Bandarini Dar: Utoaji wa gari!

Umesahahu kumwambia kuwa TRA wana bei zao....hiyo CIF yako toka Japan weka pembeni.....hayo mahesabu yaliyotolewa hapo juu yatakusaidia kukupa picha itakavyokuwa.......lakini jiandae na bei watakayoweka TRA ndiyo itakayopigiwa hesabu hizo hapo juu

Mkuu naona hapa unapotosha kidogo......TRA hawana bei yao, in principle inatakiwa waanzie kny CIF value kucalculate taxes zote kuarrive at total taxes payable, sasa kama wewe documents zako hazieleweki, ni forged etc ndio wanafanya uplifting ya CIF na sio vinginevyo.....! refer post ya Mpendanchi!
 
Lazima pia uwe na shilingi elfu tano tano kwa ajili ya kuwapa wapambe wakuonyeshe gari lilipo, wakukuonyesha ufunguo, wakukulindia, wakukuharakishia ili wasikufanyie mizengwe hadi 11.59 jioni, nn.k
 
nilisahau lazima pia umwombe mungu ashikilie hasira kwani waweza kumpiga / dunda DALALI wako pia
 
wazo lingine bora baada ya kupiga mahesabu hakikisha hiyo pesa ipo.....ndugu usiombe
likafika huna pesa za kutolea ndugu gari hilo linakuwa la TRA..........hizi mistake wengi wanazifanya....all the best
 
Mkuu naona hapa unapotosha kidogo......TRA hawana bei yao, in principle inatakiwa waanzie kny CIF value kucalculate taxes zote kuarrive at total taxes payable, sasa kama wewe documents zako hazieleweki, ni forged etc ndio wanafanya uplifting ya CIF na sio vinginevyo.....! refer post ya Mpendanchi!

kutokana na uzoefu wangu (note: sikuwahi kuwa na Forged Document wala nini mara nyingi tu nimeagiza gari na haya masuala yamenikuta)...........suala la ku-uplift haliko wazi kabisa na vigezo vyake haviko wazi.........na ndio mlango mwingine wa Rushwa pale TRA.......Ikiwezekana lile lijitabu lao likubwa basi na liwe accessible na wananchi (na waliweke hivyo vigezo vyao mtandaoni kabisaa)......na sio kuwashangaza wananchi pale wanapoleta Uplift zao za KIUONEVU.....BTW kwanini nyintyi TRA hamjifunzi kutoka kwa vyombo vingine kama hivyo hapo jirani zetu....?

Mimi nazungumzia uzoefu wangu pale.......kamwe sijawahi ku-forge document........sasa kama wewe unataka mshikaji akaawaachie gari TRA wee enedelea.............

Ndg Papizo.......Jamaa wengine hapa wapo kutetea TRA pamoja na utendaji wao m-bovu...............kama walivyokuambia wengine hapo juu.........jiandae kukutana na mambo yatakayokutia HASIRA.........uwe mvumilivu......na please ni vema ukawa na pesa yako ya kutosha kama nilivyokushauri...............

Bytheway....Papizo ukisha litoa Gari lako tungependa kupata feedback mambo yaliendaje............
 
Suala la Ku-Uplift kutokana na uzoefu wangu sikuwahi kuwa na Forged Document wala nini (mara nyingi tu mimi nimeagiza gari na haya masuala yamenikuta).......suala la ku-uplift haliko wazi kabisa.......na ndio mlango mwingine wa Rushwa pale TRA.......

Mimi nazungumzia uzoefu wangu pale.......kamwe sijawahi ku-forge document........sasa kama wewe unataka mshikaji akaawaachie gari TRA wee enedelea.............

Ndg Papizo.......Jamaa wengine hapa wapo kutetea TRA pamoja na utendaji wao m-bovu...............kama walivyokuambia wengine hapo juu.........jiandae kukutana na mambo yatakayokutia HASIRA.........uwe mvumilivu......na please ni vema ukawa na pesa yako ya kutosha kama nilivyokushauri...............

Bytheway....Papizo ukisha litoa Gari lako tungependa kupata feedback mambo yaliendaje............

Nimetoa gari mara mbili, sijawahi kupata uplift au kucheleweshewa kutoa gari kiasi cha kulipia storage charge.

Kama gari ya million 4 unaandaa milioni 4 na zaidi, plus usumbufu na kusubiri muda mrefu; kwa nini usiende show room ukachague gari, ulipie vinavyopaswa the uko barabarani na mchuma wako.
 
Uplift ya bei kwa TRA wanafanya sana kama umeagiza kutoka kwenye kampuni isiyoeleweka au umenunua kwa mtu binafsi. Ila kama umenunua kwa kampuni inayoeleweka huwa haina shida. Kuhusu show rooms za hapa Bongo ni hatari sana hasa kama huwafahamu wauzaji maana wanaleta magari mabovu sana kutoka Dubai na bei ni kubwa mno. Kama unataka gari agiza mwenyewe kutoka mnadani moja kwa moja Japan, bei ni rahisi mno na utaangalia details za gari unayoitaka kabla hujanunua. Epuka kununua gari yenye zaidi ya miaka 10 ili kuepuka faini ya 10%. Kama unataka gari ingia hapa http://www.tradecarview.com/stock/pr/7656/220/?si=220. Kuhusu clearing agents nafikiri kwa gari ndogo kama Mark II haizidi laki 2 siyo laki 5.
 
