Angalia msidanganyike kirahisi hivyo, bandari ya Dar kwa upande wa magari kwa kweli kwa sasa wamejitahidi sana, wameboresha huduma, hata ule wizi siku hizi hakuna tena. Hiyo ya Mombasa ni njia ilikuwa inatumiwa wakati ule TRA wanafanya uzembe kule mipakani ambapo watu walitumia ujanja kuingiza magari bila kulipia zile tax muhimu zote. Lakini kwa sasa ukitumia Mombasa nakuhakikishia it will cost you more than if you use Dar port. Ninafanya sana hizo biashara najua what is happening this time. Last week kuna gari ya mdogo wangu mmoja mbishi sana naye tumemshauri atumie dar port amebisha. Kilichomtokea anajuta hadi leo. Amelipa 2times more than mwenzake aliyepitisha dar port.
Kuhusu gari kuchukua muda mrefu pale dar port sometimes tunawalaumu TRA kumbe uzembe ni wetu, watu wana forge documents ili CIF ionekane ndogo walipe kidogo. Sasa zile documents zikishakuwa proccessed ziko kwenye final kuna CIA wa TRA ambao wanapitia at last!! wakishagudnua hilo wanazirudisha inabidi uanze upya zoezi zima na utalipa Uplifted CIF.
Mkuu nakushauri tumia document zako kama zilivyo bila forgery yeyote utapata gari lako within two weeks.
Mkuu hilo ni kweli, siku hizi wameimprove kwa magari, ila pia hakikisha una mpata agenti shapu!