Barabara ya lami hadi Uru Kishumundu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barabara ya lami hadi Uru Kishumundu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kithuku, Sep 18, 2010.

 1. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Ni ahadi ya Kikwete! Ahadi nyingine inabidi watu watumie akili zao pia kabla hawajaziamini. Au JK kaona hao jamaa ndio rahisi kuwadanganya. Wachaga wenyewe wanabeza huko Kishumundu, JK anasema atapeleka barabara ya lami!
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,111
  Likes Received: 24,173
  Trophy Points: 280
  Na bandari atawajengea kama kawaida. kama hakuna bahari, atawaletea bahari then atajenga bandari. Kwa CCM hakuna kinachoshindikana.
   
 3. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Yaani mkuu wangu huu ni udanganyifu wa waziwazi, au ni kutaka kuzidi kuwabeza watu wa huko Kishumundu. Imagine miaka 5 itakapoisha wawe bado hawana barabara ya lami waliyoahidiwa huku wameshampa kura lukuki JK, unadhani wachaga wenzao (ambao tayari wanawabeza kama 'clowns') watawafanyaje kama si dharau zaidi? Yaani watakuwa ndiyo wa kutolewa mfano wa wadanganyika!
   
 4. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  Barabara zote vijijini mkoani Kilimanjaro kujengwa kwa kiwango cha lami - JK

  Huu ni moja ya mikoa migumu kwa ccm. Wananchi wanataka kazi ya ujenzi ianze kabla ya 31/10/2010.

  Vioja vingine tutavisikia akiwa mkoani Iringa juma lijalo.
   
 5. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Promises! promises! and promises!!!!!
   
 6. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Akiwa ni Moshi aliwaambia Mbeya na Muhimbili zitakuwa na 'Super Special Hospitals' na Mawenzi itakuwa Referral Hospital. Hiyo Super Special Hospital inatoa matibabu ya aina gani? na madaktari wake watasomea wapi? Au ndio kina Sheikh Yahya Hussein?
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  jk muongo. Hawezi kumaliza barabara zote za kilimankarro. Au amesahau kilimanjaro unajumlisha na jimbo la anne kilango amablo ndio maskini kuliko yotea kilimanjaro
   
 8. RR

  RR JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Hadi sasa kuna mkandarasi anaanza ujenzi wa Rau hadi Uru Mawela....kilomita 10!
   
 9. e

  emalau JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Jana ameahidi atalipa ng'ombe wa wamasai waliopotea!
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ahadu za sisi m huwa hazikumbukwi baada ya miaka 5.
  Jana nilisikia yule mwandishi wa the guardian akikumbusha kuwa 2005 Kikwete aliwaahidi watu wa Mwanza kuwa katika miaka 5 mji wa Mwanza utakuwa umejengwa na kuwa kama mji wa ulaya lakini hakuna kilichofanyika na leo anatoa ahadi Kigoma kuwa Dubai ndogo hahahahahahahahaha hivi na wachaga pamoja na kisomo chao chote wanadanganywa kirahisi na matapeli hawa? hahahahahahahahha
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Iivi huwa anafikiri kabla ya kutoa ahadi?
   
 12. V

  Vaticano Member

  #12
  Sep 18, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nani asiyejua sera zenu za majimbo?
   
 13. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  It is sad my friend. He promised to have that road tarmac in 2005. As 2010 approached, there was nothing like survey, clearing of third party interests abutting the road, and the CCM MP of the area Dr Chami started making noise meeting his members of constituency explaining that what was promised was murram all weather road, but he was shut down! Next that we heard was a Contractor had been assigned to the road and set up a camp site. Ni usanii.

  There are a number of issues here, how was the contractor picked, it seems like he was handpicked, two there are a number of structures tht will have to be removed to allow a free corridor for the road equipment, this takes time as the owners need to be treated fairly, given time to remove their houses and be compensated. Nothing like that! What CCM is going to do is going to push through and mistreated asset owners on either side of the road, and if they raise argument, they going to be branded traitors of a good cause, as usual they will cow down and life continous, Kikwete gets the vote!

