Baraza la Mawaziri: Nani atoke, Nani abaki, Nani aingie?

waziri wote wa ccm hawafai

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...uye-nape-na-mzee-wa-tembo-wafunzwa-adabu.html

mleta mada namjua kwa ufundi wake wa kunong`oneza viumbe fulani fulani..hembu atuambie huo mvuto wa kinana upo wapi hapa.
20131207_154430.jpg

20131207_151107.jpg
 
Kwa maoni yangu tungeangalia kwanza ukibwa wa baraza lenyewe au la ni muhimu kuwe na mabadiliko kwenye baadhi ya maeneo. Mfano idara ya vijana ingerudi kazi na ajira, habari ingekwenda mawasiliano, sayansi na teknolojia, uwezeshaji ingekwenda viwanda. Vile vile ukiondoa wafuatao membe, lukuvi,tibaijuka,wasira,nchimbi,mbarawa, vuai, makamba na mwakyembe wengine wote wangepumzishwa.
 
Mchambuzi,

..CCM imeshindwa kwa miaka 36, unategemea mtaweza kwa miaka 2 iliyobaki.

..tangu CCM imeasisiwa, tumebadilisha maraisi, makamu wa raisi, mawaziri wakuu, mawaziri, etc lakini mambo ni yaleyale.

..ambacho hatujabadilisha hapo ni CHAMA,na hiyo ndiyo hoja ambayo tunapaswa kuijadili sasa hivi.

..tatizo la nchi hii ni CCM na mtu yeyote anayebaki huko ni kwamba ameamua kuwa sehemu ya tatizo.

..JK kaishabadilisha makamu wa raisi, waziri mkuu, na mawaziri hapo awali. why do u think this time tutapata ahueni kwa mabadiliko ya mawaziri??

NB:

..Lowassa ndiyo usimtaje kabisa. huyu ana tabia ya kufanya maamuzi ya kisiasa bila kuzingatia madhara yake kwa jamii. sekondari za kata ni moja ya maamuzi ya kisiasa ya Lowassa na athari zake will haunt this nation for a very long time.

cc Nguruvi3, Pasco, Jasusi,
 
Last edited by a moderator:
I'm sorry to say list yako inaviongozi wengi waliofikia menopause! hawana uwezo tena, ubunifu umefikia kikomo kwa wengi wao! kwakuwa hawana tena watu wa maana labda wangewajaribu vijana kama akina Makamba Jr, Deo et al...hata hivyo tatizo kubwa linalowakumba kwa sasa kuna vijana wengine walioko CCM wamechoka kuliko wazee wao! mf Mwigulu Nchemba, Nape, Juliana et al... Labda Rais ajaribu kuunda baraza dogo sana la Mawaziri; Ulinzi, Nje, Uendeshaji! wizara ya uendeshaji ichukue kila kitu na apewe Edo!
 
Topic hii ni nzuri sana na ingekuwa Rais wetu anaisoma huenda angepata pa kuanzia.
Hata hivyo hao wanaoitwa mawaziri mizigo wote wangeachwa na badala yake Profesa Mwandosya arudi katika Wizara ya Maji. Edward Lowasa apelekwe kwenye Elimu ili akaendeleze mikakati aliyoanzisha wakati akiwa PM.
Dk. Migiro apelekwe Mambo ya Nje na Membe aongoze Tamisemi. Hawa Ghasia atoke naye ni mzigo.
 
Kwa maoni yangu,,,Edo awe PM tu!Hii nchi itaamka ghafla
 
Wizara ya Kilimo iunganishwe na Mifugo ili kuondoa mgongano katika maamuzi. Mtu sahihi hapa ni Henry Shekifu. Wizara ya Ujenzi aendelee kubaki Magufuli. Nchimbi apelekwe kazi na ajira. Wizara ya Mambo ya Ndani anatakiwa mtu mwenye uwezo wa kuamua. Huyu ni Agrey Mwanri. Mama Kabaka aende Maendeleo ya Jamii. Sophia Simba naye ni mzigo atoke.
 
