Barabara nne Chalinze - Segera hadi Tanga

Juzi usiku nimeona kwenye kituo kimoja cha TV serikali yetu ikitangaza mpango wa kujenga barabara nyingine ya kiwango cha lami itakayokuwa sambamba na ile iliyopo kutoka Segera hadi Tanga, hivyo basi moja itakuwa ina kwenda nyingine inarudi (double roads).

Serikali imesema inafanya hivyo kuepusha ajali nyingi zinazotokea katika barabara hiyo, na mradi huo utaanza hivi karibuni , utafanywa kwa awamu na utagharimu Tshs bilioni nne.

1.Jamani hizo hela kwanini zisiende kujenga barabara huko madongo kwinama ambako hakuna barabara za lami na hizo za vumbi zinahali mbaya kabisa?

2.Eti wanazuia ajali watu wasife!, mbona huko madongo kwinama watu wanakufa kwa kukosa usafiri wa kuwapeleka mahosipitliani kwa sababu barabara hazipitiki! nani atwasemea wananchi hao wanaoishi kama wakimbizi ktk ncnhi yao?

3. Mbona mazao ya wakulima yanaozea mashambani kwakukosa usafiri kutokana na ubovu wa barabara, hili serikali haliihusu?

4. Yaani wanataka kutuambia hiyo barabara ndiyo chanzo kikuu cha vifo vya watanzania kikiasi kwamba ndiyo inastahili kutengewa fungu hilo kubwa wakati kiukweli haihitaji hilo fungu!?

5 Au kwakuwa pia ni njia ya kwenda kwa Mkulu wa kaya!

Jamani mimi naona nchi yetu ni kweli inahitaji miundo mbinu, lakini ni kwenye maeneo yanayo stahili, hii ikoje? ahh......... nchi yetu "inanajisiwa"! na watu wajinga kabisa ambao ni viongozi wetu.
Bilioni nne???!!! Andika vizuri!. Bilioni zinajenga sio zaidi ya kilomita nne.
 
Back
Top Bottom