Balali nenda Tanzania ukabili mashtaka dhidi yako

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,185
56
Dr Balali,

Najua umeomba kuwa watu wasikuhesabu kuwa na hatia mpaka ihakikishwe kuwa umefanya makosa. Najua pia kuwa unasisitiza kuelezea mpango wa mafisadi katika serikali wa kutaka kukutoa kafara ili wao waendelee kupeta na kufanya wizi zaidi. Najua pia kuwa pesa za wizi benki kuu zinawahusu viongozi wakubwa kabisa ikiwemo rais mstaafu Mkapa na zilitumika kwenye uchaguzi wa kumchagua Kikwete.

Karibuni pia nimepata habari za plan ya kukutoa roho ili ufe na siri zote ulizonazo za namna wizi ulivyofanyika benki. Kuna wakati nilifikia kukuonea huruma na nikatafuta namna ya kukupa nafasi ya kuishi ili useme ukweli wote na wahusika washughulikiwe.

Inavyoonekana kuwa Tanzania huko wezi na mafisadi wananguvu zaidi na habari zilizopo ni kuwa wahusika wengi wa huu wizi wameanza kukimbia Tanzania kwa msaada wa vyombo vya sheria ili wasipate adhabu yao. Kitendo cha Kikwete kutangaza tena muda wa miezi sita ni usanii mkubwa kabisa wa kufanya watuhumiwa wafute au waondoe vithibitisho vyote vya makosa yao (no wonder Mwizi na fisadi wakili Mkono anataka kukutetea).

Sasa nakugeuzia kibao, Nenda Tanzania damn it. Kama kweli uko safi kama unavyodai, nenda kasafishe jina lako. Tangazia uma wote ni lini unaenda ili watu wajue na ikiwezekana kuwe na ulinzi maalumu ili wanaokutakia mabaya wasipate nafasi ya kukudhulu. Ukienda kimyakimya unawapatia wabaya wako nafasi na usiri mwingine wa kukufanyia mbaya.

Nenda Tanzania na usilete mchezo wa kitoto hapa. Hatutaki hata nafasi moja ya kusikia maneno yako yasiyokwisha. Nilikuwa nakupa breki hapa ila sasa ni mabango tu na wewe na mimi twajuana vyema katika hili. Labda ushauri kidogo, usitegemee kabisa kuwa polisi au serikali ya Kikwete itafanya chochote ili uende ndani. So far muuza rada anatanua tu na kina Patel wanazidi kutajirika.

Nenda Tanzania ukabili mashtaka dhidi yako, kwa sasa wewe ni mwizi na fisadi mpaka uthibitishwe kuwa huna hatia.

Thanks!
 
Ninasita Kumshawishi Ballali Kurudi Tanzania Bila Tahadhari ya Juu Sana:
Atangazie umma wote ujue, kuwa anarudi nyumbani.

Tuchukulie pia kuwa Serikali nayo imwache bila ya bugha kwa wakati huu wa miezi sita wakati uchunguzi unapokuwa unaendelea, na (Mwanasheria Mkuu akitafuta sheria)

Tuana hakika gani kuwa mafisadi, serikalini au kwingineko hawatamwondoa roho? Na wakimwondosha, nani atakuwa ameshinda?
 
Je ulisoma katuni hii?

kpleo.jpg

Balali yuko tayari kuongea kuhusu sakata hili hata akiwa na drip lake. Kila mara anataka kujua yule Mama Meghji anasemaje. Lakini kuna viwingu mbalimbali vya kiswahili hutanda kumzuia kufanya hivyo.

Sijui kama messeji inayoletwa na katuni hii ni ya ukweli
 
Je ulisoma katuni hii?

kpleo.jpg

Balali yuko tayari kuongea kuhusu sakata hili hata akiwa na drip lake. Kila mara anataka kujua yule Mama Meghji anasemaje. Lakini kuna viwingu mbalimbali vya kiswahili hutanda kumzuia kufanya hivyo.

