Bank M-Connecting the dots...

Bank M-Connecting the dots...

Prove it by any first century writer/historian
To you what is the most ancient chronology event between the ancient Egypt (Egyptology) and Jesus's stuff?

Do you even know why your calendar reads like the way it looks today? Do you think the whole world is scammed?

To me this is quite a low argument and deserves no consideration from me because of it's discourse and strength but also this is not an appropriate forum for it.

Note, go read the red sea scrolls at least for beginning.
 
Mods please musiiunge hii for now kwasababu msingi wa threads nyingine ni maswali kuhusu chanzo cha Bank M. Na nyingine kuhusu kukamatwa kwa mkuu wake kwa kosa la utakatishaji! Ripoti hii hapo chini, inaonyesha chanzo cha benki hiyo ambayo kama wengi mtakumbuka, ilitumika kuzituliza zile pesa za EPA! Na ilikuwa ya vigogo! Je kukamatwa kwa mkuu wake Sanjeev Kumar, ni kufukua makaburi? Nini maoni yako? Maana ukweli ni kwamba pesa ya EPA ilikuwa ya uchaguzi kuisaidia ccm. Na Sasa hivi ni wazi Maghufuli ana hali mbaya ndani ya chama haswa kuhusiana na pamoja na mengine, pesa za kampeni!

Wanajamvi, Let’s connect the dots...

...kuna gazeti liliandika ripoti enzi hizo...

Enzi za uhuru kwa kiasi fulani wa vyombo vya habari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwana Sanjeev Kumar mwezi January 2019 alihamisha mali kiasi cha dola milioni 500 ambazo tangu August mwaka jana zilikuwapo ndani ya benki ya M.

Alihamishia kwenye benki ya Azania jambo ambalo lilionekana wazi kwamba alikuwa akijaribu kukwepa kitu fulani na ndipo BOT walipoamua kufuatilia.

Benki ya M ilikuwa na tatizo la liquidity ambapo unakuwa unataka kubadilisha kwa haraka amana au mali bila kuathiri thamani ya mali au amana hizo.

Ukiwa unafanya hivyo huku taa zote za ishara ya hatari zipo standby kutoka BOT, basi unakamatwa kwa kutaka kutorosha fedha au kutakatisha.

Pia tukumbuke kwamba siku chache zilizopita BOT wamezifungia benki 5 (ikiwemo Azania) kwa kukiuka masharti ya kubadilisha fedha ambapo benki hizo zimeshindwa kutoa taarifa ya kubadilisha au kuhamisha kwenye mfumo wa interbank foreign exchange market.

Hivyo hapo sioni sababu ya kuihusisha hii na raisi Magufuli na CCM kukosa fedha za kampeni badala ya kuona kwamba hizi ni jitihada za BOT kudhibiti soko la ubadilishaji fedha za kigeni baina ya vyombo vya fedha kwenye mfumo wa fedha wa nchi.
 
Wahindi wa Tanzania wametuangusha. Katika kashfa karibu zote kubwa wanahusika.
Ndio mambo ya kukutana kwa vikao vyao vya siri na kugawana hizo fursa? Maana walatini wanasema Quid Pro Quo....
Hii historia ibadilike sasa. Enough. Criminals wawajibishwe
Quid quo pro, that’s it!👍🏽
 
Bwana Sanjeev Kumar mwezi January 2019 alihamisha mali kiasi cha dola milioni 500 ambazo tangu August mwaka jana zilikuwapo ndani ya benki ya M.

Alihamishia kwenye benki ya Azania jambo ambalo lilionekana wazi kwamba alikuwa akijaribu kukwepa kitu fulani na ndipo BOT walipoamua kufuatilia.

Benki ya M ilikuwa na tatizo la liquidity ambapo unakuwa unataka kubadilisha kwa haraka amana au mali bila kuathiri thamani ya mali au amana hizo.

Ukiwa unafanya hivyo huku taa zote za ishara ya hatari zipo standby kutoka BOT, basi unakamatwa kwa kutaka kutorosha fedha au kutakatisha.

Pia tukumbuke kwamba siku chache zilizopita BOT wamezifungia benki 5 (ikiwemo Azania) kwa kukiuka masharti ya kubadilisha fedha ambapo benki hizo zimeshindwa kutoa taarifa ya kubadilisha au kuhamisha kwenye mfumo wa interbank foreign exchange market.

