Balozi Juma Mwapachu atangaza kurejea CCM...

Balozi Juma Mwapachu atangaza kurejea CCM...

Haha mkuu nimepigwa na butwaa!!!

Huyu ndiye alikuwa think tank ya EAC as secretary general!!!!

Dah nchi hii ina mambo!!!!

Labda ni uzushi....ngoja tusubiri tuone.

Manake siku hizi kuna kila aina ya uzushi kwenye hii mitandao!
 
Kama ni kweli karibu nyumbani maana waswahili husema kanga hatagi ugenini. pia Mwenda tezi na omo marejeo ngamani.
Hata hivyo hukupanda jukwaani kuumiza ulikotoka, hukuchukuwa kadi wala kujiunga na chama kingine bali ulimuunga mkono mwana ccm mwenzio wakati akisafishwa na waliomchafua.
 
Baada ya miezi miwili ya uongozi wa Magufuli nataka niseme nilikosea sana. Nililewa mahaba ya Lowassa, nililewa ahadi ya Lowassa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje. Niliamini mafuriko ya Lowassa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi. Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo.
Kuna mzee mmoja tangia miaka ya mwanzoni mwa tisini amekuwa cdm na hakuwahi kutaka hata uenyekiti wa kijiji. Kikubwa ni kwamba yeye tangia miaka ya sabini hakuwa na imani na ccm na ndio sababu yake kufurahia vyama vingi pale aliposikia ujio wake.
Sasa wote mtaelewa kuwa Ndg. Mwapachu hakuja cdm kwa sababu ya kuguswa na matatizo na ufisadi wa ccm bali alifuata vyeo. Na kwa kauli ya Mh. Mbowe juzi kuwa "ukiwa cdm usiogope kulala lock-up" ni wazi cdm sio sehemu ya vyeo na yuko sawa kuendelea kufuata vyeo huko vinakopatikana!
Kama ni kweli, kwa wanaoangalia swala hili na jicho la tatu watakubaliana nami kuwa safari ya kuleta mabadiliko Tanzania bado ni ndefu.
 
Alikosea kutoka ccm kwa kuwa alimfata mtu badala ya chama, lakini karudi kwa kumfata maghufuli" mimi bado hapa sijaelewa
 
Mmmmh. Haya makubwa sasa. Kama ni yeye kweli angebaki tu bila chama. Maelezo hayo ya kwa nini aliondoka ccm si ya msomi wa leval yake.
 
Kama huyu balozi mashuhuri kweli kaandika hili, ngoma yetu ngumu sana Tanzania.

I mean utamlaumu vipi country bumpkin kama Magufuli au burlesk bully kama Ndugai ?
Haha braza nausoma huo ujumbe Mara mbili mbili siamini kama umetoka kwa MTU kaliba ya balozi!!!!

Hii ina reflect fikra na viwango vya kufikiri vya viongozi wengi hapa nchini..

Duh ni shida!!!
 
Mnafiki mkubwa huyu amerudi kwa wanafiki wenzake
 
Haionekani kama lugha ya Balozi Mwapachu but anyway, alihama CCM kwa njaa zake na kama karudi basi ni kwa sababu ya utaratibu uleule wa kwake....KUGANGA njaa! na bila shaka MAERSK wanadaiwa kodi.
 
Alihama baada ya kuhaidiwa uwaziri wa mambo ya nje, sijajua sasa amehaidiwa nini?
 
Haha braza nausoma huo ujumbe Mara mbili mbili siamini kama umetoka kwa MTU kaliba ya balozi!!!!

Hii ina reflect fikra na viwango vya kufikiri vya viongozi wengi hapa nchini..

Duh ni shida!!!
Mimi nimepata shaka mpaka nafikiri labda wamemzushia tu, hakuandika yeye.

Ndiyo maana nikatanguliza kauli yangu na "Kama..."

Inatisha.
 
Mimi nimepata shaka mpaka nafikiri labda wamemzushia tu, hakuandika yeye.

Ndiyo maana nikatanguliza kauli yangu na "Kama..."

Inatisha.
Ni kweli karudi ccm, mwananchi online nao wameandika
 
Arudi asirudi haongezi value yoyote CCM.Walitutelekezea CCM vitani yeye na akina kingunge na akina Sumaye tumepigana wenyewe tumeshinda.Sasa ni HAPA KAZI TU.Atajijua yeye na wenzie waliotusaliti na kusaliti CCM kwenye vita ya uchaguzi.
Petro alimkana bwana Yesu mara 3 akasamehewa nk. Kuomba msamaha ni kitendo cha uungwana
 
Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwa sababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu.


Hapa kidogo nimemwelewa kwamba kuna kazi zake haziendi kwa kuwa serikali inakwamisha kutokana na kumsaidia lowassa, yale maneno ya wafuasi wa chadema wananyanyaswa yanadhihilishwa wazi
 
NOTHING SIMSHAURI AJUTIE KUHAMA CCM NI HAKI YAKE YA MSINGI NA KUAMUA KURUDI PIA NI HAKI YAKE KIMSINGI / HAKUNA WA KUJIVUNA AU KULALAMA KWAMBA OOH ALIONDOKA OHH UHARO UHARO.

KWANI KUONDOKA KWAO NDIKO KULIKOLETA IMPACT HATIMAYE TUKAMPATA MAGUFURI/ KWANI MKUSUDIWA MKUU ALIKUWA MEMBE / WATANZANIA HAYA MAMBO YA KUZUNGUKA ZUNGUKA MBUYU HUWA HAYATULETEI FAIDA YOYOTE TUWE WAKWELI TU DAIMA.

NINGEFURAHI SIKU MOJA TENA BILA CHUKI WALA KINYONGO RAIS WETU MAGUFURI AKAMWALIKA NDG LOWASSA, IKULU NA WAKAPEANA MKONO KUONYESHA KWAMBA UCHAGUZI UMEPITA NA SASA NI KAZI TU, THATS THE GOOD STANDARD SMARTS POLITICS.
 
Mimi nimepata shaka mpaka nafikiri labda wamemzushia tu, hakuandika yeye.

Ndiyo maana nikatanguliza kauli yangu na "Kama..."

Inatisha.
Inawezekana kweli amerudi lakini hayo maandishi wameandika watu wengine kwa malengo yao? Nitashangaa sana sana kama atakuwa ni yeye kaandika hii!
 
Mimi nimepata shaka mpaka nafikiri labda wamemzushia tu, hakuandika yeye.

Ndiyo maana nikatanguliza kauli yangu na "Kama..."

Inatisha.
Hahahah, eti Magufuli ni Nyerere.....
 
Back
Top Bottom