Barabara nyingi Dar es Salaam zimejaa mashimo, hivi wahusika hamlioni hili?

Barabara nyingi zilijengwa hapo nyuma lakini zilijengwa chini ya kiwango zikaishia kubomoka...
 
Chalamila ni mtu wa hovyo kuwahi kushika public office.

Huwa anazungumza mambo ya kijinga kijinga tu ili kuchekesha.

Ukuu wa Mkoa.sio Commedy ile ni dhamana.

Akitaka watu wacheke akajiunge na kina joti.
Chalamila ni sawa na mdogo wake tu Makonda, wote ni majanga tupu
 
Unapoingia jijini Dar es Salaam kupitia Barabara ya Morogoro, utapokewa na barabara za kuvutia zenye madaraja ya juu yanayopita magari na ya waendao kwa miguu, hakika utaona sura ya jiji inayopendeza.

Lakini unapoanza kuingia mitaani, utachoshwa na barabara mbovu na kwa kipindi hiki cha mvua, nyingi zimejaa maji katika mahandaki na kutengeneza madimbwi, huku nyingine zikishindwa kupitika kabisa.

Hali kwa sasa inatisha.

Yaani ukiachana na barabara ya kuanzia Kimara Mwisho mpaka Kibaha Maili Moja.

Nyingine zote hatua kumi tu unakwepa handaki.

Ni aibu tupu kwa nchi ambayo watu Mia nane wanakwenda kuhudhuria kongamano moja tu lakini wanaacha barabara za mji mkuu wa kibiashara hazipitiki.

Sijui kwakweli wahusika mnampango gani maana hali ya barabara za Dar es Salaam ni ya kusikitisha mno.

Njoo tu hapa Kanisa la St. Albans karibia na Holiday Inn pale kuna mashimo ya kutosha na ni city centre kabisa.

Ali Hassan Mwinyi Road mashimo, Samora mashimo kila mahali jiji zima ni mahandaki tu mnayakwepa.

Fanyeni jambo.

Yaani inakera na inatia hasira sana kuona mji kama huu una barabara za ovyo namna hii
 
Back
Top Bottom