  I wonder what the Chadema contestant in the area has to say on this!
   
 14. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #14
  Sep 18, 2010
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  i do believe on mr komu mb chadma na kunakoahidiwa barabara mawella ni jirani na kwao atawaambia mlalembeke nyira! wakipata kura hamtawaona kama ilivyokuwa 2005 dr chami aliahidi mengi lakini wapi? mashamba ya umma yamebinafsishwa(chibo,machare,uru estate)walichokiambulia wananchi ni cheap labour kwenye mashamba ya kahawa ambapo watu wanafanya kazi vile bila kuwa na vifaa vya kujikinga na madawa then magonjwa hela ya kujitibu hakuna umaskini tu!
   
 15. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  ha! ha! ha!

  Kwa mujibu wa Wachaga, ukiitwa "Wakishumundu" basi ujue wewe ni waluwalu wa kutupwa.

  Si ajabu hawajui hata lami ni kitu gani. Na JK anawamaliza hapo hapo kwenye Ukishumundu wao
   
 16. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Na wewe pia uache dharau zako. Una maanisha watu wa huko Kishumundu hawastahili barabara ya lami?
   
 17. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #17
  Sep 19, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  i have beeen in that area like 25 years ago..and still have friends coming from that area....lami ya uru kishumundi ilijengwa na mwalimu nyerere...miaka ya nyuma......ikaishia kilometa moja hivi kutoka hilo eneo...ambapo kuna kanisa...na ofisi za kata...so kwa kifupi kikwete hakutakiwa kusema anajenga barabara...bali labda kuikarabati....ile aliyojenga mwalimu zamani.........kama anavyokarabati barabara ya mandela ...badala ya kuachana na plan ya awali ya kuibomoa yote na kujenga mpya ya six lane .....kama plan ya awali ilivyokuwa!!!
   
 18. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #18
  Sep 19, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280

  ili kuvutia kura za wanafunzi ambao anajuwa ni wengi kutokana na idadi kubwa ya shule...JK amenikuna na ahadi yake ya kuunganisha shule nchini zote na in particular kilimanjaro na mtandao wa internet ndani ta miaka mitano iliyobaki...i cant wait to see that done ....wanafunzi na walimu wa msingi/sekondari kule kilimanjaro wataweza kuwasiliana na wenzao wa kigoma au mtwara........hayo yatakuwa mapinduzi ya ajabu...........
  naamini tayari shule zote nchini zina umeme angalau wa solar ...na infact walimu wote wa shule tayari wameshafundishwa kutumia hizo computer kabla ya wanafunzi......mpango kabambe huuu!!
   
 19. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #19
  Sep 19, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Kumbe ni kweli wakishumundu wanapenda sana kiingereza. Usishangae kusikia huyu ni shoe-shiner pale Samora avenue!
   
 20. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Mwenzio mmoja humu ndani kasema kumbe Kishumundu kuna barabara ya lami tangu enzi za Mwalimu Nyerere. Pengine basi JK alipaswa kuwaahidi jambo tofauti wakati huu, lakini nashangaa ahadi ndiyo hiyo na wameshangilia sana, na kura watampa. Anthony Komu aligombea ubunge huko Moshi uchaguzi uliopita, namfahamu tulikuwa naye Mlimani late 1980's, yeye alikuwa akituambia ni mtu wa Uru lakini siku zote alisisitiza kuwa si mkishumundu, sijui kuna shida gani huko? Labda nikuulize ndugu Mtu B, unaziamini ahadi za JK kuwa ataunganisha shule zote na internet? Shule hazina umeme wala computer, hiyo internet itafungwa wapi? Na ni kwa gharama za nani, maana hata hizi shule za kata tunazoambiwa ada ni sh 20,000 kwa mwaka kuna michango lukuki hadi ya kumlipa mgambo anayelinda kifusi cha kokoto kilichomwagwa uwanja wa shule!
   
Loading...