Baniyani Mbaya Kiyatu Chake Dawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baniyani Mbaya Kiyatu Chake Dawa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Spear, Apr 3, 2011.

 1. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2011
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbunge atoa milioni 6.5/- kwa waathirika


  [​IMG]MBUNGE wa Igunga, Rostam Aziz ametoa pole ya Sh milioni 6.5 kwa wananchi walioathiriwa na mvua kubwa wilayani hapa WAATHIRIKA wa mwishoni mwa wiki iliyopita.
  Janga hilo lilisababisha kaya 66 kukosa mahali pa kuishi katika kitongoji cha Hani wilayani hapa.
  Mbunge huyo alikwenda kuwatembeloea waathirika hao katika zahanati ya Kata ya Igunga jana.
  Alisema alitoa fedha hizo kwa kaya 13 ambazo zina watu 103 ambao hawana makazi hadi sasa.
  Kila kaya itapata takriban Sh 500,000 kukarabati nyumba zilizoezuliwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali, alisema.
  Wanahifadhiwa katika zahanati hiyo wakati halmashauri itasaidia kwa mahijati mengine ya binadamu.
  Mbunge huyo alisema katika tukio hilo hakuna mtu aliyepoteza maisha bali majeruhi wapatao 10
  wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga
   
 2. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Poleni wananchi wa Igunga pamoja na janga hilo lakini bado fikirieni kuhusu huyo mwizi.:noidea:
   
 3. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Poleni sana Watanzania wenzetu wana Igunga
   
 4. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Siyo bure. Wewe nadhani umelogwa. Yaani unasifia mtu anayetekeleza majukumu yake, tena kwa hela ya wizi! Ulitaka watu hawa wasaidiwe na nani zaidi ya yule aliyewarubuni kwa kanga na fulana ili kupata kura zao? Hebu ona aibu kidogo mkuu!
   
 5. m

  mtwevejoe Member

  #5
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huo siyo msaada,bali anarudisha pesa alizoiba,Tangia lini mwizi akatoa msaada?
   
 6. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Siamini kama ni mwizi ni Choyo cha baadhi ya viongozi haingi akili iwe leo mtu mwizi achiwe na serekali inayongoza nchi bila yakufikishwa katika vyombo vya sheria jamaa ni mchapa kazi na anpenda wapiga kura wake Hata Raisa kikwete amekuwa akilisema hilo mara kwa mara kuwa huyu jaama ni mchapa kazi
   
 7. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  ....ukweli ni kwamba CHUKUENI MWANASIASA YEYOTE MNAEMJUA NA KUMUAMINI NA MUMPELEKE IGUNGA AKAGOMEBEE DHIDI YA RA....
  NAWAHAKIKISHIENI.... ITAKUWA AIBU!!!
  Nyie tuendelee kuwaandika MAFISADI HUMU, NA KUPIGA KILA AINA YA KELELE, LAKINI KWA WANAKIJIJI MMMH!
   
 8. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Jamaa macho tu yanaonyesha kwamba ni mwizi
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  Apr 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,148
  Trophy Points: 280
  Kaiba nini?
   
 10. b

  banyimwa Senior Member

  #10
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi nyie watu wengine utumwa umewatawala sana mpaka mkiibiwa mnaona fahari mradi anayewaiba siyo mswahili mwenzio. Yaani wewe unadhani wezi wote wanafikishwa mahakamani au wale wanaofikishwa mahakamani wote ni wezi. Omba ondoa hoja yako ambayo iko too cheap to deserve a response. Yaani huyu mtu anayemwaga mabilioni kuwachafua wenzake, kuwang'oa madarakani wanaompinga na kuwahonga wapambe na watumishi wasio na uadilifu ili aendelee kubaki uraiani ndo anatoa milion 6.5 kwa wapiga kura wake, wakati hiyo hata nyumba moja ya matofali ya kuchoma haijengi halafu wehu wanamsifia!
   
 11. only83

  only83 JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Aliyekwambia hii nchi ina serikali nani? Nchi inajiongoza mkuu.....umeuzwa muda mrefu shauri yako...
   
 12. only83

  only83 JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Unatia hasira wewe....ungejua ungejitoa humu JF,kama unaakili timamu kweli hujui huyu fisadi kaiba nini...shit! foolish Tanzanians like you...
   
 13. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi nafikiri hizo ni ndogo sana kwake, aongeze au awajengee waathirika wote wa janga hilo nyumba mpya.
   
 14. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
   
Loading...