Tatizo ni watu au mfumo? Bila ya mabadiliko ya mfumo tutawaona mawaziri wote hawafai.

Mh. Ndungulile, unaweza kufafanua kidogo juu ya suala hili muhimu la 'mfumo", hasa kuliweka vyema katika muktadha wake? Mfumo wa chama tawala au mfumo wa utawala wa nchi?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
I'm sorry to say list yako inaviongozi wengi waliofikia menopause! hawana uwezo tena, ubunifu umefikia kikomo kwa wengi wao! kwakuwa hawana tena watu wa maana labda wangewajaribu vijana kama akina Makamba Jr, Deo et al...hata hivyo tatizo kubwa linalowakumba kwa sasa kuna vijana wengine walioko CCM wamechoka kuliko wazee wao! mf Mwigulu Nchemba, Nape, Juliana et al... Labda Rais ajaribu kuunda baraza dogo sana la Mawaziri; Ulinzi, Nje, Uendeshaji! wizara ya uendeshaji ichukue kila kitu na apewe Edo!

Pamoja na uzito wa hoja yako, binafsi sioni vijana waliotumia nafasi zao kuonyesha kwamba kweli wao ni mbadala wa wazee. Wengi wanaoanza kuaminiwa wanaonyesha kwamba wataendeleza legacy ile ile kuliko kuongoza nchi towards a renaissance of Tanzania.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wizara ya Kilimo iunganishwe na Mifugo ili kuondoa mgongano katika maamuzi. Mtu sahihi hapa ni Henry Shekifu. Wizara ya Ujenzi aendelee kubaki Magufuli. Nchimbi apelekwe kazi na ajira. Wizara ya Mambo ya Ndani anatakiwa mtu mwenye uwezo wa kuamua. Huyu ni Agrey Mwanri. Mama Kabaka aende Maendeleo ya Jamii. Sophia Simba naye ni mzigo atoke.

Ni bahati mbaya sana nimemsahau aggrey mwanri. Iwapo kuna uwezekano wa kumrusha mtu kutoka unaibu waziri hadi waziri mkuu, kama sio magufuli, basi ni mwanri ndie anayetosha. Sielewi kwanini mtu kama huyu anaachwa kwenye unaibu waziri huku wengi ya mawaziri kamili hawamfikii in terms of kiwango cha utendaji na maamuzi.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
I'm sorry to say list yako inaviongozi wengi waliofikia menopause! hawana uwezo tena, ubunifu umefikia kikomo kwa wengi wao! kwakuwa hawana tena watu wa maana labda wangewajaribu vijana kama akina Makamba Jr, Deo et al...hata hivyo tatizo kubwa linalowakumba kwa sasa kuna vijana wengine walioko CCM wamechoka kuliko wazee wao! mf Mwigulu Nchemba, Nape, Juliana et al... Labda Rais ajaribu kuunda baraza dogo sana la Mawaziri; Ulinzi, Nje, Uendeshaji! wizara ya uendeshaji ichukue kila kitu na apewe Edo!

umeongea vyema sana..pengine ni maccm waelewe kuwa CCM wangekuwa gari basi lilishazidi sana CPK limit..Yaani cost per kilometer zimemaliza ile lawa of diminishing returns.Faida imeenda ikipungua kw akila kilometr hadi ikafikia kuwa hasara .Sasa hasara inaongezeka.gari haliuziki tena zaidi ya kutakiwa kuwa disposed.Sasa bado wamechelewa na kufikia mahali pa kuweka garama hata ktk kudespose.

Tukianza waambia maccm magonjwa ya CCM hata wao wenyewe watachanganyikiwa.
 
