Balaa: Mke wa Mtu Afumwa Akijiuza Usiku na Mtoto Mkononi

kwa nini akamatwe na askari wanaume wakati sheria hairuhusu.

na hayo ndiyo maisha bora ya jk na kauli yake kuwa ukitaka kula lazima uliwe kwanza sasa kosa lake lipi.
 
Najaribu kufikiria ila sipati jibu, wakati huyo mwanamama anapoenda kuliwa tundi sijui hako kachanga huwa anazuka nako...!!!
 
Maisha ni magumu, hospital hela, maziwa ya mtoto hela,nyumba anayoishi inahitaji kodi uji wa ulezi wa mtoto hela kwa ujumla kila utakachogusa ni hela na sehemu ya kupatia kipato hakuna,siungi mkono kitendo alichokifanya cha kuzunguka na mtoto mtaani lakini pia anahitaji huruma huyo mama.

Wenye "akili" wanadai majibu ya shida zote hizo anayo Kinana!!
 
Si vizuri kumnyanyasa mama na mtoto kiasi hiki, wangewapa msaada hata wa kuwakalisha mbele na mtoto kuwa salama.
 
Kumuona tu huyo mtoto kwenye picha nimeumia sana hadi nimeshindwa kuchangia.
 
Mleta mada umeharakisha kusema mke wa mtu. Hapa kitu tunachoona ni mama mtoto. Kuna akina mama wana watoto huku wametelekezwa na wazazi wenzao, na ninaona huyu ni mmoja wao. Itawezekanaje umwache mumeo nyumbani usiku utoke kwenda kujiuza? Hapa ndio wanaume tuone madhara tunayosababisha kutelekeza wapenzi wetu na kukimbia mzigo wa kulea watoto.

NGOs zinazosema zinasaidia watu wasiojiweza, please huyu mama anahitaji msaada wenu.
 
pengine hana mume, ila tu mzazi mwenzie, ambaye hachukui majukumu yoyote kama baba/mume.
hata hivyo, maisha ni magumu kweli...
 
Dunia ina mambo mengi. Usikute amekopa kwenye FINCA na mumewe hajui, sasa kazi ipo hapo ndio kakamatwa.

Ninapoona hivi huwa naumia. Tunakula na kushiba na familia zetu wakati watu wanahangaika mitaani. Jamani tuwe na huruma. Hao waliomkamta kweli wana watoto? wana familia? utu uko wapi? hivi kitendo cha kuzunguka na mtoto huwezi kujiuliza kwa nini? wangemuita pembeni kumhoji ingekuwaje? sijafurahia kabisa! hivi kama angekuwa malaya mzoefu angeenda na mwanae? Hapo hakuna mume anasimama yeye kama yeye.

Tuombe sana Mungu azidi kutupa pumzi!
 
Napata shida sana kuamini kuwa huyo dada alikuwa akijiuza (akiwa na mtoto hivyo). Najiuliza, hivi wapo wateja ambao watakuwa na mzuka wa kuchukua huyo dada na mwanae na kwenda nae gesti kwa ajili ya ngono....mtoto anawekwa wapi?

Mimi nahisi alikuwa anazunguka kuomba omba tu kama wale tunaowaona mara kadhaa pale mataa ya moroco na kwengineko. Hili la kujiuza na mtoto bado sijalikubali.

Na hizi picha hazijamtendea haki kwa sababu yoyote ile.
 
Simtetei huyo mama kwa kosa alilolifanya, atalipia kosa lake kadiri ya taratibu za kisheria au za kijamii. Nisichokubaliana nacho ni udhalilishaji wa namna alivyomatwa, karibu kuchaniwa nguo, kupigwa picha na kusambazwa kwa picha zake. kuna watu ambao tayari maisha yamewadhalilisha, tusiwaongezee mzigo zaidi. Ficheni basi hata sura yake, isijetokea kwamba mwisho wa siku, hana makosa lakini sura yake imeshasambazwa kwamba ni kahaba.

i support what u'v said. GOD help her and her beby please, let her forget by giving smooth way of handling her life. In JESUS CHRIST NAME, i'v pryd Amen.
 
kwa nini akamatwe na askari wanaume wakati sheria hairuhusu.

na hayo ndiyo maisha bora ya jk na kauli yake kuwa ukitaka kula lazima uliwe kwanza sasa kosa lake lipi.

I LIKE THIS! Slogan ya magamba " ukitaka kula lazima uliwe" tumeiona hata kwenye uchaguzi wao ulipita. Nyingine ilikuwa " bia zake mnywee ila gesti usiende" hahaaaa! Nilijiuliza hivi akishalewa atajuaje anapelekwa gesti?
 
Binafsi imenisikitisha sana.

Hapo wanasema ilikuwa ni kamata-kamata, ambayo naamini kuwa polisi wetu wengi wakiwa kwenye zoezi kama hilo hawatumii akili hata kidogo ya kuhoji kwanza kabla ya kukamata. Inawezekana alikuwa kwenye kijiwe na mashoga zake wakipunga upepo basi polisi wakamchanganya. Ila wangekuwa na busara kidogo wangemuoji kabla ya kumsweka kwenye pick-up.

Naamini kabisa kuwa hakuwa anajiuza akiwa na mtoto. Pengine alimchukua kama kinga ili asikamatwe au aonewe huruma. Kuna maswali mengi kuliko majibu.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Hivi kwanini wateja wao huwa hawakamatwi. Hapa naona kuna tatizo katika mamlaka zetu kushughulika matatizo katika jamii yetu. Wangejiuliza maswali yafuatayo kabla ya kukimbilia kuwakamata hawa dada na binti zetu. Ni mambo gani yanayopelekea kuongezeka kwa tabia ya wadada kujiuza? Je biashara hii ina madhara gani kwa jamii yetu. Je kuna njia ya kuwakomboa watu hawa zaidi ya kuwakamata? Mtazamo wangu ni kwamba wadada wakiacha kujiuza UBAKAJI utaongezeka asilimia 500
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom