Elections 2010 Balaa ya hongo Chadema

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,127
headline_bullet.jpg
Takukuru yakamata mgombea aliyejitoa
headline_bullet.jpg
Adaiwa kuwa alishawishiwa kwa fedha
headline_bullet.jpg
Awekwa chini ya ulinzi Makao Makuu Dar

Chadema%2816%29.jpg

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Makao Makuu jijini Dar es Salaam, imemkamata na kumhoji aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Jimbo la Musoma Vijijini, Michael Makenji, kwa tuhuma za kupokea rushwa.
Makenji anadaiwa kupokea Euro 1,000 (Sh. 1,850,000) kisha kujitoa katika kinyang’anyiro hicho.
Habari zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa Makenji alihojiwa na maofisa wa Takukuru juzi jioni kuhusiana na tuhuma hizo na kwamba hadi jana alikuwa akiendelea kushikiliwa kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Makenji ni miongoni mwa wanachama wa Chadema waliochukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea katika jimbo hilo, lakini hakurejesha fomu kwa msimamizi wa uchaguzi hivyo jimbo hilo kubaki na mgombea pekee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nimrod Mkono.
Habari zinaeleza kuwa Makenji baada ya kutorejesha fomu kwa msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Musoma Vijijini, alikwenda katika ofisi za Makao Makuu ya Chadema jijini Dar es Salaam, lakini baadaye baadhi ya wanaChadema walimtilia shaka kutokana na mawasiliano kati yake na baadhi ya watu.
Chanzo chetu cha uhakika kimebainisha kuwa, baada ya wanaChadema kumtilia shaka, walimuweka chini ya ulinzi na kukuta taarifa mbalimbali alizokuwa anatumiana na watu hao kupitia ujumbe mfupi wa simu.
Taarifa za ndani ya Chadema zinasema kwamba baada ya mgombea huyo kuhojiwa na kupekua kwenye simu yake ya mkononi, alipatikana na ujumbe kadhaa zilizoashiria kwamba kulikuwa na mkono wa mtu katika kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha ubunge.
Miongoni mwa jumbe hizo (sms) ambazo ziko sehemu ya zilizotumwa zilisema:
“Mzee ameshanikatia tiketi ya kwenda Dar sasa muhimize amalizie kiasi kilichobaki maana hali yangu ya kiuchumi si nzuri.”
Nyingine ilisomeka: “Tumeshamaliza kama tulivyokubaliana.” Na mwingine ukisema: “Niko Makao Makuu ya Chama niko chini ya ulinzi.” Ujumbe huo ulionekana kujibiwa hivi: “Nani kakwambia uende huko watakuua. Siwezi kuja huko kukutetea.” Simu iliyotuma ujumbe huo unadaiwa ni ya kiongozi mmoja mwandamizi wa chama hicho.
Chadema baada ya kuona hali imekuwa hivyo, waliamua kuwasiliana na Takukuru na baada ya muda mfupi, maofisa wa taasisi hiyo walifika na kumchukua Makenji.
Hata hivyo, Takukuru haikuwa tayari kuthibitisha tukio hilo licha ya jitihada za NIPASHE kuwatafuta maofisa wake tangu juzi jioni.
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, juzi jioni alisema alikuwa katika mkutano mjini Arusha na kuahidi kuwa angepiga simu baadaye kutoa ufafanuzi. Hata hivyo, hadi tunakwenda mitamboni hakufanya hivyo.
Ofisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwaya, jana alisema kuwa maofisa wa Makao Makuu wangeweza kulizungumzia, lakini mwandishi wetu alipokwenda katika ofisi hizo, aliambiwa kuwa ofisa anayeshughulikia kesi hiyo alikuwa katika kikao.
Hata hivyo, ofisa huyo aliyetambulika kwa jina moja la Kassim, alipoulizwa baadaye jioni, alisema: “Sina comment (sina la kusema) katika hilo, labda kama ungefuata zile taratibu zetu za kila siku kwa kupitia kwa ofisa Uhusiano wetu hadi kwa Mkurugenzi Mkuu.”
Dk. Hoseah alizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu majira ya saa 18:20 jana jioni, alisema: “Sina taarifa, kwa sasa nipo nje ya Dar es Salaam, nani amekuambia hayo.”
Uongozi wa Chadema ulipoulizwa kuhusiana na taarifa hizo, ulithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kwamba mtuhumiwa (Makenja) alikiri kupewa kiasi hicho cha pesa.
“Kimsingi ni kwamba Idara yetu ya Ulinzi na Usalama ilimhoji mgombea wetu na akakiri kupewa fedha hizo, tena kwa maandishi ndipo tukawasiliana na Takukuru kwa hatua zaidi…lakini tunawasiliana na mamlaka mbalimbali ili kuona hatua stahili za kumchukulia kwa sababu amekiuka kanuni na sheria za uchaguzi,” alisema Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika.
Kufuatia hali hiyo, Mnyika alisema chama hicho kimelazimika kuwaandikia barua wagombea wake ambao hawakurudisha fomu ili kujua tatizo lililokwamisha kufanya hivyo.
Alisema chama kimeamua kuchukua hatua hiyo ili kubaini kama kinafanyiwa hujuma na kwamba watakaobainika kutorudisha fomu makusudi, kitawachukulia hatua kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.

