Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,186
- 56
Dr Balali,
Najua umeomba kuwa watu wasikuhesabu kuwa na hatia mpaka ihakikishwe kuwa umefanya makosa. Najua pia kuwa unasisitiza kuelezea mpango wa mafisadi katika serikali wa kutaka kukutoa kafara ili wao waendelee kupeta na kufanya wizi zaidi. Najua pia kuwa pesa za wizi benki kuu zinawahusu viongozi wakubwa kabisa ikiwemo rais mstaafu Mkapa na zilitumika kwenye uchaguzi wa kumchagua Kikwete.
Karibuni pia nimepata habari za plan ya kukutoa roho ili ufe na siri zote ulizonazo za namna wizi ulivyofanyika benki. Kuna wakati nilifikia kukuonea huruma na nikatafuta namna ya kukupa nafasi ya kuishi ili useme ukweli wote na wahusika washughulikiwe.
Inavyoonekana kuwa Tanzania huko wezi na mafisadi wananguvu zaidi na habari zilizopo ni kuwa wahusika wengi wa huu wizi wameanza kukimbia Tanzania kwa msaada wa vyombo vya sheria ili wasipate adhabu yao. Kitendo cha Kikwete kutangaza tena muda wa miezi sita ni usanii mkubwa kabisa wa kufanya watuhumiwa wafute au waondoe vithibitisho vyote vya makosa yao (no wonder Mwizi na fisadi wakili Mkono anataka kukutetea).
Sasa nakugeuzia kibao, Nenda Tanzania damn it. Kama kweli uko safi kama unavyodai, nenda kasafishe jina lako. Tangazia uma wote ni lini unaenda ili watu wajue na ikiwezekana kuwe na ulinzi maalumu ili wanaokutakia mabaya wasipate nafasi ya kukudhulu. Ukienda kimyakimya unawapatia wabaya wako nafasi na usiri mwingine wa kukufanyia mbaya.
Nenda Tanzania na usilete mchezo wa kitoto hapa. Hatutaki hata nafasi moja ya kusikia maneno yako yasiyokwisha. Nilikuwa nakupa breki hapa ila sasa ni mabango tu na wewe na mimi twajuana vyema katika hili. Labda ushauri kidogo, usitegemee kabisa kuwa polisi au serikali ya Kikwete itafanya chochote ili uende ndani. So far muuza rada anatanua tu na kina Patel wanazidi kutajirika.
Nenda Tanzania ukabili mashtaka dhidi yako, kwa sasa wewe ni mwizi na fisadi mpaka uthibitishwe kuwa huna hatia.
Thanks!