Balozi Ami Mpungwe anapata wapi ujasiri kuwaita wengine "majipu"?

Mleta.mada umeleta analysis nzuri sana kumhusu huyu mheshimiwa Balozi mstaafu. Huko kwake Ifakara ni kijiji fulani utafikiri uko sicily italy. Hilo hekalu lake mbezibeach lina.ukuta wa vioo na pavement mtaa mzima. Yuko mtaa mmoja na.Balozi Peter Kabisa. Kwa kweli huyu mh ana utajiri wa ajabu kupitia utumishi wake serikalini. Mungu si mzee mkumba.asema mbwiga wa mbwiguke
 
Balozi Ami Mpungwe,mwanadipolomasia na mtumishi wa umma wa miaka mingi.Alikuwa balozi wetu wa kwanza wa Tanzania nchini Afrika Kusini,Ami Mpungwe ndiye aliyekabidhiwa na chama cha ANC kukaa na Nelson Mandela week nzima Manyara National Park wakati Mandela akiwa kwenye mfadhaiko mkubwa wa ndoa yake na Winnie Mandela.

Kwa ukweli Balozi Ami Mpungwe katika harakati na ukombozi wa kusini mwa Afrika hakuna asiyemfahamu,Jongwe Robert Mugabe,Thabo Mbeki,Comrade Pohamba,Jacobo Zuma na kina Kenneth Kaunda ni moja ya watu wanaomfahamu Mpungwe kama mmoja wa "vijana" wa Mwalimu Nyerere aliyepigania ukombozi wa nchi zao na kuufukuzia mbali ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini.

Lakini ukisema utaje watu waliotumbukiza nchi hii katika matatizo ya "uwekezaji wa makaburu" basi jina la mwana Ifakara Balozi Ami Mpungwe halikosi kuwepo,juzi ameonekana kwenye TV na wameitisha kipindi Maalumu ITV kuelezea kupanda kwa bei ya sukari,na kuwaelezea watu wanaoingiza sukari toka nje kama ni "Majipu yaliyoiva muda mrefu na kukosa kutumbuliwa",kauli hii si ya kutolewa na Balozi Mpungwe huyu tunayemfahamu.

Balozi amekuwa kama wakala wa wawekezaji "wanyonyaji" huku yeye akiwekwa kama "Non-Executive Director" ili kulinda maslahi ya wawekezaji hao.

Mfano wa Mashirika ambayo Mpungwe amewekwa kama "Buffer zone" yao dhidi ya Serikali ni kama:
-Tanzanite One
-Multi Choice Tz
-Illovo Sugar hawa wanamiliki Kiwanda cha Kilombero
-Tanzania Breweries
-NBC Tanzania Ltd(1997)
Air Tanzania Ltd(Hii aliiuza kwa South Africa Airways matokeo yake shirika letu likafa kifo cha mende
African Gem Resources
-TANESCO(Ndio aliwaleta Net Group Solutions kwa mtutu na wakaiharibu Tanesco).

Na kwasasa ni mwenyekiti wa Wazalishaji wa Sukari Tanzania,katika mashirika yote hayo aliyokaa hali kwa wazawa ilikuwa mbaya,kule Tanzanite One tumeona jinsi wafanyakazi walivyodhulumiwa na kuishi kwa tabu,mpaka sasa Tanzanite ikaonekana inatoka Kenya na S.Africa.

Sisi washabiki wa mpira tunajua jinsi DSTV ya Multi-Choice ilivyotulipisha kwa dola badala ya shilingi,wafanyakazi wa Kilombero na ugumu wa mazingira ya kazi.

Tunajua jinsi Air Tz ilivyochomekwa ndani ya South Africa Airways na kuiua kabisa,sasa South Afrika ndege yao inakuja mara mbili kwa siku Dar es Salaam wakati ATCL ipo mahututi,"Ujanja Ujanja" huu wa Comrade Mpingwe aligunduliwa na Balozi Abas Sykes wakati huo Sykes ni Mwenyekiti wa bodi ya ATCL akanusa jinsi Mpigwe anavyotaka "kuliuza" shirika,Kwa uchungu Sykes alisema "Mpigwe ni kijana wetu,tumemtuma Afrika Kusini akawe muwakilishi wetu,lakini amegeuka kuwa wakala wa makaburu na kutka kuliuza shirika letu,vijana wa sasa wanawaza maslahi yao badala ya maslahi ya Taifa",matamshi haya yalimfanya Balozi Mpingwe amfungulie kesi Balozi Abasi Sykes na Gazeti la Mtanzania,kesi iliunguruma Mahakama kuu kwa muda.

