Shirika la kutetea haki za wanahabari, Reporters Without Borders (RSF), imelaani hatua ya Niger kusitisha machapisho ya vyombo tisa vya habari vya Ufaransa. Hii inakuja wakati serikali ya kijeshi nchini humo ikiendelea kukaza uzi katika kuwakandamiza wanahabari.
Niger ilitangaza uamuzi huo siku ya Ijumaa Mei 8, 2026, ikidai kuwa vyombo hivyo vimekuwa vikitangaza maudhui ambayo "yana uwezekano mkubwa wa kuvuruga usalama wa umma, umoja wa kitaifa, mshikamano wa kijamii, na utulivu wa taasisi za Jamhuri."
Kwa mujibu wa tamko lililosomwa kupitia runinga na Mamlaka ya Mawasiliano ya Kitaifa (ONC), mashirika yaliyosimamishwa ni:
Mamlaka hiyo ilisisitiza kuwa uamuzi huo unaanza kutumika "mara moja" na unahusisha mifumo yote ikiwemo ving’amuzi vya satelaiti, mitandao ya kebo, mitandao ya kijamii, tovuti, na programu za simu (apps).
RSF imeuita uamuzi huo kuwa ni wa "uonevu" na wenye nia mbaya. Katika tamko lao walilochapisha kwenye mtandao wa X, walisema:
"RSF inalaani mkakati huu ulioratibiwa wa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari ndani ya muungano wa AES (Muungano wa Mataifa ya Sahel) na inataka uamuzi huu wa kidhalimu ubatilishwe mara moja."
RSF ilitoa tamko hilo kwa nchi za Niger, Mali, na Burkina Faso—ambazo zote zinaongozwa na serikali za kijeshi na zimeonekana kufuata mkondo mmoja wa kudhibiti habari.
Source: Al Jazeera

- France 24 na RFI (Radio France Internationale)
- France Afrique Media na LSI Africa
- AFP (Agence France-Presse)
- TV5 Monde na TF1 Info
- Jeune Afrique na Mediapart