Hivyo hapo sioni sababu ya kuihusidha hii na raisi Magufuli na CCM kukosa fedha za kampeni badala ya kuona kwamba hizi ni jitihada za BOT kudhibiti soko la ubadilishaji fedha za kigeni baina ya vyombo vya fedha kwenye mfumo wa fedha wa nchi.
Hahaha! Dah! Mbona umechaguwa jibu jepesi hivyo kwenye swali gumu?
 
Hayo makampuni hewa yalikuwa yanafanya kazi ya utapeli at the next level.
Kina Msofe wanadhulumu wajane viwanja, wengine wanapiga kimya kimya bado wanavaa suti na tai, na kusifiwa ni wawekezaji
Waache sasa utapeli maana nao wanatapeliwa
Halafu jamaa anaitwa Richard yeye anasema ni jambo dogo tu linahusiana na “kushuka na kupanda” kwa dola!😀
 
Mimi nmetaja tu eneo moja la kuhamisha fedha kijanja.

Ila Benki M ni sawa tu na Meridian Biao Bank ilivyokuwaja kwa kasi miaka ya 90.
Meridian Biao Bank ilianzishwa kifisadi vile vile?


Hivi unadhani hizo usd 500m alizotaka kuondoa wameanza leo? Halafu hapa mjadala ni zaidi ya hiyo tiny weeny idea!

Hata hujasema lolote kuhusu chanzo cha bank M, ufisadi wake pamoja na jinsi ambavyo serikali imekuwa ikiilinda benki hiyo na kuendelea kulisababishia Taifa hasara?

Usisahau style ya mjadala hapa JF wewe ni mkongwe toka hili jamvi linaanzishwa mwaka 2006 ukituambia kuwa upo Uingereza. Enzi zile tunawapinga mlipokuwa mnafungua matawi ya ccm huko. Nadhani utakuwa unakumbuka!
 
Mkuu Kalamu1 , utaratibu wa kununuwa madeni upo. Ebu kwa kuanzia, tizama hii tafsiri rahisi kutoka Investopedia...

DEFINITION of Debt Buyer. A debt buyer is a company that purchases debt from creditors at a discount. Debt buyers, such as a collection agencies or a private debt collection law firm, buys delinquent or charged-off debt at a fraction of the debt's face value.Jan 23, 2018

Debt buyers make money by acquiring debts cheaply, and then trying to collect from the debtors. Even if the debt buyercollects only a fraction of the amount owed on a debt it buys—say, two or three times what it paid for the debt—it still makes a significant profit.

Perfect.

Kwa hiyo Chavda wetu alinunua deni kwa 2.5 millioni, jamaa akaenda kuvuna mabilioni toka kwa mdaiwa ambaye ni serikali yetu!

Nimekupata barabara na kila kitu sasa kimefunguka vyema.
Haya tuendelee!
 
kuna kitu nakuomba usikisahau, brains behind all this plunder ni Watanzania wenzetu. Majina ya Watanzania hao huwezi kuyakuta katika orodha ama ya wamiliki au ya wenye hisa lakini ni wanufaika wakubwa katika biashara hizi kupitia kivuli cha CCM.

Ahsante Mag3, kwa kunipa tahadhari hii, hata mimi mwenye kisomo cha kutosha, lakini utambuzi wangu bado unakuwa ni hafifu.
Najua tupo wengi tu watu wa namna yangu ndani ya nchi yetu hii.
Tunapoambiwa ukweli juu ya matendo kama haya yanayokihusu chama chetu cha CCM, na viongozi wetu, (wenzetu), bado tunakuwa wagumu wa kuamini tunachoambiwa, kwa sababu zetu mbalimbali zisizo na mashiko. Tunatafuta visingizio vya kila aina kuendelea kuhalalisha uovu wa hawa waTanzania wenzetu tuliowaamini watuongoze.


Kwa hiyo, wakati mimi msomi ninayejiamini, na kujitambua ninaposhindwa kuyaona haya na kuyakataa, mTanzania mwenzangu aliyeko kule kijijini ambako CCM ya Mwalimu Nyerere ndio bado anaiamini akijua inaendelea kulinda maslahi ya wakulima na wafanya kazi, huyu mwananchi mwenzetu ataachaje kuendelea kuichagua CCM?

Tunao wasomi wengi sana ndani ya CCM, niwataje wachache vijana, kwa sababu unafiki ni lazima ufikie mwisho. Watu ni lazima waambiwe ukweli na wajijue wao ndio wasaliti wanaposhiriki kwa njia yoyote kuendelea kulididimiza taifa hili.
Kuendelea kufichana ukweli ndio msingi wa maovu ya CCM kwa waTanzania.


