wazee wastaafu.
 
Back
Top Bottom