Mkuu Hujapatikana (Not Found), kijana anafanya kazi nzuri sana, na tena kwa 2015, atatufaa sana kule juu!, kama kigezo ndio hiyo barabara, ulipaswa kuipiga picha wakati alipoingia na kuipiga tena sasa!, unaona wazi kabisa, barabara hiyo imechongwa angalau sasa mabasi yanapita!, kabla ya hapo si nimlikuwa mnalazimika kugeuzwa mizigo kwa kupanda mikokoteni?!.
Barabara imechongwa na bahati mbaya Mungu kaleta mvua mapema kabla haijakomaa!, hii ni dalili nzuri ya uletaji maendeleo, inabidi yaletwe kidogo kodogo ili mummpe miak mitano mingine ya kumalizia hiyo barabara!.
Tukiamua kuwapima wagombea wetu kwa kigezo cha kutuleta maendeleo kwa kipimo wamefanya nini, hakuna mgombea yoyote wa kushindana na yule "jamaa yangu!", ila ili kuleta kipimo cha haki, inabidi tuletewe humu precedence ya Mwinyi alifanya nini kabla kustahili ofisi ile?!, Mkapa alifanya nini kabla kustahili ofisi ile?!, na Jakaya alifanya nini kabla kustahili ofisi ile?!, ndipo tulinganishe na huyu kijana amefanya nini kustahili ofisi ile!.
Nasisitiza kijana namfahamu, anafaa!.
Pasco