Sijui kama messeji inayoletwa na katuni hii ni ya ukweli

Mkuu Kichuguu,

Huyu Balali na Meghji wanacheza mchezo mzuri kwa upande wao so far. Inachoonekana hapa at the end of the day hakuna mtu ambaye atakuwa na hatia. In the process mzee Mgonja na mwenzake wakutaka wenzake wale nyasi wanapeta tu kama hawana akili nzuri vile.

Tanzania hii kunahitajika mapinduzi ya kweli ili kubadilisha mambo! Kikwete naye masikini kila siku kutoa muda tu na vitisho
 
nasikia huyo fisadi mgonja mfupi kaa andazi kachaguliwa kwenye BOT board,kweli huyu JK anatuona hatunazo!
 
Bwana Koba ni kweli si habari za kusikia .Mwafika naamini sasa Ballali siku si nyingi atasema yaliyomfika .Kwa habari ambazo nimezipta hivi punde Mzee anataka kupasua jipu na mafisadi sasa hawalali na Rais ana kiwewe maana hajui atasema nini kwa ushahidi upi .Naomba aseme akiwa US na abakie US maana wao wanasema so far na yeye aseme pia .
 
Mimi nafikiri cha msingi ni yeye kusema, asemee wapi nadhani sio muhimu. Popote atakaposemea tutasikia. Hakuna shaka kwamba atakuwa salama zaidi akisemea akiwa US kuliko akisemea pale Dar. Huko Dar anaweza akanyimwa hata huo ukumbi wa maelezo au hata hao waandishi wetu wakafichwa kabisa wasiende kwenye mkutano wake, nyie mnacheza na watu wanaoitwa mafisadi!
 
Ninasita Kumshawishi Ballali Kurudi Tanzania Bila Tahadhari ya Juu Sana:
Atangazie umma wote ujue, kuwa anarudi nyumbani.

Tuchukulie pia kuwa Serikali nayo imwache bila ya bugha kwa wakati huu wa miezi sita wakati uchunguzi unapokuwa unaendelea, na (Mwanasheria Mkuu akitafuta sheria)

Tuana hakika gani kuwa mafisadi, serikalini au kwingineko hawatamwondoa roho? Na wakimwondosha, nani atakuwa ameshinda?

Ni kweli Mkuu nami namtaka Dr.Balali achukue Tahadhari kubwa kabla ya kutamka yote yaliyotokea pale BOT.Watanzania tumekuwa tunasahau kwa haraka sana!Wale wenye umri kama wangu kumbukeni Uizi ulotokea BOT enzi za Mzee Nyirabu!!Walipoona Ushahidi utawabana/Waumbua waliamua waiunguze BOT ili kupoteza nyaraka muhimu,Sasa watakuwa Tayari kumuua Dr. Balali ili jina Mramba,Mgonja na Mkapa yasitajwe Mahakamani.

Kwani kwenye Report ya Kikwete Mlisikia jina la Deep Green,Meremeta,Tanpower au Tangold? Humo wakurugenzi wake wote ni Wakuu Serikalini,Wananchi waandamane kushinikiza kuona Report kamili ya Ernst & Young.
 
Na zaidi ya hayo Mawado:

Inabidi tkubali tu sasa kwamba serikali nzima sasa hivi imo katika harakati za "Zima Moto."Hizi mbinu zote za miezi sita; sijui kamati za Takururu/InspektaGeneral/Msheria Mkuu, n.k., ni sehemu ya mbinu tu! Hawa watu hawawezi kuukata mkono unaowalisha.

Nimeanza kukubaliana na baadhi ya watu wanaosema kuwa hakuna lolote la maana litakalotokea hapa.

Labda sasa tusubiri 2009, wakati ambapo wapinzani (kama watapenda) kutukumbusha baadhi ya mambo haya ili tuwapigie kura.
 
Niliwaonya na ninawaonya bado.Kusema Lunyungu data zake huwa ni za mtaani ni kujidanganya .JK could be right on the track kama siku ile ile akalisema kamata walioko TZ na fungua mashitaka maana ushahidi wa kwanza anao mkononi na mengine yaje badaye . Ndiyo maana hakutaja deepgreen nk kwa kuwa anajua what is the connection . Tuandike tu lakini issue ya BOT ndiyo imeisha .
 
nasikia huyo fisadi mgonja mfupi kaa andazi kachaguliwa kwenye BOT board,kweli huyu JK anatuona hatunazo!

