Balali alishakufa hatukuambiwa?

MKjj anafanya analysis kulingana na trend ya matukio ndo maana hata ukiangalia hile posting yake imekaa kimatukio matukio. alikuwa anuliza je kila baada ya sentensi ili kuonyesha trand ya matukio na akamaliza na conclution kutokana na matukio.
 
Posti yangu hii ilikuwa hewani Jumanne ya wiki iliyopita. Makala yangu iliyogusia kifo cha Balali ilitoka Tanzania Daima Jumatano (kesho yake). Balali tumeambiwa amekufa Ijumaa. Sasa kama Balali kafariki Ijumaa iweje miye niingizwe kwenye hiyo conspiracy yenu? Well sorry I broke the news before it happened...
 
Slaa: Tume ichunguze kifo cha Daudi Ballali

na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amependekeza kuundwa kwa tume huru ya kimataifa itakayochunguza mazingira ya kifo cha Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Ballali.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Dk. Slaa ambaye ni Mbunge wa Karatu, alisema umuhimu wa kuundwa kwa tume hiyo unatokana na utata uliozingira habari zote zinazomhusu Ballali tangu alipoondoka hapa nchini Agosti mwaka jana.

Dk. Slaa, mwanasiasa aliyeibua tuhuma kadhaa dhidi ya Ballali, na mmoja wa wanasiasa waliokuwa mstari wa mbele kutaka kurejeshwa nchini, ili aje kujibu tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikimkabili, ikiwa ni pamoja na kusaidia uchunguzi wa wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya BoT, alisema kifo chake kabla ya kukamilika kwa suala hilo, ni pigo kubwa.

'‘Tunaiomba serikali iunde tume ya kimataifa ili ukweli ujulikane. Huyu ni mtu mkubwa, ana siri nyingi za taifa. Anahusishwa na ufisadi. Hatuwezi tukaliacha suala hili likaachwa hivi hivi tu.

'‘Kama serikali imeficha ugonjwa, hospitali na hata hicho kifo ambacho taarifa zake zimepatikana baada ya siku nne, tunataka tume huru iundwe ihusishe majaji na watu wenye heshima katika jamii ya kimataifa," alisema Slaa.

Mwanasiasa huyo ambaye ndiye aliyesoma orodha ya mafisadi mwaka jana na kuibua mwamko wa kipekee katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi, alirejea kauli aliyopata kuisema siku zilizopita kuhusu Ballali na umuhimu wake wa kumrejesha hapa nchini wakati akiwa hai.

'‘Nilipata kusema huko nyuma, na leo narejea tena kulisema hili kwamba, iwapo Ballali atakufa kabla ya hajarejeshwa nchini kujibu tuhuma za ufisadi ndani ya BoT na hata kabla hajahojiwa na Kamati ya Mwanasheria Mkuu inayochunguza kashfa ya EPA, basi damu yake itakuwa juu ya serikali," alisema Slaa.

Alisema mwenendo mzima wa namna serikali na Rais Jakaya Kikwete walivyolishughulikia suala zima la Ballali, kuanzia kuondoka kwake kwenda nje kwa matibabu, kulazwa na baadaye kufa, ni jambo linalotia shaka na kuibua maswali mengi.

Mwanasiasa huyo alisema anaamini haiwezekani Ballali, ambaye ugavana wake ulitenguliwa na si kufukuzwa, aende nje kwa matibabu na alazwe pasipo serikali kupitia Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Marekani, kujua mahali aliko.

Alisema anaamini kwamba gharama zote za matibabu ya Ballali zilibebwa na serikali, kwani hata baada ya uteuzi wake wa ugavana kutenguliwa, aliendelea kubakia kuwa mtumishi wa serikali.

'‘Hiki kiini macho cha serikali kudai eti hawajui alikokuwa amelazwa na anakoishi Ballali, ni ushahidi wa wazi kwamba serikali ilikuwa inaficha jambo.

'‘Walikuwa wakijua aliko, na walifanya hivyo wakijua kwamba iwapo angerejea angeweza kutoa siri kwa kuwataja wahusika wengi, na hivyo kuleta mtikisiko mkubwa serikalini," alisema Dk. Slaa.

Aliilaumu serikali kwa kutoa taarifa nyingi zinazokinzana kila mara waandishi wa habari walipokuwa wakifanya juhudi kubwa katika kufuatilia alikokuwa gavana huyo wa zamani wa BoT.

Alisema uamuzi wa serikali kukaa kimya kwa muda mrefu pasipo kutoa taarifa hata baada ya Ballali kufa, ni ushahidi mwingine wa namna ilivyokuwa ikishikwa na kigugumizi kuhusu suala hilo.

