Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,810
- 11,977
Watahiniwa 95,955 wa kidato cha sita wanatarajiwa kuanza mitihani ya Taifa leo Mei 9, 2022 na wakitarajiwa kumaliza Mei 27, 2022 ambapo washiriki wanatoka katika shule za sekondari 841 na vituo vya kujitegemea 250.
Kuelekea kuanza kwa mitihani hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza za Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde ameonya juu ya vitendo vyovyote vya udanganyifu.
Amesema baraza halitosita kukifutia kituo chochote cha mitihani endapo litajiridhisha kuwa kinahatarisha usalama wa mitihani ya Taifa.
Dk Msonde alisema mitihani ya kidato cha sita ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwani hupima maarifa, stadi na umahiri wa wanafunzi katika yote waliyojifunza ndani ya miaka miwili.
"Baraza linatumia nafasi hii kuwataka wamiliki wa shule wote kutambua kuwa shule ni vituo maalumu vya mtihani hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani katika kipindi chote.
"Mtihani wa kidato cha sita ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwani upima maarifa, stadi na umahiri wa yale waliyojifunza katika kipindi cha miaka miwili ya elimu ya sekondari ya awamu ya juu," alisema.
Ameongeza kuwa watahiniwa 85,531 ni wa shule wakati 10,424 ni watahiniwa wa kujitegemea. Kati yao wanaume ni 47,859 sawa na 55.9% wakati wanawake apo 37,672 sawa na 44%.