tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,039
Sheikh tapeli na muongo, angeanza tena kwa msisitizo kuzungumzia HAKI ningeamini anasimamia misingi ya Uislamu.Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir amesema Baraza Kuu ya Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) itaendelea kusimamia maslahi ya Nchi ambapo ametoa wito kwa watanzania kuendelea kuwa wazalendo na Taifa lao pamoja na kuilinda amani.
Mufti ameeleza hayo leo wakati akizungumza na baadhi ya viongozi wa dini na serikali wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Njombe ambapo pia amesema miongoni mwa kazi ya BAKWATA ni pamoja na kuhimiza watu kuilinda amani na kuwa wazalendo na taifa tofauti na wengine wanavyodhani kuwa Baraza hilo linatumiwa na serikali.
Soma pia: Mufti Abubakar Zubeir: BAKWATA si vibaraka wa serikali
View attachment 3488017
"Tunazungumza sana swala la amani na uzalendo kwasababu tunaijua nchi ilivyo sasa akili ya watu wengine wanafikiri labda sisi ni vibaraka yani serikali inatutumia nendeni huko mkaseme hivi, a a sisi hatutumiwi na serikali tunajua umuhimu wa kutengeneza jamii ambayo inajua umuhimu wa kuwa mzalendo katika nchi yako" amesema Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir amesema Baraza Kuu ya Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) itaendelea kusimamia maslahi ya Nchi ambapo ametoa wito kwa watanzania kuendelea kuwa wazalendo na Taifa lao pamoja na kuilinda amani.
Mufti ameeleza hayo leo wakati akizungumza na baadhi ya viongozi wa dini na serikali wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Njombe ambapo pia amesema miongoni mwa kazi ya BAKWATA ni pamoja na kuhimiza watu kuilinda amani na kuwa wazalendo na taifa tofauti na wengine wanavyodhani kuwa Baraza hilo linatumiwa na serikali.
Soma pia: Mufti Abubakar Zubeir: BAKWATA si vibaraka wa serikali
"Tunazungumza sana swala la amani na uzalendo kwasababu tunaijua nchi ilivyo sasa akili ya watu wengine wanafikiri labda sisi ni vibaraka yani serikali inatutumia nendeni huko mkaseme hivi, a a sisi hatutumiwi na serikali tunajua umuhimu wa kutengeneza jamii ambayo inajua umuhimu wa kuwa mzalendo katika nchi yako" amesema Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir
Watu walianza kufunga tarehe 19 so leo ni exactly Ramadhani 30. Hakuna mwezi wa kiislam wenye siku 31 so kesho ni Shewal 1, 1447 hakuna wa kuzuia siku kuu Kesho kuna wakati miezi ndo inaletaga kisingizio hasa yenye siku 27, 28, au 29 lakini one’s ukishafunga mpaka Ramadhani 30 basi mwezi unakua umeisha kwa Siku ya Jana hata Sunni/ Saudia Hawajauona mwezi hakuna mtu yeyote ambaye anaweza ku influence hili jambo!Lazima eid iende jmosi. Maelekezo kutoka juu
Wadanganye kondoo wenzakoWatu walianza kufunga tarehe 19 so leo ni exactly Ramadhani 30. Hakuna mwezi wa kiislam wenye siku 31 so kesho ni Shewal 1, 1447 hakuna wa kuzuia siku kuu Kesho kuna wakati miezi ndo inaletaga kisingizio hasa yenye siku 27, 28, au 29 lakini one’s ukishafunga mpaka Ramadhani 30 basi mwezi unakua umeisha kwa Siku ya Jana hata Sunni/ Saudia Hawajauona mwezi hakuna mtu yeyote ambaye anaweza ku influence hili jambo!
wewe ndie kondoo...mwezi wa kiislamu una siku 30 na leo alhamisini tarege 30 kiarabu au mwezi wa kiislamu, kwa hiyo kesho ni tarehe moja....Wadanganye kondoo wenzako
Vyote hivyo hutoka serikalini, mpaka ulinzi.Mshahara, marupurupu, gari, mafuta, kodi ya nyumba n.k wa shehe mkuu unatoka serikalini au ni michango ya wanachama wa BAKWATA?
Sijawahi kuwa kondoo wala MbuziWadanganye kondoo wenzako
Mnajuwa umuhimu wa AMANI ambayo wananchi wake hawana HAKI ya kufanya maamuzi yanayowahusu?tunajua umuhimu wa kutengeneza jamii ambayo inajua umuhimu wa kuwa mzalendo katika nchi yako
Heshima mkuu 'CHIEF'; najuwa na kukumbuka vyema sana kwamba tuliyamaliza kule.Bakwata ni jumuia ndani ya CCM kama ilivyo UVCCM, na jukumu la Bakwata ni kuwaghilib Waislamu waiunge mkono CCM nyakati za uchaguzi.
Uko sahihj,CCM hii sasa imekuwa genge maslahi linalotumia vyombo vya dola kuendelea kutawala kidhalimu na hata taasisi kama Bakwata wameigeuza kuwa chombo chake cha kuleta ushawishi kwa Waislam ili waiunge mkono.K Kwa hali ya CCM kuwa chama dola na mapungufu yaliyopo kwenye Katiba ni vigumu kuiondoa CCM madarakani kwa njia za kistaarabu.Heshima mkuu 'CHIEF'; najuwa na kukumbuka vyema sana kwamba tuliyamaliza kule.
Lakini taasisi hii inanikumbusha vizuri zaidi kuwa mfano mzuri na unaoeleweka kirahisi kuwa miongoni mwa "makosa aliyofanya Mwalimu Nyerere"; kwa kuchukulia tu dhana ya mtizamo wa juu juu wa swala lenyewe. Lengo la kuundwa kwa taasisi hii na inavyotumika sasa hivi ni tofauti kabisa.
Ni vilevile CCM ilivyogeuka sasa, ni vigumu sana kumshawishi yeyote kwamba chama hicho kiliundwa ili kije kuwa kama kilvyo sasa.
Imenilazimu niliseme hili kustua tu akili yako bila kutafuta mjadala juu yake