CHANZO: NIPASHE
 
Ni muda muafaka pia kwa CHADEMA kumkatia rufaa Mkono kwenye NEC kama walivyofanya kwa akina Membe na wenzake.
 
So mtoa NA MTOAJI MATATANI
OK NTAFURAHI MKONO ASIPOSHIRIKI UCHAGUZI PIA
 
Ila nimewaza sana nakuona kuwa kama mtu huyu kalubuniwa kiasi hicho na hizo senti je angepewa ubunge si angeweka pesa mbele tu ,duh safari ndefu tunayo
 
Ila nimewaza sana nakuona kuwa kama mtu huyu kalubuniwa kiasi hicho na hizo senti je angepewa ubunge si angeweka pesa mbele tu ,duh safari ndefu tunayo
=====

Kuna mgogoro hapa. Ndani ya CCM wilaya wanalalamika kuwa Mkono kwa kupita bila kupingwa wamekosa ulaji kwa sababu hawatapata mgawo wa fedha toka Makao Makuu kwa ajili ya Kampeini wakati waliishaweka mipango ya mafuta hewa, chakula hewa, pombe hewa, photocopy hewa, n.k. Kwamba, badala ya kumkamua Mzee Mkono ili kumpigia Kampeini, yeye amempa mgombea euro 1,000 biashara ikaisha, wao wakaambulia bure. CCM ndio wamewatonya Chadema na TAKUKURU. Hali hii iko majimbo yote yanayosemekana yana wagombea waliopita bila kupingwa.

Rushwa ya Tanzania ina mizizi mirefu sana.
 
Kaaazi kwelikweli.
 
so what next,sijuhi busara au sheria ijukue mkondo wake?
 
Kaaazi kwelikweli.

yes, it is true, katibu wa ccm wa musoma vijijini ndiye aliyekuwa amemfanya mkono kama ATM.

Chama cha mapinduzi tunasikia kimeumia sana kuona Mkono amepita bila kupingwa! HAKIKA CHAMA CHAMA MAPINDUZI KINAWAKAMUA WAGOMBEA WAKE,
MKNO AMEFANYWA KAMA ATM YA CCM!
 
Ila nimefurahi kusikia kitu kimoja -- kwama Chadema ndiyo waliomkabidhi mgombea wao kwa Takukuru. Hivi CCM wammewakabidhi kwa Takukuru wagombea wao wangapi walitoa rushwa? Big up Chadema. You have shown you can really fight ufisadi.
 
sijui sijaelewa??

Ina maana huyu jamaa amehongwa na kiongozi wa chadema asigombee??
 
Government gave Takukuru some teeth to bite, but now they are suffering
from toothache
 
money can buy anything!!!!!!!!!!!! tehetehe
hata CHADEMA? rushwa ni mbaya sana na inaonekana imejichimbia mioyoni mwa watu
 
Tuhuma kwa mgombea wa CCM toka kwa Upinzani? sijui kama Takukuru watatimiza wajibu wao stahili. Ngoja tuone mazingaombwe.
 
Ila nimefurahi kusikia kitu kimoja -- kwama Chadema ndiyo waliomkabidhi mgombea wao kwa Takukuru. Hivi CCM wammewakabidhi kwa Takukuru wagombea wao wangapi walitoa rushwa? Big up Chadema. You have shown you can really fight ufisadi.
Big up CHADEMA kwa uzalendo wa kupiga vita rushwa hata kama linahusu memba wenu mko tayari kumkabidhi takukuru.

Vyama vingine viige mfano huu ikiwamo sisi M.
 
Tangu ninafuatilia kesi za TAKUKURU sijawahi kusikia wamemtia nguvuni aliyepokea rushwa. Labda ndio kisa na mkasa wanashindwa kesi zote. Hii ya CHADEMA itawavuriga zaidi kwa sababu mbili. Kwanza hawana uzoefu na kushughulikia wapokea rushwa, lakini pili tuhuma za CHADEMA kwa mtu wa CCM si rahisi zikafanyiwa kazi na wateule wa Mwenyekiti wa CCM (Dr Hosea).
 
jamaa kachaPA SANA PESA ZA TIRDO KULE MSASANI MPAKA KAJENGA BENKI YAKE MWENYEWE...............
 
Ila nimewaza sana nakuona kuwa kama mtu huyu kalubuniwa kiasi hicho na hizo senti je angepewa ubunge si angeweka pesa mbele tu ,duh safari ndefu tunayo

Hata mimi nimeshangaa sana kwa yeye kurubuniwa kwa hela ndogo kiasi kile. Inawezekana alikuwa anajua kuwa hatashinda kwenye uchaguzi, lakini hakutakiwa kuuza utu wake katika swala zito kama lile kwa hela yoyote ile. Kujitoa kwenye kinyanganyiro kumemfanya mpinzani wake apate nguvu ya kwenda kuikampeinia CCM sehemu nyingine za nchi.
 
Hii ukiichunguza kwa makini, utabaini jinsi CHADEMA wasivyo makini na hence hawafai kupewa kuongoza.
 
Back
Top Bottom