masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,882
- 13,171
Huyo msichana kama likuwa anafanya ukahaba na mtoto mkonono basi ni wa kumhurumia zaidi kuliko kushitaki.Simtetei huyo mama kwa kosa alilolifanya, atalipia kosa lake kadiri ya taratibu za kisheria au za kijamii. Nisichokubaliana nacho ni udhalilishaji wa namna alivyomatwa, karibu kuchaniwa nguo, kupigwa picha na kusambazwa kwa picha zake. kuna watu ambao tayari maisha yamewadhalilisha, tusiwaongezee mzigo zaidi. Ficheni basi hata sura yake, isijetokea kwamba mwisho wa siku, hana makosa lakini sura yake imeshasambazwa kwamba ni kahaba.
Hali ya maisha mbaya sana kwa watu wa kipato kidogo au wasio na kazi.
Ukiona hivi basi hata ndugu wa karibu hawana msaada kwa kinda huyu.
Msichana anatoka kutafuta hela ya chakula na maziwa bila kujua hatari ziambatanazo na shughuli hiyo, achilia mbali hatari kwa malaika mtoto huyo.
Hii imenisikitisha sana.