Bangladesh yafunga tovuti za ngono

Bangladesh yafunga tovuti za ngono

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,609
SERIKALI ya Bangladesh imezima takriban tovuti 20,000 ambazo zimekuwa zikipeperusha mambo ya ngono na michezo ya kamari, kama sehemu ya operesheni ya kumaliza biashara hiyo, waziri amedhibitisha.

Watoaji wa huduma za intaneti wiki iliyopita waliondoa tovuti zote ambazo zinatoa huduma za Kamari ama kanda za ngono, baada ya kuamrishwa na mamlaka ya kudhibiti mitandao ya mawasiliano nchini humo.

“Nataka kuwe na intaneti salama na safi kwa raia wote wa Bangladesh, ikiwemo watoto. Na hivi ni vita vyangu dhidi ya mitandao ya ngono na vitakuwa vita visivyoisha,” akasema Mustafa Jabbar, waziri wa mawasiliano.

Mitandao ya kijamii kama TikTok na Bigo ambayo ina umaarufu mkubwa nchini humo- na ambayo serikali inaamini imekuwa ikitumiwa vibaya- aidha ilizimwa, Bw Jabbar akadhibitisha.

Mitandao mingi iliyozimwa imekuwa ikiendeshwa kutoka nje ya nchi hiyo, japo mingine pamoja na ile ya kijamii imekuwa ikiendeshwa kutoka ndani ya mipaka yake.

Operesheni hiyo ilianzishwa baada ya Mahakama Kuu ya nchi hiyo Novemba mwaka uliopita kuamrisha tovuti za ngono kupigwa marufuku na kuzimwa.

Korti ilitoa uamuzi huo baada ya shirika la kutetea haki kufika kortini, likisema kuwa mitandao mingi ilikuwa ikichapisha mambo ya kupotosha kimaadili.

“Tunachunguza kurasa za Facebook za humu nchini, mitandao ya Youtube na tovuti pia,” akasema Bw Jabbar.

“Chache zimezimwa kwa kuwa na mambo yasiyokubalika kimaadili. Tumeshauri watu wengine kutochapisha kitu chochote ambacho kinakiuka maadili yetu ya kijamii,” akasema.

Bangladesh kuna zaidi ya raia milioni 160 na asilimia 90 yao ni watumizi wa intaneti. Masuala ya ngono yamekuwa yakiongoza kitu ambacho raia wa nchi hiyo wanatumia kwenye intaneti sana.

Taifa leo
 
Duh! Kama Asilimia Kubwa Ya Wananchi Ni Wapenzi Wa Hayo Mambo Basi Hilo Ni Pigo Kubwa Sana Kwao!
 
amedhibitisha = amethibitisha

Kudhibiti na kuthibiti zina maana tofauti.
 
Pamoja na nia safi serikali haina uwezo wa kudhibiti distributed system.
 
Safi sana.

ᴾᵘⁿⁱˢʰ ᵒⁿˡʸ ʰᵉ ʷʰᵒ ᶜᵒᵐᵐⁱᵗᵗᵉᵈ ᵗʰᵉ ᶜʳⁱᵐᵉ✓
 
Back
Top Bottom