Barabara za Mwendokasi zinadharaulika na wenye mamlaka wenyewe

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Matukio ya magari yasiyohusika kupita kwenye barabara ya mwendo wa haraka, yameibua hisia za kudharau utendaji wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) na Sheria ya Usalama Barabarani.

Uvunjifu wa sheria na taratibu zilizowekwa umeonekana kufanywa zaidi na magari ya vyombo vya usalama, magari ya wagonjwa, watu binafsi na maofisa wengine wa Serikali, kiasi cha baadhi ya nyakati kuzua mshikemshike na wasimamizi wa barabara hizo.

Juzi video fupi iliyosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, ilionesha askari polisi wakizozana na walinzi wa barabara ya mwendokasi, baada ya askari hao kulazimisha kupita njia hiyo.

Tayari Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, David Misime limetoa taarifa ya kukemea mazoea hayo na kutangaza hatua za kuchukua kwa wahusika.

Licha ya ukweli kwamba kifungu cha 54 (1), (2), (3), (4) na (5) cha Sheria ya Usalama Barabara kinatoa mwanya kwa magari ya dharura kukiuka kanuni za usalama barabarani kwa lengo la kuokoa maisha au mali, mwanya huo umekuwa ukitumika vibaya kiasi cha kuleta usumbufu barabarani.

Baadhi ya madereva wa magari ya wagonjwa wamelaumiwa pia kwa tabia ya kupiga ving’ora kutaka wapishwe njia kwa dharura lakini wakichunguzwa hukutwa hayana wagonjwa wala dharura ya kufuata mgonjwa na kusabisha usumbufu kwa waendesha magari wengine.

Baadhi ya watu waliozungumza licha kuunga mkono hatu hiyo ya Polisi, wamesema tatizo la matumizi mabaya ya vyombo vya dola ni kubwa kuliko linavyochukuliwa.

“Kwa kweli kuna wakati na sisi tunabaki kushangaa tu, unakuta lori la jeshi lina dereva mmoja linahama njia na kuingia upande mwingine wa barabara kukwepa foleni. Wakati mwingine utakuta mabasi yao yanarudisha staff nyumbani jioni lakini wanahamia upande wa pili wa barabara kukwepa foleni, hapa kuna dharura gani?” alihoji mkazi wa Kawe aliyeomba kutotajwa jina gazetini.

Akijibu swali la Mwananchi kwa simu ni hatua gani jeshi linachukua kudhibiti hali hiyo, Misime alisema dereva anaruhusiwa kupita njia hizo kwa dharura ya kuokoa maisha ya watu au vitu, na si vinginevyo.

“Kilichopo sasa hivi kila mtu kwa sababu tu ana gari la umma anaamua kupita barabara ya mwendo kasi au upande wa pili wa barara kukwepa foleni. Sheria lazima ifuatwe jinsi ilivyo,” alisema.

Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Kanali Gaudentius Ilonda, hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo, akisema ni suala la kipolisi na haitakuwa busara kwake kuingilia masuala ya kipolisi.

Jana, Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) ilitoa taarifa kwa umma kama muongozo kwa magari yanayoweza kutumia barabara hiyo.

“Magari ya Zimamoto, magari ya wagonjwa, magari ya kusafirisha fedha, majeshi ya ulinzi na usalama wanaweza kutumia barabara kwa kibali cha cha operesheni maalum kutoka Dart,” ilisema sehemu hiyo ya taarifa, huku wavunjifu wa sheria hata jana waliendelea kukamatwa. Katika maeneo mbalimbali hasa barabara ya Morogoro, maofisa wa Udart walionekana kusimamisha magari mbalimbali yaliyokuwa yakipita kwenye njia hizo.

Tofautina siku nyingine, jana maofisa hao walikuwa kwenye mshikemshike kudhibiti magari yanayopita kwenye barabara hizo. Msemaji wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi nchini (Taboa), Mustafa Mwalongo alisema hakuna haja ya kusitasita kama sheria imevunjwa basi waliohusika wakibainika wachukuliwe hatu a ili kutoa mfano kwa wengine.

Ofisa wa kitengo cha habari Dart, Elias Malima alisema wao wanaendelea na operesheni ya kukamata magari yanayopita kwenye barabara hizo.
 
Wanavyotumia nguvu kuzuia,utadhania gari tofauti zinazopita humo ni vifaru vya jeshi kwamba barabara itatoboka.kumbe ni gari muhimu,nyepesi,na chache kuliko gari husika za mwendokasi.