'‘Ninachosema hapa ni kwamba, wakati serikali inapotoa majibu yenye utata na yenye kupingana, haijawahi kusimama na kusema aliyeondoka ni mtu wetu, Mtanzania mwenzetu. Ni kwa nini serikali ilikuwa haifuatilii? Kwa nini ubalozi haukufuatilia? Unaweza kuona namna serikali inavyojaribu kuficha jambo," alisema Dk. Slaa.

Alisema ni jambo la ajabu kwamba, maofisa wa ubalozi wamekuwa wakifuatilia kwa karibu kila mara Watanzania wanapokwenda India kwa matibabu ya moyo, tena kwa watu wa kawaida kabisa na hivyo kuzua maswali ni kwa nini kwa Ballali hali ilikuwa ni tofauti.

Kama hiyo haitoshi, Dk. Slaa alieleza kushangazwa na kifo cha Ballali ambacho kimetokea siku chache tu baada ya kuwapo kwa taarifa za makachero kutumwa kumfuatilia nchini Marekani.

'‘Ni jambo lisiloeleweka sawa sawa na linalopaswa kutolewa maelezo. Haiwezekani tunasikia makachero wamekwenda kumfuata na siku chache baadaye kupitia katika mtandao tunaambiwa amefariki na kisha siku chache baadaye inatangazwa rasmi amekufa. Nini kimemuua? Serikali itujibu," alisema.

Alisema huko nyuma na hata katika mtandao kulikuwa na taarifa za mtu huyo kuwekewa sumu, jambo ambalo serikali pamoja na kutakiwa kulitolea ufafanuzi ilikaa kimya.

Alieleza kushangazwa kwake pia na hatua ya Kamati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayochunguza Kashfa ya EPA, kuwahoji watuhumiwa wengine na wamiliki wa kampuni 22, huku ikimuacha shahidi muhimu Ballali, katika muda wote wa miezi karibu mitano ya kazi yao.

'‘Ni kwa nini wanahojiwa akina Jeetu Patel na wengine wa makampuni 22, na hawa watu hawakuteremka BoT kama Roho Mtakatifu. Ninaamini Ballali angekuwapo angeeleza siri hizo," alisema Dk. Slaa

..................

NADHANI DK. SLAA ANAPOINT NZURI HAPA. KUNA HAJA YA UCHUNGUZI WA JAMBO HILI.
 
NADHANI DK. SLAA ANAPOINT NZURI HAPA. KUNA HAJA YA UCHUNGUZI WA JAMBO HILI.

Hivi kweli alikufa????!!!!! Mimi siamini hadi leo ni mpaka mtu aliyeshuhudia maiti yake ikiwekwa ardhini aje atoe Proof. Jamaa linawezekana linaishi maisha ya raha huko visiwani siye tumebaki na EPA EPA EPA na 3rd parties only!!!
 
Karibu mara kadhaa sasa kila ninapotembea maeneo mbalimbali nchini na kubhatika kutana na baadhi ya wananchi, kila tunapojikita katika majadiliano juu ya EPA wengi wamekuwa wakigusia kifo cha aliyekuwa gavana wetu Daud Balali.

Asilimia kubwa ya wanazania hao wenzagu wamekuwa wakionekana kutosadiki iwapo Balali amekufa. Baadhi wamefikia hatua ya kuelezea sababu za kuamini kwao hivyo ambazo chache nani nazinakilisha hapa:

1. Kama alikufa kwa nini msiba (maiti yake haikuletwa nchini) kwa ajili ya maziko?
2. Kasisi (Hawaelezi wa kanisa gani) amekaririwa na vyombo vya habari akieleza kuwa wakati wa maziko ya balali ambayo alishiriki kuedesha ibada yake hakuweza kuiona maiti yake kutokana na kufungiwa ndani ya sanduku.
3. Kifo chake kiliandaliwa kama sehemu ya kumwondoa katika kitaswira Tanzania lakini bado anaishi nje ya nchi na kwamba amefanyiwa Plastic Surgery- hivyo akiishi kwatika taswira nyingine.

Hizi ni baahi tu ya sababu zinazojitokeza katika majadilino.
 
Haya mambo ni kizungumkuti sasa Wana JF je Mar. Mkuu wa Mkoa wa Tabora? Alikufa Kweli? hebu tulitafakari.
 
