Bao la kisigino

Bao la kisigino

We nawe ni Mbulula tu,Fisadi wako kaenda kujipendekeza kwa wakubwa wake samaki ana nguvu akiwa majini lakini ukimtoa hana ujanja,nguvu ya Lowasa ilikua ndani ya CCM kwa sasa yupo kwenye foleni tu ya akina Mrema
Mbona hajatumbuliwa kanisani??????????????????? Nani mwenye kushika mpini na nani kashika pakukatia????????
 
Kwakweli bado
Lowasa hajawi na hatokuwa mpinzani, amelelewa na ccm, kwa mfumo huohuo,
Alikuja chadema ili apate urais, hakuwa na mapenzi na upinzani, Sasa kilichomleta kime expire, ndo maana anaanza safari ya kurudi kwao ccm, kwa watu walewale ombapo ana maslahi
 
Kama kweli CCM ina ubavu, imuite LOWASSA kwenye hii mahakama mfu ya ufisadi ambayo kila kukicha wanashadidia.

Nakuhakikishia hakuna jiwe litasalia juu ya jingine, utashangaa Raisi amejishika mwenyewe
wew jamaa tangu asubuhi nilikuwa sjacheka
 
ni mwendelezo wa kaulimbiu ulipo tupo komaa nae tu mwenyekiti wenu mpaka sasa yuko kimya ile gia aliobadilishia angani uku hana Mafuta ya kutosha inaanza kumcost
 
Nini lengo hasa la mleta mada? Kwahiyo watu wakifanya mazuri na mema yenye kuwapendeza watu wasipewe sifa kwa kuwa na tofauti za kiitikadi za siasa? Nafikiri ule ujumbe kwa wananchi na wafuasi wa Lowaassa na Magufli kuwa tunatakiwa kuishi kwa amani na salama na sio kwa vijembe na majungu.Tumekuwa tukigombana sisi kwa sisi huku chini ngazi ya wananchi na vitongoji ila wenyewe tunaowapigania wamekuwa wakituonesha mifano mizuri na hai lakini tumekuwa wagumu kuyaelewa wanayotokea.
Lowassa anaipenda Tanzania kwa dhati kwa mfano wake.
Kule zanzibar watu hawasalimiani yaani CUF na CCM kwa kuwa hta viongozi wao wameridhihirsha hili kwa wanachi wao.Kma kiongozi wetu mpendwa Lowassa ameonesha uungwana wa hali ya juu vile basi sisi huku tunapaswa hata kukumbatia kwa upenda bila kujali nani yuko chama gani.
Lowassa huyu hatojirudia katika medali za siasa endapo atatangaza kustaafu.
HONGERA MH.WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD NGOYAI LOWASSA umepata bahati kupendwa na CCM na CHADEMA.
 
ni mwendelezo wa kaulimbiu ulipo tupo komaa nae tu mwenyekiti wenu mpaka sasa yuko kimya ile gia aliobadilishia angani uku hana Mafuta ya kutosha inaanza kumcost
Unajua kuna tofauti kubwa kati ya kuongea na kumaanisha! Wewe unaongea lakini humaanishi kile unachoongea na hata ukiambiwa kitolee tafsiri nina hakika utashindwa
 
View attachment 389673

Ni aina ya bao kwenye soka ambalo hakuna anayetegea kama litafungwa, huja kiaina yake kimtindo na bila kipa kujiandaa au wale walinzi. Mpira hutikisa nyavu na hadhira kulipuka kwa shangwe na kelele za goooooo....!!!!

Hiki ndio kilichotokea wiki iliyopita Pale EL alipokutana uso kwa uso na Magufuli. Wengi hawakutarajia kile alichokifanya Lowassa, kwa tabasamu toka rohoni alimsabahi Magufuli bila chembe ya kinyongo! Katu Magufuli hakulitegemea hili na yeye bila kuficha hisia zake za ndani kabisa akakiita kitendo kile kama ni muujiza.

Ilikuwa ni 'brief moment' iliyoleta impact kubwa sana kisiasa hasa kwa upande wa Lowassa! Kwa kasi ya ajabu ikawa ni mjadala kila mahali lakini kote huko kete ikimwangukia Lowassa. Hamasa ya kumpongeza EL kwa kuonyesha uuungwana mkubwa kiasi kile umeikumba CCM hata kufikia nacho kutoa tamko rasmi la kumpongeza.

Kisiasa hili ni bao la kisigino na si la mkono

Ukomavu wa kisisa, adui au rafiki wa kisiasa si wa kudumu!
 
Ninaungana na JK kwamba EL ni mwanasiasa halisi. Wengi tusingeweza kuwa na roho hiyo hasa baada ya mambo yalitotokea kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Yote mzee kasamehe mara saba.
 
We nawe ni Mbulula tu,Fisadi wako kaenda kujipendekeza kwa wakubwa wake samaki ana nguvu akiwa majini lakini ukimtoa hana ujanja,nguvu ya Lowasa ilikua ndani ya CCM kwa sasa yupo kwenye foleni tu ya akina Mrema
U͢s͢i͢p͢a͢n͢i͢k͢ m͢c͢h͢e͢z͢o͢ h͢u͢u͢ h͢a͢u͢i͢t͢a͢j͢i͢ h͢a͢s͢i͢ra͢!
 
Kumbe ni msafi tayari! Sasa ile mahakamani si mliwaaminsha watu wenu kwamba inafunguliwa kwa ajili yake. Itakuwaje sasa?
Hahaha....mabosi wenu walizunguka nchi nzima kwa zaidi ya miaka 8 wakisema Lowasa Fisadi,baada ya kumtukana na kuiponda CCM kwa muda wote huo iliamua kumtosa kwenu....sasa hivi joka liko ndani ya chama chenu....wote kimyaaa...mmeufyata mkia,mmebaki kusifia na kusafisha tu.Anyway,babu yenu hatauona urais tena ataishia kukaribishwa kwenye party za mabosi wake na kujipendekeza pendekeza tu kwa wakubwa.
 
mabosi wenu ... kukaribishwa kwenye party za mabosi wake na kujipendekeza pendekeza tu kwa wakubwa.
Fikra za kitwana hizi. watu wanaochaguliwa kwa kupigiwa kura hawawi mabosi wa wale wanaowachagua!! Yaani unadhani muuza nyanya wa Soko Matola mbeya "mkubwa" wake ni hawa wapigiwa saluti? Au hujui ni kwa nini wanaitwa watumishi wa umma?
 
Hekima ni kipawa...! Si kila mmoja wetu anaweza kubarikiwa hicho kipawa
Hivi ujinga nao hauwezi kuwa kipawa? Maana kama mtu unaita waandishi wa habari na kumtangaza mtu kuwa ni muungwana halafu hutaki kuiga uungwana wake huo si ni "ujinga"?
Namzungumzia Sendeka, jee sio kuwa atakuwa na hicho kipawa?
 
Tukiacha unafiki kuna kitu cha kujifunza hapa kama binadamu na hasa tukiwa ni watanzania, kwa pande zote mbili, kwa mh Rais na kwa upande wa EL . Kukubali na kutambua maamuzi ya wengi, lakini pia si kila nafasi unayoipta kusimama kugongea unaitumia kumtukana na kumshambulia mtu, kwa ajili ya ku m furaha asha mtu au kikundi cha watu walioko nyuma au mbele yako.
 
Back
Top Bottom