Nadhani wangejikita katika kuboresha huduma,maana kadri siku zinavyozidi kwenda mradi unazidi kudorola wateja.
 
ni kwa vile tu hujafanya utafiti, ili ukweli ni kwamba idadi ya magari yanayoingulia BRT ni mengi kuliko mabasi,
Na issue ya msingi ni safety, watu wanagongwa sana kwenye mwendokasi na ajali nyingi ni za magari ya kawaida, tukubali tu kuziachia hizi barabara za mwendokasi zitumike na mabasi pekee,
dharura zinaeleweka lakini hakuna dharura ys kila siku.
 
Kwa kawaida viongozi wetu huwa hawafuati sheria, wao kufanya kinyume cha utaratibu ndio sifa ya nafasi uliyonayo. Kwa maneno marahisi ni unanijua mimi ni nani?

Hata hivyo huo usafiri wa mwendo kasi unafanyika kwa uduni sana, kiasi kwamba wenye kiburi cha madaraka ni rahisi kutumia hiyo barabara yenye magari machache ya mwendo kasi.
 
ni kwa vile tu hujafanya utafiti, ili ukweli ni kwamba idadi ya magari yanayoingulia BRT ni mengi kuliko mabasi,
Na issue ya msingi ni safety, watu wanagongwa sana kwenye mwendokasi na ajali nyingi ni za magari ya kawaida, tukubali tu kuziachia hizi barabara za mwendokasi zitumike na mabasi pekee,
dharura zinaeleweka lakini hakuna dharura ys kila siku.
Uko sahihi kabisa. Jumamosi iliyopita usiku kama saa 4 kuna mtua alifika kinondoni B akawa anataka bodaboda ya kwenda posta. jamaa wakamwambia 4,000 na kwa bahati mbaya alikuwa ana 3,000 ambayo bodaboda walisema hailipi.

Ikabidi avuke barabara ili akapande tu mwendokasi, alivuka barabara ya kawaida vizuri tu ila wakati anavuka ya mwendokasi kuna gari lilitoka spidi likamgonga akatua umbali wa kama mita 7 hivi, palapale hakuongea kitu. Wakapigiwa simu ndugu zake waje wamchukue tu mpendwa wao.

Unajua hili tatizo linaonekana la kawaida ni kwa sababu vifo vingine havitangazwi.
 
eeh mkuu huo ndo ukweli,
hawa watu wanaosimamia hili waungwe mkono, hili ni jambo jema, uhai ni kitu chenye thamani kubwa sana.
 
Uko sahihi kabisa. Jumamosi iliyopita usiku kama saa 4 kuna mtua alifika kinondoni B akawa anataka bodaboda ya kwenda posta. jamaa wakamwambia 4,000 na kwa bahati mbaya alikuwa ana 3,000 ambayo bodaboda walisema hailipi.

Ikabidi avuke barabara ili akapande tu mwendokasi, alivuka barabara ya kawaida vizuri tu ila wakati anavuka ya mwendokasi kuna gari lilitoka spidi likamgonga akatua umbali wa kama mita 7 hivi, palapale hakuongea kitu. Wakapigiwa simu ndugu zake waje wamchukue tu mpendwa wao.

Unajua hili tatizo linaonekana la kawaida ni kwa sababu vifo vingine havitangazwi.
kwahiyo alikufa kwa sababu gari ya kawaida ilipita mwendokasi au kwa sababu hakuwa makini???
hata mwendokasi kuna zebra cross,na zinafuatwa na magari yote.
 
Watu kama wana haraka wajengewe Express way...unamwaga moto huku ukiwa umweka salio kabisa kuongeza pato la Nchi.
Wafikirie Miradi kama hiyo ndani ya majiji.

Mtu unamwagika ile mbaya.

Tuwaze nje ya Box...tena hizo ziwe za Underground kwa 80%.
Mwezi tu wanarudisha pesa yote.

Huku tunapenda sifa sana.
Mfano hizi foleni wakati tunakuja kuhesabiwa majumbani kwetu..kungekuwa na Express way ...Serikali ingeupiga mwingi sana kwenye kukusanya mapato.

Hakuna asiyetaka haraka hapa Duniani,kasoro kufa tu.

Naomba nikosolewe kitaalamu.😀😀😀
 
kwahiyo alikufa kwa sababu gari ya kawaida ilipita mwendokasi au kwa sababu hakuwa makini???
hata mwendokasi kuna zebra cross,na zinafuatwa na magari yote.

Mwendokasi Zipi zinazoheshimu zebra?

Labda zile Za Morocco Ila hao wengine ni uongo.
 
Back
Top Bottom