Bother Koba huyo Avae anaingia kwenye bodi ya BOT kama mtendaji mkuu wa wizara mama ya BOT (BOT technically iko chini ya wizara ya fedha). Ujiko wa moja kwa moja brother siye tulie tu.

Kuna habari kuwamba wakati Meghji anateuliwa kuwa waziri, inasemekana JK alitaka kumweka mtu wake amabye siyo hakuwa na uenyeji pale wizarani; lakini kwa vile Mgonja ndiye alikuwa mwenyeji pale Meghji kwa kujua kuwa ni kilaza katika mambo ya fedha akaomba Mgonja babaki. Ndiyo maana hata baada ya Balalai kumwingiza mkenge ilibidi akamuulize Mgonja na ndiye alimwambia kuwa mama umelizwa!
 
Hivi ndugu zangu, Rais katika tamko lake kaelezea jinsi pesa zilivyochotwa (hazikupotea) kutoka Benki Kuu. Kiuanganisha cha maelezo yake alisema "Kwa kuangalia hayo yote...Rais amefanya yafuatayo"

moja, ametengua uteuzi wa Gavana wa Benki Kuu Bw. Daudi Balali.

...

sasa, kama Raia ameona kuwa Balali anahusika na yaliyotokea EPA, yaani anahusika kiasi cha kuwa wa kwanza kufukuzwa kazi ina maana kuna ushahidi mkubwa wa kumfanya Rais kufikia uamuzi huo.

Sasa, Bi. Mdogo badala ya kumtaka Balali arudi nyumbani, mimi naomba zile 84 Cents zako uzihamishie kwenye Balali afunguliwe mashtaka. Kuwa, kama wanaamini Balali ndiye fisadi numero uno, they should charge him!

Na mimi nitaongezea 15 cents kumpa JK kama serikali yake itamfungulia mashtaka Balali...
 
Hivi ndugu zangu, Rais katika tamko lake kaelezea jinsi pesa zilivyochotwa (hazikupotea) kutoka Benki Kuu. Kiuanganisha cha maelezo yake alisema "Kwa kuangalia hayo yote...Rais amefanya yafuatayo"

moja, ametengua uteuzi wa Gavana wa Benki Kuu Bw. Daudi Balali.

...

sasa, kama Raia ameona kuwa Balali anahusika na yaliyotokea EPA, yaani anahusika kiasi cha kuwa wa kwanza kufukuzwa kazi ina maana kuna ushahidi mkubwa wa kumfanya Rais kufikia uamuzi huo.

Sasa, Bi. Mdogo badala ya kumtaka Balali arudi nyumbani, mimi naomba zile 84 Cents zako uzihamishie kwenye Balali afunguliwe mashtaka. Kuwa, kama wanaamini Balali ndiye fisadi numero uno, they should charge him!

Na mimi nitaongezea 15 cents kumpa JK kama serikali yake itamfungulia mashtaka Balali...

Unajua mimi nimeanza kumtaka Balali aende nyumbani maana nina hakika kabisa kuwa Kikwete na serikali hakuna mtu mwenye ubavu wa kumpeleka mahakamani. Ngoja aende ili amuumbue Kikwete kwa sababu sasa hivi kila mtu anatoa visingizio tu kuwa serikali ipo mbioni kumshtaki wakati wanajua hawana ubavu huo.

Yaani kama ulijua vile, kama nilivyoandika kwenye thread, nina hakika kuwa Kikwete hatafanya na badala yake Balali akifika tu basi Kikwete ataunda kamati nyingine ili hiyo kamati iunde tume ya kusaidia polisi namna ya kumshtaki Balali.

Hiyo tume itachukua miaka miwili kufanya kazi yake. Itabidi kweli nimuahidi Kikwete 84 cents labda atafanya kitu.

Asante.
 
