Mkuu
Kalamu1 , nia ya kununua madeni ni kutengeneza profit, na kwa madai yao, pesa hizo walisema zitatumika kwenye miradi mbali mbali waliyoiorodhesha! Mfano mashamba na makampuni. Hata Rostam Aziz alifunguwa kampuni ya kilimo iliyoitwa Kagoda.
Pesa hizo zilikuwa zimetengwa kwa akili ya kulipa madeni ya nje kama sikosei! Kwahiyo hayo makampuni na hao watu walichota hizo pesa kwa kigezo cha kununua madeni!
Ni kamba tu na utapeli wa kuzichota pesa za walipa kodi(ambapo kuna wakati eti walithubutu kusema pesa za EPA si za wananchi)
Mkuu ni bora hata wangewekeza kwa wananchi basi. Sasa bank M hizo pesa waliziweka humo zilipotolewa. Hata ule utaratibu wa Jk wa kusema zirudishwe sijui utaratibu wake umefikia wapi.