Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,731
- 40,836
Kwa vile Balali alipelekwa kwenye matibabu huko Marekani, matibabu ambayo yalisababisha alazwe kwa muda mrefu;
Kwa vile hali yake haikuwa nzuri na iliendelea kuwa mbaya hadi kumlazimisha amuombe Rais amruhusu aachie ngazi
kwa vile Rais hakukubali Balali ajiuzulu na baadaye kumtimua kazi akiwa mahututi kitandani;
Kwa vile Rais aliamua kuunda kamati maalumu ya kuchunguza wizi wa EPA na mhusika mkuu wa sakata hilo alidaiwa kuwa ni mahututi;
Kwa vile kwa muda mrefu sasa viongozi wetu wamekuwa wakituambia kuwa hawajui aliko Balali jambo ambalo limerudiwa tena hapo jana na Waziri Mkuu
Kwa vile Balali alikuwa mgonjwa mahututi, hana kazi, na serikali haijui alipo
Hivyo basi, madai ya serikali kuwa wakimtaka watampata hayana ukweli; Kuwa serikali ikimhitaji mtu wasiyejua alipo wataweza kumpata kwa haraka, kimsingi madai hayo ya serikali na kauli hizo hazina msingi wowote.
Kwa sababu,
Balali alishafariki na kuzikwa huko huko majuu baada ya hali yake kuwa mbaya. Na kwa vile serikali haijui alipo hawana njia yoyote ya kujua liliko kaburi lake na hawana ujuzi wowote kuwa ni mzima au ni marehemu.
Hivyo, basi anayesubiri kumuona Balali akirudi Tanzania mzima anasubiri mvua jangwani!!
RIP Balali!!
NB: Kama ni mzima bado, serikali imejuaje wakati hawajui aliko?