Pre GE2025 Serikali yatoa bilioni 2.5 kuendeleza ujenzi hospitali ya Dtk. Samia Muheza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
1,091
1,792
Serikali imeipatia hospital ya Dkt Samia Suluhu Hassan iliyopo wilayani Muheza kiasi cha sh. 2,570,164,000 fedha kuendeleza ujenzi wa hospitali hiyo pamoja na ununuzi wa vifaa tiba.

Akikabidhi sehemu ya vifaa tiba vilivyotolewa na serikali Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Hamis Mwinjuma maarufu MwanaFA, alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa alioufanya katika sekta ya afya katika wilaya ya Muheza.

Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Alisema hafla ya kukabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 300 inatokana na dhamira njema ya Rais, kuboresha huduma kwa kuwasogezea huduma za afya wananchi nchini kutokana na kujengwa zahanati, vituo vya afya na hospital.
1739974703008.png


Alisema Rais tangu aingie madarakani ameguswa na kutibu kiu ya Watanzania ya kupata huduma bora za afya akieleza kwamba wananchi wa Muheza watakuwa mashahidi ya kazi ambazo zimefanywa na serikali.

Alisema serikali imeweza kutoa kiasi cha shilingi bilioni 1.470 kuendeleza ujenzi wa hospital hiyo kusimika mashine za X-ray zenye thamani ya shilingi milioni 199.864 ikiwemo kuleta fedha kiasi cha shilingi milioni 900 za kununulia gari la wagonjwa (Ambulance).

Vifaa ambavyo mheshimiwa Naibu Waziri na mbunge wa Muheza amekabidhi ni pamoja na vifaa vya meno, vifaa vya mazoezi tiba (Physiotherapy), vifaa vya maabara, mionzi na vifaa mchanganyiko vyenye thamani ya shilingi milioni 300.

"Vifaa hivi ninavyokabidhi leo vinakwenda kuboresha utoaji wa huduma za afya katika wilaya yetu, kwani Sasa tutaanza kutoa huduma za matibabu ya mazoezi (Fiziotherapia) kwa waliopata madhara yatokanayo na ajali, kiharusi na unene uliokithiri.

Mbunge huyo alitoa Rai kwa watumishi wa hospital hiyo kuhakikisha kwamba wanatunza vifaa hivyo na vinafanyiwa matengenezo mara kwa mara kwakuwa vifaa hivyo vimenunuliwa kwa fedha nyingi.

Awali akizungumza katika risala yake Mkuu wa Divisheni ya afya na ustawi wa jamii na lishe na mganga Mkuu wa hospital hiyo Dkt Fani Mussa alimpongeza mbunge MwanaFA kwa mchango wake katika hospital hiyo wa kiasi cha sh 73,764,453.56 ambao ulininulia vifaa tiba.
 
Back
Top Bottom