Barabara ya Bumbuli jimboni kwa January Makamba

Barabara ya Bumbuli jimboni kwa January Makamba

Kama wa Bumbuli mnaseme hivyo wa Lindi Kibiti road watasemaje.....?

Tatizo la barabara ni kubwa Nchini lakini Leo ni Vizuri Tupaangazie hapo kwa Bumbuli kwanza kabla ya kwenda kwingine .
 
Hii ndio mentality ya Mtanzania msaka tonge. Always settling for less. Always trying to defend the indefensible...kisa NJAA. Ubovu wa Mkapa si uimara wa January. Mapungufu ya Kikwete si umahiri wa January. Uzembe wa Lowassa si ubora wa January. Suala si waliotangulia WAMEBORONGA PIA bali MTARAJIWA AMEFANYA LIPI la kumfanya awe sahihi au tofauti na hao ulowataja.

Kwa mujibu wa mdau, kwa kuwa waliotutangulia waliboronga basi na sisi tuendelee kuboronga, thinking hii ni kituko cha mwaka.
 
Tanzania imepata uhuru lini?

Uhuru wa vitendo bado haijaupata? Upo Uhuru wa Bendera tu, kwani Bado Nchi inaendeshwa kwa kutegemea Misaada toka Nje, Barua za TRA,mahakamani, na Barua za kuomba kazi maofisini bado ni lazima ziandikwe kwa Kingereza, Kiswahili bado ni Lugha ya majaribio , Wazungu,wachina, na hata wahindi bado ni wakoloni kwa Staili ya Kijanja zaidi ( Ukoloni Digtal ) Nchi haina Uhuru kamili.
 
Navyojua mimi mpumbavu ni yule asie elewa sasa umeshaambiwa usimamizi wa barabara upo chini ya wizara ya ujenzi, zingine zipo chini ya ofisi ya waziri mkuu na serikari za mitaa unajuaje mipango na budget zao hizo sehemu na mikakati yao au unafikiri mmbunge anatakiwa ajenge kwa hela zake mwenyewe hizo barabara kama jamaa hawapo tayari mwerevu wewe?
Kama mbunge huwa anajua barabara si kazi yake iweje wakati wa Kampeni huwa wanawahidi wananchi barabara nzuri? ina Maana ahadi za mbunge wakati wa kampeni zilikuwa za Uongo?
 
Kwa hiyo wewe unataka hadi miaka mingapi ndio maendeleo kwa maana ya ubora wa barabara yaonekane? ndio maana CCM hata baada ya miaka 50 wanaona nchi bado changa kupata maendeleo yanayoonekana!

Ngoja ngoja huumiza matumbo, mambo ya kesho kesho, Mara mwezi Ujao,mwakani mara tuvute Subra, mchakato na lugha za kijanja janja Watu wamezichoka, Wanataka Maendeleo ya Haraka Mda story umekwishapita.
 
Kwa mujibu wa mdau, kwa kuwa waliotutangulia waliboronga basi na sisi tuendelee kuboronga, thinking hii ni kituko cha mwaka.

Nchi hii haiishi Vituko ,watu wanaishi kwa kukariri na ku-copy huku Visingizio vikiwa ni sehemu ya maisha ya Kawaida, yaani hata Mbunge akiharibu anatetewa kwa Vigezo vya mbunge wa awali ! inashangaza !
 
Nadhani ndio maana Makamba anataka agombee urais ili awasaidie wakazi wa Bumbli ama watanzania wengine. Kwa ubunge tu sio rahisi kuwaletea maendeleo katika kila Nyanja
 
Lakini pia utaonekana ni mpumbavu ukaenda kuuambia umma kuwa nataka niwe kiongozi wenu ili nihakikishe kila mmoja anamiliki nyumba ya ghorofa kumbe wewe mwenyewe unaishi kwenye tembe.

Mambo ya kusema Mkapa, Mwinyi au Kikwete wakati wanagombea, huko majimboni kwao bado kulikuwa na matatizo lukuki, ni fikra za kijinga na wakati huo umepita. Watanzania tusiwachague tena viongozi kwa vigezo vya porojo. Kwa wale ambao walikwishakuwa viongozi, kwanza watuthibitishie wame-deliver nini kwenye nafasi walizozitumikia kabla ya kufikiriwa kupewa madaraka makubwa. Hatuongelei kumaliza matatizo yote lakini watueleze walichofanikisha kiasi cha kufikiria wanaweza kupewa majukumu makubwa zaidi.

