Madiwani walalamika uhaba wa Viti (Wanakaa Chini)

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Madiwani wa Halmashauri ya Tanganyika mkoani Katavi, wamelalamika kukosekana kwa meza na viti katika ukumbi wa mikutano na ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo na kupelekea madiwani hao kukaa chini wafikapo katika ofisi hiyo huku wakidai kushindwa kuandika kumbukumbu pindi wakiwa katika vikao vya baraza kwakukosa meza za kuandikia.

Madiwani hao wametoa kilio chao katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo ambapo wamesema walikubaliana suala hilo toka mwaka jana lakini mpaka sasa bado halijatekelezwa.

Akijibu malalamiko hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tanganyika, Shabani Juma amesema wameshatangaza tenda kwaajili ya kupata mzabuni wakutengeneza meza na viti katika ukumbi huo.

Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu amewataka madiwani kuendelea kuhamasisha na kuhakikisha watoto wote wanakwenda shule na kuingia darasani.

Source - Nipashe
 
Back
Top Bottom