Baraza la Mitihani acheni kuua wawekezaji binafsi kwenye elimu kwa kisingizio cha udanganyifu katika mitihani

Nimekushauri kutembelea NECTa ili ukaelimishwe namna huo udanganyifu unavyofanyika, hutaki! Badala yake umechagua njia ya kulalamika! Huku ukiwa hujui chochote.
Anayelalamika ni kweli hajui chochote na kwa bahati mbaya anapata majibu ya hovyo kutoka kwa wanadhani wanajua kumbe hawataki kusumbua akili zao na kuhoji. Kwa ujumla mimi silalamiki nina hoji.
Kwa bahati mbaya sina shule binafsi lakini ningekuwa na shule binafsi halafu nifanyiwe ujinga kama huu - hayo maelezo baraza la mitihani wangeyaleta mahakamni
 
Wacha kelele kwenye mambo ya msingi! Baraza liweke hadharani nyaraka za serikali? Au wawaache wadanganyifu kwasababu ni wawekezaji? Hatutaki wawekezaji wezi! Kama huna akili unakuja kuwekeza wizi wa mitihani, hufai
Mbona hii taarifa ilitolewa na huu ni ushahidi kwenye eneo la tukio
Afande RPC, so.1 op-officer & RCO

Taarifa ya kufanya udanganyifu katika mtihani wa kidato cha nne tarehe 15/11/2021

Kamil:mkr/ir/1240/2021 (xx) ilani ya kwanza (xx) kosa: taarifa kufanya udanganyifu katika mtihani wa kitaifa kidato cha nne (xx) mnamo tarehe 15/11 /2021 saa 13:45hrs huko katika kijiji cha Mrere, kata ya Masahati, tarafa ya Mashati, Wilaya ya Rombo na mkoa wa Kilimanjaro (xx) mtoa taarifa afisa elimu sekondandari (w) Rombo Petronila d/o Paul aligundua kufanywa udanganyifu wa mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne katika kituo cha mtihani shule ya secondari Shauritanga kwa watahiniwa feki.

Elida Selesti Odele na Pendo Joseph wote ni wanafunzi wa kidato cha sita shule ya Sekondari Shauritanga, wakitaka kuwafanyia mtihani watahiniwa binafsi waliosailiwa kwa namba *p 0389-0007 Diana Domick Kimpere aliyetakiwa kufanyiwa mtihani na Elida Selisi Masawe, 20ys, mchaga, mwanafunzi kidato cha sita shauritanga sekondari na p 0389-0025 sharifa O. Ramadhani aliyetakiwa kufanyiwa na pendo joseph mashenene, 20yrs, msukuma, mwanafunzi kidato cha sita shauritanga sekondari.

Watahiniwa hao feki waliingia katika chumba cha mtihani saa 13:30hrs kwa ajili kufanya somo la Geography kwa maelekezo wanayodai kupewa na makamu mkuu wa shule mwalimu Joseph s/o Masasi maduka wakiwa na nakala za picha za utambulisho(photo entry) (xx) baada ya kukaguliwa picha za watahiniwa ndipo ilipobainika kuwa watahiniwa hao sio wenyewe kisha kukamatwa na kufikishwa kituo cha polisi mkuu Rombo kwa mahojiano (xx) makamu mkuu wa shule alitoroka kabla ya kukamtwa.

Mkuu wa shule aitwaye Ally Mgaya, 36yrs, mzigua mkazi wa mashati pia amekamtwa kuhusiana na tukio hili (xx) tukio limekaguliwa na sp. Geofrery g. Gulenga- OCD Rombo, akisaidiwa na timu ya makachero(xx) upel mbioni fcr/maendeleo vinafuata(xx)


Toka: Polisi (w) rombo.6
 
Sina neno na NECTA. Zaidi sana Mungu azidi kuwasaidia muendeleze uadilifu katika kazi zenu
 
Sina neno na NECTA. Zaidi sana Mungu azidi kuwasaidia muendeleze uadilifu katika kazi zenu
320365302_666058831823542_1910935165227789627_n.jpg
 
Umeandika maelezo mengi ila hakuna jipya ndani yake. Naomba unisaidie maelezo kama:-
1. Kuna ushahidi wa moja kwa moja uliokamatwa kwenye kituo wakati mitihani ikifanyika?
2. Kuna maelezo ya wahusika kwa maana ya i) wanafunzi waliokamatwa wakidanganya ii) wasimamizi waliogundua na kukamata wanafunnzi wakifanya udanganyifu iii) ushahidi uliokamatwa
Hii habari ya kuwa kuna sijui viashiria au sijui darasa zima majibu yanafanana ni ujinga mtupu ambao unaweza kutumia ama unatumika kwa nia ovu
Kwa kifupi ni kama umedata.

Kama wewe una ushahidi wa kituo chochote cha mtihani kilichifungiwa bila ushahidi usioacha shaka na kwa kuwa umekuja kulalamika hapa basi weka ushahidi wako wote hapa ili usaidiwe kupaza sauti.
 
Do you any evidence which you have submitted here to convince this audience? Or you just want people to believe your hearsay??
I did submit my evidence which is that the National examination council informed the public that it has withheld/ cancelled altogether the result of some primary school leaver 2022 on the ground of violation of examination regulation and that it has also revoked the examination centre licence for the respective school. The National examination council did not disclose these grounds upon which their decision is based. My plea is that the public ought to know these grounds.
 
Kwa kifupi ni kama umedata.

Kama wewe una ushahidi wa kituo chochote cha mtihani kilichifungiwa bila ushahidi usioacha shaka na kwa kuwa umekuja kulalamika hapa basi weka ushahidi wako wote hapa ili usaidiwe kupaza sauti.
Wala ninataka tu haki na uwazi
 
Back
Top Bottom