Huyu ndio balozi Mpingwe,Mwanadiplomasia wa kweli,Jongwe wa kusini mwa Afrika katika harakati za Ukombozi,mwana Ifakara kindakindaki na "wakala" wa makampuni yote ya makaburu Tanzania,anapata wapi kuwaita wengine "majipu" wakati yake mengi watu bado hawajayafumua??
Inawezekana nyie ndo waingiza sukari sasa imewachoma... Tulieni hivyo hivyo muendelee kutumbuliwa
 
Ungejuwa mkuu ZIRO walaa hata sihusiki na sukari.Hata mimi ninataka marufuku hiyo iwepo ili watu wa chini maisha yetu yawe salama..hili nimelisema tu si kwamba nina chuki nae,ndio maana mwanzoni nimeelezea kuwa huyu ni gwiji wa siasa za kidiplomasia za kusini mwa Afrika
 
Mleta.mada umeleta analysis nzuri sana kumhusu huyu mheshimiwa Balozi mstaafu. Huko kwake Ifakara ni kijiji fulani utafikiri uko sicily italy. Hilo hekalu lake mbezibeach lina.ukuta wa vioo na pavement mtaa mzima. Yuko mtaa mmoja na.Balozi Peter Kabisa. Kwa kweli huyu mh ana utajiri wa ajabu kupitia utumishi wake serikalini. Mungu si mzee mkumba.asema mbwiga wa mbwiguke
Huyu ndio Jongwe Ami Mpungwe...Mkuu visiwa vya Sicily umefika??kule ndio maskani ya Mafia huko
 
Inawezekana nyie ndo waingiza sukari sasa imewachoma... Tulieni hivyo hivyo muendelee kutumbuliwa
Mjibu jamaa kwa Hoja aliyoleta usipaparike kama kuku aliechinjwa
 
Mleta.mada umeleta analysis nzuri sana kumhusu huyu mheshimiwa Balozi mstaafu. Huko kwake Ifakara ni kijiji fulani utafikiri uko sicily italy. Hilo hekalu lake mbezibeach lina.ukuta wa vioo na pavement mtaa mzima. Yuko mtaa mmoja na.Balozi Peter Kabisa. Kwa kweli huyu mh ana utajiri wa ajabu kupitia utumishi wake serikalini. Mungu si mzee mkumba.asema mbwiga wa mbwiguke
Juzi nimesoma gazeti la Daily News kuwa jamaa ndio Mwenyekiti wa Chamber ya wachimbaji wa madini Tanzania
 
huyu mama anaoneka sio mzalendo kabisa tena ni kirusi ktk maendeleo ya tz.

hata hao wachimbaji wadogo hataweza kuwasaidia ktk maendeleo yao.
 
umeongea vitu vya msingi sana aiseena izo sehemu zote tunapigwa sana..Madini yamekua faida kwa Watanzania wachache aisee...
 
Balozi Ami Mpungwe,mwanadipolomasia na mtumishi wa umma wa miaka mingi.Alikuwa balozi wetu wa kwanza wa Tanzania nchini Afrika Kusini,Ami Mpungwe ndiye aliyekabidhiwa na chama cha ANC kukaa na Nelson Mandela week nzima Manyara National Park wakati Mandela akiwa kwenye mfadhaiko mkubwa wa ndoa yake na Winnie Mandela.

Kwa ukweli Balozi Ami Mpungwe katika harakati na ukombozi wa kusini mwa Afrika hakuna asiyemfahamu,Jongwe Robert Mugabe,Thabo Mbeki,Comrade Pohamba,Jacobo Zuma na kina Kenneth Kaunda ni moja ya watu wanaomfahamu Mpungwe kama mmoja wa "vijana" wa Mwalimu Nyerere aliyepigania ukombozi wa nchi zao na kuufukuzia mbali ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini.

Lakini ukisema utaje watu waliotumbukiza nchi hii katika matatizo ya "uwekezaji wa makaburu" basi jina la mwana Ifakara Balozi Ami Mpungwe halikosi kuwepo,juzi ameonekana kwenye TV na wameitisha kipindi Maalumu ITV kuelezea kupanda kwa bei ya sukari,na kuwaelezea watu wanaoingiza sukari toka nje kama ni "Majipu yaliyoiva muda mrefu na kukosa kutumbuliwa",kauli hii si ya kutolewa na Balozi Mpungwe huyu tunayemfahamu.

Balozi amekuwa kama wakala wa wawekezaji "wanyonyaji" huku yeye akiwekwa kama "Non-Executive Director" ili kulinda maslahi ya wawekezaji hao.