Mh. Ndungulile, unaweza kufafanua kidogo juu ya suala hili muhimu la 'mfumo", hasa kuliweka vyema katika muktadha wake? Mfumo wa chama tawala au mfumo wa utawala wa nchi?
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Naongelea mfumo wa utendaji kazi Serikalini. Kwanza tunahitaji kuwa na malengo yanayopimika, pili tunahitaji rasilmali fedha na tatu rasilmali watu wenye uwezo wa kuelewa majukumu yao na kutekeleza kikamilifu. Mwisho, kusiwepo ukiritimba katika utekelezaji wa majukumu.
Swali la kujiuliza. Je mfumo wetu wa utendaji Serikalini una vigezo hivi vyote?
Ni kweli kuna baadhi ya mawaziri wenye uwezo mdogo na wapo wengine pamoja na changamoto zilizopo wameweza kufanya vizuri.
Mwisho kabisa, ni kuelewa vigezo vinavyotumika kupata mawaziri. Pamoja na uwezo vigezo vingine vinavyotumika ni pamoja na jinsia, uwakilishi wa mikoa, dini n.k.
 
Ni bahati mbaya sana nimemsahau aggrey mwanri. Iwapo kuna uwezekano wa kumrusha mtu kutoka unaibu waziri hadi waziri mkuu, kama sio magufuli, basi ni mwanri ndie anayetosha. Sielewi kwanini mtu kama huyu anaachwa kwenye unaibu waziri huku wengi ya mawaziri kamili hawamfikii in terms of kiwango cha utendaji na maamuzi.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mkuu umesahau ile slogan yao maarufu kuwa Rais hatakaa atoke Kaskazini? kuwapa watu wa Kaskazini nafasi ya juu ni hatari kwao hata kama atakuwa na faida kwa nchi!
 
ni kweli naunga mkono sababu wizara nyingi hazisaiidi na hazina. faida. na pia wizara zipunguzwe

Ukubwa wa baraza la mawaziri mara nyingi huwa ni kwa ajili ya ujenzi wa "patron - client relationships" kuliko kwa nia ya ujenzi wa taifa. Vile vile, public office imefanywa kuwa ni sehemu kubwa ya private life ya kiongozi, hivyo uteuzi huwa unalenga zaidi kumtoa mhusika na familia yake kimaisha kuliko kusimamia sera kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
hoja nzuri pumba nyingi, mwandosya????, tibaijuka???, sitta???? wote ni aibu hapo mtu ni magufuli, Mlawa my lecturer yuko fit lakini sidhani wizara ulmpa ni sahihi. TUNATAKA VIJANA KAA FILIKUNJOME, MBUGE A KISESA SHIMIYU,ESTER BULAYA ETC,
 
RockSpider, Nicholas,

Ni bahati mbaya sana kwamba mabandiko yangu #31 na #35 yameshindwa kuwaelewesha msingi na pia umuhimu wa hoja yangu, hivyo mmeshindwa kunielewa na kunijibu accordingly.
Cc Jasusi, Nguruvi3, JokaKuu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Ukubwa wa baraza la mawaziri mara nyingi huwa ni kwa ajili ya ujenzi wa "patron - client relationships" kuliko kwa nia ya ujenzi wa taifa. Vile vile, public office imefanywa kuwa ni sehemu kubwa ya private life ya kiongozi, hivyo uteuzi huwa unalenga zaidi kumtoa mhusika na familia yake kimaisha kuliko kusimamia sera kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Angalizo lako linaukweli mwingi na uhalisia katika kila neno uliloliandika! Kama tungekuwa serious kwa manufaa ya Taifa; Makatibu wakuu wa wizara wote wangekuwa wanapewa malengo kama CEO wa wizara na pindi wakishindwa kudeliver wangetimuliwa haraka iwezekanavyo! kuna baadhi ya wizara na vitengo vingefanywa kama agency za serikali na yangepewa malengo yaliyowazi yanayopimika, mwisho wa siku ingekuwa rahisi sana kujua kuwa mchango wa rasilimali moja moja kwenye pato la Taifa kwa uwazi na uhalisia ...
 
Back
Top Bottom