comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 8,171
- 5,905
Baraza la mitihani limekubuhu kwa tabia ya kufuta na kufungia shule kwa kisingizio cha udanganyifu katika mitihani. Hii inafanyika kwa namna ya kuonyesha kuwa udanganyifu huo unafanyika kwenye shule binafsi tu. Bahati mbaya hakuna uwazi wa namna wanavyofikia maamuzi yao.
Kwa kawaida udangayifu unatakiwa uonekane wakati mitihani inapokuwa inafanyika. Kama ni hivyo kweli basi malalamiko yasingekuwepo mengi na wahusika wangekuwa wanajua kabisa kuwa kwa ushahidi waliokamatwa nao watakuwa wanakabiliwa na adhabu ya kufutiwa matokeo au kituo.
Kwa namna inavyotokea na kwa kuhusisha shule za watu binafsi, tunahitaji maelezo kamili kutoka kwa baraza la mitihani ili tuelewe kinachotokea. Vinginevyo itaonekana kuwa ni njama za baraza kuua uwekezaji kwenye elimu kutoka kwa sekta binafsi.