Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), limesema wanafunzi 2,095 kati ya 2,180 waliofanya mtihani wa marudio wa darasa la saba uliofanyika kati ya Desemba 21 na 22 mwaka 2022 wamefaulu daraja A hadi C sawa na asilimia 96.1.

Limesema wanafunzi hao kati ya 2,194 waliofutiwa matokeo ya mtihani huo na Necta baada ya kubainika kufanya vitendo vya udanganyifu uliofanyika Oktoba 5, 6 mwaka 2022.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Amasi amesema kati ya wanafunzi 2,194 waliofutiwa matokeo waliofanya mtihani 2,180, wachache hawakushiriki mchakato huo kwa sababu mbalimbali, akisema huenda wengine walikwenda nje ya nchi.

Amasi ameeleza hayo leo Jumatano Januari 4, 2023 wakati akitangaza matokeo ya upimaji wa darasa la nne na mtihani wa kidato cha pili uliofanyika kati ya Oktoba na Novemba 2022.

"Watoto hawa walisababishiwa kufanya vitendo vya udanganyifu, siyo kwamba hawana uwezo. Uwezo wanao tena mzuri lakini kwa sababu wanazozijua wenyewe wanawapa majibu ya mtihani na kuwaharibu watoto hawa.

"Wanawaondolea hali ya kujiamini katika jamii kwamba bila kupewa majibu hawafaulu wakati wana uwezo na mtihani huu wa marudio walioufanya wamesimamiwa na Necta na wamefanya vizuri na ufaulu mzuri," amesema Amasi.

Amasi amewataka watu wanaowapa majibu wanafunzi kuacha tabia hiyo, akisema wanaharibu Taifa na elimu kwa malengo binafsi sambamba na kuwaondolea hali ya kujiamini wanafunzi hao.

"Tuwaache watoto wafanye mtihani wenyewe na tuwafundishe vizuri ili waweze kufaulu, kama ambavyo umeona wamefanya vizuri bila usaidizi," amesema Amasi.

Kwa mujibu wa Amasi, matokeo ya wanafunzi hao yatawasilishwa katika mamlaka husika kwa ajili ya uteuzi wa shule za sekondari ili kuunga na wenzao katika hatua hiyo.


Mwananchi
 
Baraza la mitihani la taifa hiki ni kituko cha karne- acheni kucheza na akili zetu.
Tuelezeni
  1. Je matokeo haya na yale ya mwanzo yapi yako juu ya mengine
  2. Kama mnathibitisha watoto wana uwezo mkubwa kwa kuona majibu yao kwanini walimu na wazazi wa watoto waliokaa na watoto hao mda wote wawe na mashaka na uwezo wao kiasi cha kuwaibia mitihani.
  3. nini mchango wa wasimamizi kwenye vituo
  4. kwanini msibebe tuhuma kuwa mna njama za kuumiza shule binafsi
 
Elimu yetu iko ICU, siku hizi ni kufurahishana tu.
Unafuta matokeo na kufunga vituo kwa mbwembwe; unawavuruga watoto kisaikolojia; unawapa mitihani nje ya vituo vyao chini ya usimamizi wa vitisho; halafu unakuja kutwambia kirahisi eti wamefaulu. jamani tuheshimiane kidogo basi mbona heshima ni kitu cha bure
 
Elimu yetu iko ICU, siku hizi ni kufurahishana tu.
Wangetakiwa kufaulu wote kabisa... tutoto twa miaka 13 afeli aende wapi jamani...

Mi nashauri serikali ifute mtiani wa la saba kabisa.. wawekeze kujenge shule nyingi za secondary...

Mtoto anafeli lasaba halafu anaenda wapi.. kama sio kwenda kujazwa mimba na kuwa kibaka akiwa mdogo?

Waende tu huko shuleni wakatekenyane huko ila sio kubaki mtaani
 
Back
Top Bottom