Wana Ukumbi,
Kurejea kwa Dr Slaa kutoka Marekani lilikuwa ni tukio la furaha kwa wapenzi wa CHADEMA na katika kuonyesha hisia za furaha yao baadhi ya mashabiki wameenda mbali zaidi na kuivuka mipaka!
Imeelezwa na mmoja wa viongozi waandamizi wa CUF kuwa, wameshuhudia mabango yakisomeka "Dr Slaa ndiye rais wa awamu ya 5 wa Watanzania" siku ya mapokezi ya Dr Slaa katika viwanja vya mwalimu JKN!
Mtoa habari aliongeza, "Kwa kuzingatia makubaliano tuliojiwekea UKAWA, mabango yaliyokuwa na maneno hayo ni mkakati wa CHADEMA katika kushinikiza Dr Slaa asimamishwe kwenye nafasi ya mgombea urais kupitia UKAWA, kinyume kabisa na tulichokubaliana kwenye kikao."
Kwa mujibu wa makubaliano ya UKAWA yaliyofanyika Zanzibar ni kwamba, mjadala kuhusu nani atasimama katika nafasi ya urais usogezwe mbele ili kutoa muda kwa vyama washiriki kutathmini nani anafaa kuwa mgombea wa UKAWA.
Viongozi hao wa CUF (Zanzibar) wameandika barua makao makuu ya CUF kumtaka mwenyekiti taifa kuwaonya CHADEMA kuhusu kuheshimu na kulinda makubaliano ya vikao ili kuendeleza umoja wao huo wa UKAWA pasipo migogoro isiyo ya lazima.
Source: Zanzibar leo
Bango lililozua mgogoro ni hili hapa chini:
View attachment 246513