Lowasa ana vitu anaweza kuvitaja, alivyovifanya, vitu vikubwa. Je, vinatosha kufikiriwa kupewa madaraka makubwa zaidi, watu wanaweza kujadili. Dr. Slaa kuna mambo makubwa aliyoyafanya kwenye jimbo lake, je vinatosha au la watu watajadili. Lakini January Makamba, Membe, Pinda, Kigwangala, Sita - hawa wote ni zero. Hakuna chochote cha maana zaidi ya porojo.

Mkapa alitatua matatizo yote Masasi? Alikuwa mbunge miaka mingapi?

Kikwete alitatua matatizo yote ya Chalinze na Bagamoyo? Alikuwa mbunge miaka mingapi?

Lowassa amemaliza shida zote za Monduli? Amekuwa mbunge miaka mingapi?

Pinda, Membe wote wamemaliza umaskini majimboni kwao na barabara zote safi?

Mbowe amemaliza shida zote za Hai? Au Dr Slaa amemaliza kero zote za Karatu?
 
Kwa hiyo wewe unataka hadi miaka mingapi ndio maendeleo kwa maana ya ubora wa barabara yaonekane? ndio maana CCM hata baada ya miaka 50 wanaona nchi bado changa kupata maendeleo yanayoonekana!

Jamani hebu msomeni huyo bwana katikati ya mistari amejaribu kutoa mifano ya wilaya zee zaidi ya hiyo kama kielelezo cha utendaji wa serekali yetu sikivu. Au sio nngu007.
 
Last edited by a moderator:
Hatuoongelei kumaliza matatizo ya sekta zote. Lakini angalao tunataka kujua ni mambo gani makubwa ambayo January amefanikisha katika jimbo lake kiasi cha kuonekana anastahili kupewa nafasi kubwa zaidi?

Kukosa kujiuliza swali hili mwaka 2005, sasa hivi kunaligharimu Taifa. Kikwete alikuwa kiongozi katika nafasi nyingi kwa kipindi kirefu, na hakuna mahali popote alipoweza kufanya kitu cha pekee. Tulimchagua kuwa kiongozi wa nchi kwa kusikiliza porojo za mdomoni. Leo tunashuhudia utendaji duni wa Kikwete kwenye ngazi ya Taifa. Amefikia mahali kuwaaminisha Watanzania kuwa tunaweza kupata maendeleo kwa kusaidiwa saidiwa tu. Hotuba zake zote za kuonesha mafanikio yake zimekuwa za kuelezea amepewa nini toka kwa nchi gani - huo siyo uongozi. Uongozi ni kuwaonesha watu njia ya namna ya kujiletea maendeleo yao wao wenyewe, msaada iwe ni nguvu ya kuongezea kwenye jitihada za ndani lakini Kikwete imeigeuza nchi miguu juu kichwa chini, sasa kila mmoja anaamini tutapata maendeleo kwa kuhesabu tumepata nini toka nchi gani. Na yeye Rais amekuwa mtu wa kuzunguka Dunia nzima, akitangatanga kuomba. Big shame!

Hatuhitaji tena Rais atakayekuwa na fikra za kijinga za kudhani tutalijenga Taifa kwa kusaidiwa tu. Fikra za kuombaomba zimefifisha hata uwezo wa ndani wa ubunifu. Kila tatizo sasa hivi, kila kiongozi akiulizwa, jibu utasikia ------ mhisani amepatikana, lakini hajatoa hela.

Tunataka kuondokana na mawazo ya kipumbavu kuwa tutajenga nchi kwa kuomba.

Nadhani ndio maana Makamba anataka agombee urais ili awasaidie wakazi wa Bumbli ama watanzania wengine. Kwa ubunge tu sio rahisi kuwaletea maendeleo katika kila Nyanja
 
Very poor thinking. Unaposema jimbo lile lina umri chini ya miaka 25 unamaanisha nini? Unataka kutuambia hakukuwa na watu pale tokea uhuru? Kabla ya hapo hawakuwahi kuwa katika jimbo lolote lile? Nadhani tunajadiliana na watu wa ajabu kabisa?

