barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Balozi Ami Mpungwe,mwanadipolomasia na mtumishi wa umma wa miaka mingi.Alikuwa balozi wetu wa kwanza wa Tanzania nchini Afrika Kusini,Ami Mpungwe ndiye aliyekabidhiwa na chama cha ANC kukaa na Nelson Mandela week nzima Manyara National Park wakati Mandela akiwa kwenye mfadhaiko mkubwa wa ndoa yake na Winnie Mandela.
Kwa ukweli Balozi Ami Mpungwe katika harakati na ukombozi wa kusini mwa Afrika hakuna asiyemfahamu,Jongwe Robert Mugabe,Thabo Mbeki,Comrade Pohamba,Jacobo Zuma na kina Kenneth Kaunda ni moja ya watu wanaomfahamu Mpungwe kama mmoja wa "vijana" wa Mwalimu Nyerere aliyepigania ukombozi wa nchi zao na kuufukuzia mbali ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini.
Lakini ukisema utaje watu waliotumbukiza nchi hii katika matatizo ya "uwekezaji wa makaburu" basi jina la mwana Ifakara Balozi Ami Mpungwe halikosi kuwepo,juzi ameonekana kwenye TV na wameitisha kipindi Maalumu ITV kuelezea kupanda kwa bei ya sukari,na kuwaelezea watu wanaoingiza sukari toka nje kama ni "Majipu yaliyoiva muda mrefu na kukosa kutumbuliwa",kauli hii si ya kutolewa na Balozi Mpungwe huyu tunayemfahamu.
Balozi amekuwa kama wakala wa wawekezaji "wanyonyaji" huku yeye akiwekwa kama "Non-Executive Director" ili kulinda maslahi ya wawekezaji hao.
Mfano wa Mashirika ambayo Mpungwe amewekwa kama "Buffer zone" yao dhidi ya Serikali ni kama:
-Tanzanite One
-Multi Choice Tz
-Illovo Sugar hawa wanamiliki Kiwanda cha Kilombero
-Tanzania Breweries
-NBC Tanzania Ltd(1997)
Air Tanzania Ltd(Hii aliiuza kwa South Africa Airways matokeo yake shirika letu likafa kifo cha mende
African Gem Resources
-TANESCO(Ndio aliwaleta Net Group Solutions kwa mtutu na wakaiharibu Tanesco).
Na kwasasa ni mwenyekiti wa Wazalishaji wa Sukari Tanzania,katika mashirika yote hayo aliyokaa hali kwa wazawa ilikuwa mbaya,kule Tanzanite One tumeona jinsi wafanyakazi walivyodhulumiwa na kuishi kwa tabu,mpaka sasa Tanzanite ikaonekana inatoka Kenya na S.Africa.
Sisi washabiki wa mpira tunajua jinsi DSTV ya Multi-Choice ilivyotulipisha kwa dola badala ya shilingi,wafanyakazi wa Kilombero na ugumu wa mazingira ya kazi.
Tunajua jinsi Air Tz ilivyochomekwa ndani ya South Africa Airways na kuiua kabisa,sasa South Afrika ndege yao inakuja mara mbili kwa siku Dar es Salaam wakati ATCL ipo mahututi,"Ujanja Ujanja" huu wa Comrade Mpingwe aligunduliwa na Balozi Abas Sykes wakati huo Sykes ni Mwenyekiti wa bodi ya ATCL akanusa jinsi Mpigwe anavyotaka "kuliuza" shirika,Kwa uchungu Sykes alisema "Mpigwe ni kijana wetu,tumemtuma Afrika Kusini akawe muwakilishi wetu,lakini amegeuka kuwa wakala wa makaburu na kutka kuliuza shirika letu,vijana wa sasa wanawaza maslahi yao badala ya maslahi ya Taifa",matamshi haya yalimfanya Balozi Mpingwe amfungulie kesi Balozi Abasi Sykes na Gazeti la Mtanzania,kesi iliunguruma Mahakama kuu kwa muda.
Huyu ndio balozi Mpingwe,Mwanadiplomasia wa kweli,Jongwe wa kusini mwa Afrika katika harakati za Ukombozi,mwana Ifakara kindakindaki na "wakala" wa makampuni yote ya makaburu Tanzania,anapata wapi kuwaita wengine "majipu" wakati yake mengi watu bado hawajayafumua??