Sitakaa kuamini kama ballal kweli alikufa,najua ni mambo ya movie tu hayo ili kuziba macho watu basi,lakini iko siku yataasha,nakuu Hayati baba wa Taifa usemi wake usemao "You can fool some people sometime but not all the people all the time" siku moja watasema yote
 
Balali HAJAFA hupo katika visiwa vya Carribean anakula life kama unataka ingia website ya Carribean usearch mfufua uchumi kutoka Tz. Pia Serikali haijawai kutangaza Balali amekufa
 
Balali HAJAFA hupo katika visiwa vya Carribean anakula life kama unataka ingia website ya Carribean usearch mfufua uchumi kutoka Tz. Pia Serikali haijawai kutangaza Balali amekufa

Website ya Carribean ndio ipi mkuu? Halafu kumbe wanazungumza kiswahili, eh? Manake tusearch mfufua uchumi
 
Sitakaa kuamini kama ballal kweli alikufa,najua ni mambo ya movie tu hayo ili kuziba macho watu basi,lakini iko siku yataasha,nakuu Hayati baba wa Taifa usemi wake usemao "You can fool some people sometime but not all the people all the time" siku moja watasema yote
Wewe unataka kuamini kwa kuona kaburi????!! Acha tabia ya UTOMAS na umwache Balali alale kwa amani . MUNGUaiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.
 
kwani wao kama serikali walikuwa na sababu gani ya kutangaza kifo cha Balali? kwani alikuwa mwajiri wao? mambo mengine bwana!!!!
 
mmh.. haya tumerudi tena huku vipi? sasa hamtaki kuiamini serikali yenu na familia yake?
 
mmh.. haya tumerudi tena huku vipi? sasa hamtaki kuiamini serikali yenu na familia yake?

Tumeiamini serikali tumeishia kulipa milioni 150 kwa siku to Richmond, tumeiamini serikali ndio tumeishia kuwa na madeni hadi kisogoni. Leo hii unataka tuiamini serikali kwa kipi?

Waungwana hebu tupeni data
 
kwani wao kama serikali walikuwa na sababu gani ya kutangaza kifo cha Balali? kwani alikuwa mwajiri wao? mambo mengine bwana!!!!

Umuhimu wa serikali kutangaza kifo chake upo pale pale. Kama kuna watu ambao hata hawafahamiki katika jamii kubwa ya Tz bado serikali mara nyingi kupitia waziri mwenye dhamana husika, hutangaza vifo hivyo, leo ndio ije kwa Balali ambaye alikuwa gavana tena ambaye hadi fedha halali za Tz zilikuwa na signature yake. Yaani hata Kikwete na u-Rais wake, akitaka kununua kitu, anatumia the same note (ambayo yeye ingawa ni Rais, hakuna signature yake) kulipa. Mtu aliyekuwa anasimamia Fiscal Policies za nchi leo unasema ni halali kwa serikali kutojigusa..?? Unless utuambie kuwa na wewe pia ulishiriki kuficha jambo kama Dk. Slaa anavyosema.

Mimi naomba nihakikishe mambo yafuatayo toka kwa wana JF:

1. Hivi President, Vice President & PM, kuna mmoja wao alienda kwenye mazishi ya Balali..?? Na if not, kwa kweli nitakuwa na maswali mengi zaidi ya kujiuliza.
2. Hivi familia yake ambayo ilipewa bahati kwenda kwenye mazishi imerudi bongo mpaka leo au imesikika..?? Kuna wadau mbali mbali nimewasikia wakisema kuwa hawa jamaa ambao walipata chance as si kila mtu alipata bahati ya kwenda kumzika Balali, hawajaonekana kitaa.
3. Kuna mwana JF ambaye amewahi kumuona Balali akiwa kwenye Coffin..??

Binafsi, hayo maswali matatu hapo juu yananipa utata kidogo.
 
Swali jingine kwani lazima kumuona mtu katika jeneza. Wewe unahusika vipi na ndugu zake? tuwe na tamaduni za watu kutafuta ukweli sio gossips, hazitusaidii kitu. gazeti la Majira lilienda ndani zaidi likaandika mahojiano na mdogo wake huko iringa kijijini kabisa na akaconfirm kuwa ndugu yake ni no more na yeye anasimamia maslahi yake hapa nchini.Ikumbukwe kwamba balali alikuwa na uraia wa Marekani na mkewe ni Mganda hapa nyumbani pamoja na kutoka iringa alikuwa TX. Mnataka kuchukua raia wa nchi nyingine kumzika ahh sawa yaani mtu tx alisema anataka kuzikwa hapa. Jambo jingine hivi mnajua kwamba huyu kabla ya kifo chake safari za afrika Kusini kwa matibabu zilikuwa nyingi. Mnasema tu. nani ashiriki kuficha kifo cha mtu kwa sababu gani hasa. Mliona maiti ya wako jacko?Kama mnakuwa na haja naye kwanini msitafakari maisha wakati mwingine unacheka madaktari wazima wanatengeneza conspiracy story ili wawini uanasiasa. kweli siasa si hasa!
 
Back
Top Bottom