Unataka kusema tukienda Katavi tukakuta hakuna shule, hakuna hospitali, hakuna barabara, ni sahihi kwa sababu ule mkoa umeanza mwakajuzi? Kwani kabla ya hapo hao wananchi na maeneo yao hayakuwahi kuwa na mkoa, na hivyo kustahili kuwa na haki hizo?

Tatizo lenu ni hilo la kutaka kumtia makosa Makamba kana kwamba lile jimbo lina miaka 25.
Kwann hukueka zuri alilofanya kuhusu barabara then ndio umkosoe ?
 
Aisee ndio maana huwa anapitwa bila kupingwa kumbe ndio pako hivyo kha!
 
Yaani hili ni JIMBO JIPYA halina hata MIAKA 15; Lilianzishwa na Mzee Shelukindo; Sasa unataka liwe na kila kitu sababu tu MAKAMBA ni MBUNGE?

What a JOKE... inaonyesha ni baadhi ya sisi wananchi ndio tumechoka hatujui Maendeleo ni nini



c.c NOT FOUND

Nakubaliana na wewe kabisamiaka 15 ni michache sana, kama chama chake kimeshindwa kuleta maisha bora kwa watanzania kwa zaidi ya miaka 50 yeye ataweza wapi?
 
Ni lazima Bumbuli paangaziwe zaidi maana mbunge wa hapo ameutangazia umma kuwa yeye ana uwezo mkubwa zaidi wa kuongoza kuliko wabunge wengine, ndiyo maana sasa anataka apewe mamlaka ya kuongoza nchi nzima. Ni sahihi kabisa kuchunguza kwa umakini sana hapo alipokuwa akiongoza kuna nini zaidi ya majimbo mengine. Maana anasema anataka kutumia rasilimali za Taifa kuibadilisha Tanzania, sasa atueleze ameibadilisha vipi Bumbuli kwa kutumia rasilimali za Bumbuli.

Tatizo la barabara ni kubwa Nchini lakini Leo ni Vizuri Tupaangazie hapo kwa Bumbuli kwanza kabla ya kwenda kwingine .
 
Jamani hebu msomeni huyo bwana katikati ya mistari amejaribu kutoa mifano ya wilaya zee zaidi ya hiyo kama kielelezo cha utendaji wa serekali yetu sikivu. Au sio nngu007.
mkuu jamaa alimaanisha jimbo lilianzishwa na Shelukindo miaka 15 iliyopita, hakutaja habari ya kuwa halmashauri, Janauary ndo alianza na ikawa halmashauri miaka 4 iliyopita,
 
Kwa hiyo wewe unataka hadi miaka mingapi ndio maendeleo kwa maana ya ubora wa barabara yaonekane? ndio maana CCM hata baada ya miaka 50 wanaona nchi bado changa kupata maendeleo yanayoonekana!

Na kwa asilimia 99 hii ndo akili ya watawala wetu wa CCM. Akili mbovu sana na uelewa duni wa kupambanua majira na nyakati. Mkuu Utotole wanaotuangusha ni watu wachache sana lakini yana mwisho.
 
Last edited by a moderator:
Issue sio January Makamba issue hapo ni CCM!!! hiyo ndio Taswira katika taifa chini ya utawala wa majizi CCM, kuna barabara zingine ni balaa zaidi ya hapo
 
Hizi thread zingine mnazianzisha ilimradi muweze kujifirahisha na kurusha mawe. Mtu yoyote mwenye uelewa kidogo zaidi ya punje ya mchele anajua kazi kubwa iliyofanyika Bumbuli ndani ya miaka 4 iliyopita.

Yaani, kwa mtazamo wangu kitendo cha thread zinazohusu maendeleo ya Bumbuli kuongelewa sana, inaonyesha tu January amefanikiwa kuiweka Bumbuli kwenye ramani. Maana watu hawajadili Monduli, Karatu, Hai, Arusha mjini, Mtama, Mpanda, nk. Big up JM.
 
Yaani hili ni JIMBO JIPYA halina hata MIAKA 15; Lilianzishwa na Mzee Shelukindo; Sasa unataka liwe na kila kitu sababu tu MAKAMBA ni MBUNGE?

What a JOKE... inaonyesha ni baadhi ya sisi wananchi ndio tumechoka hatujui Maendeleo ni nini



c.c NOT FOUND

kiongozi ni wewe kweli ?
 
Back
Top Bottom