Mfano wa Mashirika ambayo Mpungwe amewekwa kama "Buffer zone" yao dhidi ya Serikali ni kama:
-Tanzanite One
-Multi Choice Tz
-Illovo Sugar hawa wanamiliki Kiwanda cha Kilombero
-Tanzania Breweries
-NBC Tanzania Ltd(1997)
Air Tanzania Ltd(Hii aliiuza kwa South Africa Airways matokeo yake shirika letu likafa kifo cha mende
African Gem Resources
-TANESCO(Ndio aliwaleta Net Group Solutions kwa mtutu na wakaiharibu Tanesco).

Na kwasasa ni mwenyekiti wa Wazalishaji wa Sukari Tanzania,katika mashirika yote hayo aliyokaa hali kwa wazawa ilikuwa mbaya,kule Tanzanite One tumeona jinsi wafanyakazi walivyodhulumiwa na kuishi kwa tabu,mpaka sasa Tanzanite ikaonekana inatoka Kenya na S.Africa.

Sisi washabiki wa mpira tunajua jinsi DSTV ya Multi-Choice ilivyotulipisha kwa dola badala ya shilingi,wafanyakazi wa Kilombero na ugumu wa mazingira ya kazi.

Tunajua jinsi Air Tz ilivyochomekwa ndani ya South Africa Airways na kuiua kabisa,sasa South Afrika ndege yao inakuja mara mbili kwa siku Dar es Salaam wakati ATCL ipo mahututi,"Ujanja Ujanja" huu wa Comrade Mpingwe aligunduliwa na Balozi Abas Sykes wakati huo Sykes ni Mwenyekiti wa bodi ya ATCL akanusa jinsi Mpigwe anavyotaka "kuliuza" shirika,Kwa uchungu Sykes alisema "Mpigwe ni kijana wetu,tumemtuma Afrika Kusini akawe muwakilishi wetu,lakini amegeuka kuwa wakala wa makaburu na kutka kuliuza shirika letu,vijana wa sasa wanawaza maslahi yao badala ya maslahi ya Taifa",matamshi haya yalimfanya Balozi Mpingwe amfungulie kesi Balozi Abasi Sykes na Gazeti la Mtanzania,kesi iliunguruma Mahakama kuu kwa muda.

Huyu ndio balozi Mpingwe,Mwanadiplomasia wa kweli,Jongwe wa kusini mwa Afrika katika harakati za Ukombozi,mwana Ifakara kindakindaki na "wakala" wa makampuni yote ya makaburu Tanzania,anapata wapi kuwaita wengine "majipu" wakati yake mengi watu bado hawajayafumua??
Mkuu naona umeusahau ukoo wa kambale au ule wa panya
 
Achana na Tanzania mkuu, kama marope anaweza kumponda JK na utawala wake ni kipi hakiwezekani!?
...mind you, na JK naye nasikia etui anataka kutumbua majipu.
Teeeeeeeeh teeeeeeeeh, jk atumbue majipu ya wapi?au walio mzunguka?
 
Mie sioni tatizo mtu kubainisha majipu anayoyafahamu ili yatumbuliwe katika.serikali imara.isiyo na simile na majibu,hapa kazi tu
Kweli kabisa na tunasubiri sana jipu la mv dsm litumbuliwe haraka sana
 
image.jpeg

Mnatuchanganya Je, ni Baba au ni Mama.?
Mkuu idawa ni BABA na si vinginevyo,ni huyu hapa
 
Mkuu umenena vyema.
Ila kwa kuongezea katika hayo mazuri kumhusu balozi mpungwe ni pamoja na ukweli kwamba ni Balozi wa "kwanza" Tanzania kustaafu kazi hiyo akiwa katika kituo cha Afrika kusini huku akiwa na umri wa miaka 48.

2. Wakati huo katikati hadi mwisho wa 1900) magazeti la Rai na Mtanzania enzi za akina Ulimwengu na Dr shoo, Rweyemamu na Mbwambo walikuwa hawaivi naye hususan namna ATCL ilivyouzwa kwa makaburu.

3. Serikali ya Che Nkapa ilikuwa katika vifganja vya mkono wake huku akichagua akune wapi, lini na nani
Loh! hivi watu wakiwa na kumbukumbu ya madhambi yako tu popote unapo kwenda utakuwa na raha gani ktk hii Dunia hata kama una japo nayo pia ni haramu,uta hitajika uwe na roho ngumu kama mchawi.
 
Back
Top Bottom