Balozi huyu ni Mbaguzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi huyu ni Mbaguzi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Game Theory, Feb 11, 2008.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Je wana CHADEMA au CUF watakapo muita kwenye mikutano yao atakuja au?

  Keshaitwa kuhudhuria mikutano ya jumuiya mbili za watanzania akajidai yuko bize lakini jumuiya ya abuu faraji anakwenda na CCM ndio zaidi


  Mumewe ilibidi agombane na watu ndipo akaamua kuachia ngazi kutaka huo uenyekiti sasa jamani mambo haya yanakubalika?

  Najisikia mnyonge sana nionapo mabalozi wetu wanapoingia kwenye ushabiki wa kiasiasa


  Je sheria inasemaje?


  sherehe za kuzaliwa ccm reading  [​IMG]
  Mgeni wa Heshima Balozi wa Tanzania Bi. Mwanaidi Maajar akiwa na Bw. Maajar na Katibu wa CCM Tawi la London Bi Suzan Mzee.

  [​IMG]
  Mdau Wa TanzananiaOne Uk Ally Muhdin akiwa na Balozi Bi Maajar

  [​IMG]
  Wadau wa Southhampton wakiwa na Mgeni wao Toka Bongo

  [​IMG]
  Wadau wa Tanzania association kutoka kushoto Juma Pinto , Abuu Faraji na John Lusingu
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Huyu Mama mimi namjua kama ni Chadema damu na U CCM ni baada ya kuchukua Ubalozi.Sasa mengine siyajui.
   
 3. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2008
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Mkuu Lunyungu heshima mbele!

  Sasa ndugu mbona unamwaga the dataz hapa...unataka mama awe jobless ghafla kama kijana wa Ngoyai? mzee mkuu wa kaya akitonywa mama akapoteza kitumbua...utalaumiwa weye..mi simo!

  Brazamen..mbona weekend bado bana.....au utaratibu umebadilika...
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Unajua naangalia hizi picha napata wazo kwamba wengi wao hawajaja Tanzania miaka mingi sana .So hata siasa kwao si Siasa walienda kupoteza muda na kupata habari za wachache wao ambao wanakuja nyumbani kila mara .Wengi wamezamia na hawawezi tena kuja TZ maana hawana PP zao na wamejiita wakimbizi.Wengine akina Faraji na Minto wao wana mission ya kuyatafuta maisha so wanatumia kila njia kuweza kula na mafisadi kwa jina la CCM chama ambacho kina mafisadi wajuzi .

  Huyu kumwaga Unga hapana .Mkuu wa Kaya anajua kwamba huyu ni Mdhamini wa Chadema lakini ngeke likamwangukia na akapewa Ubalozini Mkulu ana sababu zake .Mimi wananichekesha hawa wabongo wa UK na kimbembe cha Uccm .Ni wa kweli hawa ?
   
 5. M

  Masatu JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wanasema "Shamba la Bwana Kheri, na Mbuzi wa Bwana Kheri!" hivyo waache wafanye watakavyo..........
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Huhuhuu Masatu bwana sawa mkuu .

  Hivi Samvulachole ni wapi walipo kupanhusa mikono kwenye uongozi wa akina Faraji ama ujumbe wa CCM UK ? Maana hii ngoma unaijua vyema njoo ubaelezee
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ukarabati unahitajika sana katika Balozi za Tanzania kwani wamekuwa watu ambao Mtanzania hawezi kuwafika kiurahisi labda wasikie unawapelekea mchango ,hapo ndio utawaona wakijichekesha chekesha kuna ufisadi wa fedha za Passport hadi hii leo kuna waTanzania wanakwenda mbio hawajazipata wanapewa matarehe tu kama ya mikakati ambayo utekelezaji wake ni baada ya miaka mia ndio mradi utatimia ,wakati tuliopo sasa tunakufwa na njaa.
  Utapeleka picha watakwambia sio ,nenda kapige sehemu fulani ulete na risiti kama umepiga hapo ,na baada ya hapo unaambiwa subiri utapigiwa simu basi ndio imetoka hiyo ,mpaka upande presha na kuwafuatilia ,hapo utasikia zimeshapelekwa Tanzania zikifika tu utakuwa mtu wa kwanza kupigiwa simu na ukiamua kwenda Tanzania utaipata na kurudi wakati ile uliyoomba pale ubalozini zaidi ya miezi sita haijafika ajabu wanaweza wakakupigia simu ukachukue pasi yako kwani imeshakuwa tayari na imeshafika ,utashangaa unakuwa na passport mbili !!!
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mwiba sasa umezinduka na unaongea kama mwiba kweli .Nilijua tu kwamba JF is a free University for Free Education . Unaanza kukomaa sasa .Karibu tuendelee
   
 9. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2008
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Wadau angalieni Msije Mtisha Mama wa Watu akaogopa hata Kuhudhuria Misa za Wafu. JF si-mchezo!!
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hapana yeye aende tu ila ajue kwamba tunamjua vilivyo na anapaswa kutumia Nchi na si Chama . Kama ni Chama baso iwe vyama maana ni balozi wa Watanzania .Akichukua side we know much and better .Faraji mchaga mwenzio anampa tenda zote za Ubalozini pesa zinaliwa hapo tuna mwangalia tu .Si matisho ajue tunaweza record.
   
 11. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Sula la BALOZI MWANAIDI MAJAAR kuwa mdhamini wa CHADEMA ni kweli na halina utata na nadhani wenyewe walipomchagua walilijua hili

  Tatizo ni pale anapo anza kuwa Biased katisha shughuli za watanzania

  Keshaitwa kwenye shughuli mbili za jumuiya mbili zinazowawakilisha Watanzania lakini kagoma kwenda kwa kisingizio cha ubize

  cha ajabu muda wa jumuiya ya Faraji anao

  Muda wa kwenda kwenye shughuli za CCM anao

  Je wasio CCM tutajisikiaje?

  Je hii ni directive toka FOREIGN au ni presha toka kwa Mumewe?

  Je kama mama Majaar ni innocent je anashindwa nini kumwambia mumewe kuwa mambo yake ya CCM yatakuwa na conflict of interest?

  Mwisho zaidi ni kuwa kwa sababu mwaka huu watu wameamua kuwavalianjuga hawa watawalawetu hamuoni kama mambo kama haya ni dalili za ma balozi kama Majaar kuwa katika hatari ya kuwa wabaguzi zaidi watakapo pewa nafasi kubwa zaidi za kisiasa?
   
 12. M

  Masatu JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kumbe mama Chadema baba CCM! makubwa!
   
 13. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2008
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Brazameni,Nakusikia usemacho Mkuu.Lakini hizo Jumuiya, hasa hizo MBILI unazozitaja hapo juu,je Ni jumuiya Rasmi?Zimeundwa chini ya Misingi gani?(Za-kidini,Kikabila,Kijinsia,kimajimbo,Kifamiliya???).Unaweza kututajia hizo jumuiya Mkuu?(Kwa manufaa ya Wa-Tz waishiyo UK)

  Kwasababu wasiwasi wangu ni kwamba kama kila mtu atataka eti Balozi ahudhuriye Vipaimara,Ndoa,Mahafali,Ujio wa Ze Comedy,basi itakuwa vigumu sana,na akitoa udhuru wa kutoweza jumuika nasi,tusimlaumu jamani,tumuelewe!!.
   
Loading...