Mkuu Jasusi,

Fungua PM yako, toka jana kuna watu wanataka kukutumia ujumbe mzito huko kuhusiana na hii ishu, niliongea na mmoja wao kwa simu jana mkuu, anasema anashindwa kwa sababu inaonyesha imejaa!

Ahsante Mkuu!
 
Sasa, Bi. Mdogo badala ya kumtaka Balali arudi nyumbani, mimi naomba zile 84 Cents zako uzihamishie kwenye Balali afunguliwe mashtaka. Kuwa, kama wanaamini Balali ndiye fisadi numero uno, they should charge him!

Na mimi nitaongezea 15 cents kumpa JK kama serikali yake itamfungulia mashtaka Balali...
Mzee mwanakijiji, hapa naona kweli umeonesha kuwa wewe ni mzee tena wa kijijini. Nina hakika unaifahamu Tanzania in and out. Unapo-suggest Balali aletwe mahakani Tanzania, sujui unategemea nini, nina hakika unajua justice ya Tanzania.

Unafahamu kabisa kuwa Tanzania myonge hana haki, labda serikali ipende. Mfano unao kwenye issue ya kesi ya Dito, Nyari, Mahalu the list goes on and will go on. Kuna mahakama gani Tanzania ambayo unaweza kusema ina competence ya kushughulikia issue hii, kuna jaji gani ambaye ana freedom kutoka serikalini. Hii kweli ni kudanganyana tu. Huyu Dr Balali akikanyaga tu Ardhi ya Tanzania kuna watu wanaweza kuchekelea kweli, the next hour he will be a dead fish. Hata hao wote waliokimbia Tanzania watarudi kwa furaha na kufanya party kubwa, na hata kumsindikiza kwenye mazishi na kusema as usual....alitoa mchango mkubwa kwa taifa, alikuwa mtu mwema na porojo nyingi.

Lakini hata hivyo as long as anaendelea kuwa na siri hiyo aliyonayo, maisha yake yanaendelea kuwa hatarini. Siri anayoendelea kuwa nayo moyoni inatoa opportunity kwa watu kumshughulikia. huko US nasikia kuwa watu wanaofanya dirty work, ukimlipa dola lakini moja sio rahisi kukataa. Kwa hiyo the faster he blasts the better for him.
 
Kwanini huyu Balali asiseme tuu ukweli? na wala sio lazima aende Dar maana huko wanaweza wakammaliza,hata akimwita Mwanakijiji huko Boston najua Mwanakijiji atachekelea sana na dunia nzima watajua siku hiyo hiyo...mambo yameshaharibika na anaonekana fisadi tuu,bora aseme ukweli tuu nani kachukua chetu na vipi walichukua tunataka ukweli tuu maana tunajua hakuna kitu tutapata back labda vinyumba vyao vya masaki na upanga,tunataka ukweli tuu ili utusaidie kusafisha mafisadi
 
Balali aje Tanzania kujibu mashtaka? He! mnafikiri walioshughulika na marehemu Amina (RIP) wamekufa?
Balali kashasema anataka kurudi, na anasema hivyo kwasababu anafahamu fika kuwa anadeal na mafioso wa Tz; it is his wish kuwa arudi salama..waaapi bwana, tumeona watu wakifariki hapa kwa maelezo yaliyokwisha andaliwa kabla ya matangazo ya kifo..ukiacha cha Nyerere hivyo vingine vitakuwa havina sababu nyingine zaidi ya kumziba mtu mdomo kabla wadanganyika hawajajua ukweli.

Balali akitaka kutusaidia wadanganyika asemee hapo hapo kitandani; news zitatufikia tu hata kama kaongea na mwandishi wa kujitegemea, hii ya yeye kuja mimi naona ni ndoto...just imagine ni watu wangapi wanaloga sasa hivi balali afe! acha mchezo bwana , hii ni bongo!
 
Asirudi Tanzania, njia rahisi ni kutumia technology ya kina Osama na Zawahiri anunue kijicamcorder ajirekodi akitoa maelezo yake yote na kuonyesha hizo evidence then aitundike ngoma kwenye net.
 
Back
Top Bottom