Hawa vijana wasomi ndani ya CCM wanafanya nini:
Januari Makamba
Bashe
Kigwangala
Nape
Kassim Majaliwa
Madilu Mwigulu Nchemba
Kama sio wanafiki watueleze wanafanya nini.
 
Perfect.

Kwa hiyo Chavda wetu alinunua deni kwa 2.5 millioni, jamaa akaenda kuvuna mabilioni toka kwa mdaiwa ambaye ni serikali yetu!

Nimekupata barabara na kila kitu sasa kimefunguka vyema.
Haya tuendelee!
Ndiyo mkuu. Walikuwa wamejipanga kama mafisi waliokamata mzoga.

Kwa Mfano Chavda baada ya kununua hilo deni kwa 2.5m Tzs, alipewa mkopo wa Tzs 661m, ili kuendeleza mashamba ya mkonge ambapo yangeliingizia Taifa pesa za kigeni(deni la Taifa hulipwa kwa fedha za kigeni).

Lakini yeye hizo pesa, akawagawia ama “kuwalipa” Subash na Patel bila hata ya kuonyesha malipo hayo yalikuwa ya minajili gani ama kazi gani!

Wenzake nao walipochukuwa mikopo kutoka kwenye kampuni zao, walifanya hivyo hivyo kugawana, huku vigezo vya kukopa pesa hizo za wavuja jasho vikiwa ni kuanzisha biashara Alan shughuli zitakazolipatia Taifa pesa za kigeni, kutengeneza ajira na kusaidia uchumi wa nchi kwa ujumla.

Hata Kagoda ya RA yenyewe ilichukuwa kwa sababu za kilimo!

Swali ninalojiuliza, hata kama walipewa hizo pesa kifisadi, kwanini hata wasingewekeza kama walivyokubaliana kwenye kupewa hizo pesa? Kwasababu at least tungenufaika kama Taifa na wananchi wangepata ajira nk. Kuna waliodai ni viwanda vya ngozi nk. Ingekuwa kweli uchumi ungeimarika! Na wangewekeza kwa wakulima pia ingewanufaisha wananchi walio wengi ambao ni wakulima wenye vipaji vidogo ama masikini.

Hizo pesa mpango mzima waliamuwa kuziweka kwenye akaunti ya madeni ya nje ama EPA! Nadhani waliona huko hazitakuwa monitored! Maana kama ni za kulipa madeni si ni kama zimeshatoka? Kwahiyo wakazitafuna badala ya kuziwekeza ili kulisaidia taifa kwenye uchumi na ulipaji wa madeni ya nje!

Baada ya zile kelele, JK aliwaambia baadhi yao(hao wa EPA ya pili), kuwa wazirudishe na kwamba wakulima watapewa hizo pesa! Hadi leo hakuna anayejuwa status ya hizo zilizopatikana kwenye hii EPA ya pili. Kumbuka EPA ya kwanza ni hiyo ya miaka ya 90 kabla hawajaanza mpango rasmi wa kuzichota kutoka kwenye akaunti maalum iliyofunguliwa.

Kitendo walichokifanya, ni kutuongezea urefu wa shimo... down deep in a rabbit hole!
 
Sijui wangapi wanakumbuka wakati Ikulu yetu ilipogeuka na kuwa kama pango la walanguzi, naam waliokuwa wanunuzi wa madeni walikuwa kama walanguzi wengine tu. Ilifikia hatua ambapo first lady alikuwa anaitwa shemeji na walanguzi hao. Tofauti yao na walanguzi tuliokuwa tunawapiga vita ni kwamba wao walikuwa wanailangua serikali yetu. Baba wa Taifa ambaye kitaaluma alikuwa mchumi alitambua mara moja hatari iliyokuwa inalinyemelea taifa letu na hakukaa kimya.



Mikataba yote ambayo walanguzi hawa walikuwa wanaingia na serikali ilikuwa inapata pia baraka za aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Huyo mwanasheria wa serikali ananikumbusha aliyekuwa mwanasheria wa Rais wa Marekani wa sasa Michael Cohen. Huyo baada na kushtakiwa sasa anatubu na kuelezea jinsi alivyokuwa akitekeleza majukumu yake huku jela ikimsubiri. Tofauti na Tanzania ambapo mtu kama huyo aliyehusika katika mikataba yote hiyo anaendelea kula bata. Tuendelee...
 
Wapi Idd Simba mzee wa UDA? Umenikumbusha Meridian Biao. I hope it was not a scheme to fund top position aspirant/s. Mambo ya Club Saigon
Soma hayo makampuni niliyoweka pamoja na wamiliki wake. Kama sikosei Iddi Simba nilimsikia in one way or another.
 
Back
Top Bottom