Kwa bahati mbaya sana, clearing agents wanaotakiwa kuwasaidia wateja wao kutoa mizigo yao bandalini yakiwamo magari, ndio hao hao wanaoshirikiana na watu wa TRA kuwaumiza wateja wao!! Mimi niliagiza gari kupitia Dar port sasa clearing agent wangu akazembea kuprocess documents; kumbe meli iliisha fika zamani na gari kushushwa nakuchelewa kwake kukanifanya nilipe demurrage charges almost $2000!! Licha ya kuniomba fedha za kuwahonga watu wa bandalini na gharama zake agent mwenyewe!!!. Ni muhimu kumtafuta clearing agent anaeheshimu kazi yake na muadilifu kwani si wote wachafu.
 
Nimetoa gari mara mbili, sijawahi kupata uplift au kucheleweshewa kutoa gari kiasi cha kulipia storage charge.

Kama gari ya million 4 unaandaa milioni 4 na zaidi, plus usumbufu na kusubiri muda mrefu; kwa nini usiende show room ukachague gari, ulipie vinavyopaswa the uko barabarani na mchuma wako.

Mama,
tafadhali tuwekee structure ya kodi uliyolipa wewe iwapo hautajali.
hili swala linatuchanganya wengi, apparently mpaka Rais wa nchi linamchanganya!
 
Bongo kweli tumelala. Hii thread ipo siku ya pili sasa, Bandari ina Afisa masoko, Afisa uhusiano, mkurugenzi mkuu na maofisa kibao. Hamna hata mmoja anayekuja kuitetea bandari yao hapa !! Watu wanabishana kwenda Mombasa, lakini wao kimyaaa... Wanashindwa hata na Malkia Elizabeth mwenye Facebook!! Matangazo siyo lazima yatoke kwenye gazeti la Mzalendo.Kuja kutetea hoja hapa inaweza kulipa zaidi....
 
Mkuu Dilunga,

Kwenye soko huria hakuna 'kwetu' wala 'ukwetu'

si unasikia jinsi champions wa ku-advocate soko huria jinsi wanavyobuni mikakati ya kuyabana makampuni ''yanayo ship jobs overseas''. Sasa akili kichwani, ukidanganyika kuwa soko huria ni muhimu kuliko uchumi wa nchi yako utabaki hapohapo.
 
Politically unaweza ukawa sahihi, lakini ktk mazingira halisi jaribu kuchukulia scenario ifuatayo; Mathalan mimi kama mwananchi mjasiriamali nimedunduliza ndururu zangu kwa miaka yote ya ujana wangu naanzisha biashara, nachukua mzigo say China nataka kuutoa bandarini, Mombasa wanataka USD 3,000 mzigo unakuwa tayari 1 week. Dar wanataka USD 6,000 + mikwaruzo na kubembeleza huduma + miezi 3 ya ucheleweshaji. Unategemea nitakubali nilipe zaidi na kucheleweshewa biashara zangu?

Huu ndio utandawazi, unatiririsha fedha kwenye route inayolipa zaidi.
 
Mfano uliotoa hauko sahihi,
Kodi ya mzigo uliotoa Mombasa hauilipii Bandarini, unailipia mpakani Horohoro na bei yake haitofautiani na ile ya DSM unless unadhamiria kucheza ''karate''. Ukijumlisha na gharama za kuusafirisha mzigo mpaka Dizim unarudi palepale. Bandari ya Mombasa wanaitumia watu wanaitaka kucheza carate mpakani, ili kuepuka kodi. Huo ndio uhalisia wenyewe, na tunaujua ipasavyo.
Swala la sababu kubwa ya ucheleweshaji waliotangulia wamelifafanu ipasavyo, nadhani umepitia michango yao.
Tusipokuwa wazalendo tutashindwa kuwafundisha watoto wetu uzalendo halafu wataishia kuwa watumwa.
 
Pia kuna wakala anaitwa TISCAN naye hu-evaluate docs na anaweza ku-uplift pia. So kuna uwezekano wa kuwa uplifted na both TISCAN na TRA au hongo kwa wote. Lakini usumbufu mkubwa upo kwa clearing agents. Hawa kila time mm lazima kugombana nao...hawa ni headache mbaya.
 
Mhhh mbona kazi ipo. Sasa na kama ndiyo nataka kutoa kontena lenye personal effects (i.e. gari, nguo, furniture, electronics, etc... nimeishi ughaibuni miaka minne), ngoma yake inakuwaje? Maana nasikia kuna misamaha ya kodi kwa "returning resident" lakini hizo info sijaziona anywhere kwenye website ya TRA.
 
Nadhani unajua Bongo Mafisadi wengi...kwa ushauri wangu jaribu kwanza kuangalia kama unaweza kupata hiyo gari bongo kisha nunua hapohapo bongo kwa Mafisadi kuepusha usumbufu...wanaingiza magari bila ushuru, kodi na wanauza bei chee. Sasa kwa nini upoteze muda kufuatilia gari la kuagiza.
 
Mhhh mbona kazi ipo. Sasa na kama ndiyo nataka kutoa kontena lenye personal effects (i.e. gari, nguo, furniture, electronics, etc... nimeishi ughaibuni miaka minne), ngoma yake inakuwaje? Maana nasikia kuna misamaha ya kodi kwa "returning resident" lakini hizo info sijaziona anywhere kwenye website ya TRA.

na hilo ndio tatizo tunalopigia kelele hata kwenye idara nyingine.........yaani information ambazo ilibidi kuwa public....zinafichwa!!....yaani bongo!!
 
Back
Top Bottom